Tanzania ya Leo ina katiba na sheria vinavyosimamia usawa wa watoto na haki zao.Ikitumika sheria ya kidini kuwanyima urithi watoto shauri likienda mahakamani watoto watapata urithi.
Kifupi walifunga ndoa ya Bakwata ambayo hamrithishi mwamamke mali. Hivo pointi ya msingi ni moja tu wosia na warangi lazima wafoji ndo maana hawataki kufungua nyumba.
Kupeleka kesi ya mirathi Bakwata au kwa Mali ya Wakf kwa Zanzibar inategemea wenyewe familia kwani kuna commission kubwa pale wanachukua - niliwahi kusikia zaidi ya asilimia ishirini ya thamani ya mirathi. Asilimia kubwa ya akina sisi huwa hatupendi kwenda mpaka pale iwapo lazima (hasa unapokuwa na wanafamilia watata au wengi kama vile matumbo tafauti).
Mirathi ya kiislamu ni taaluma na siyo kila sheikh anaweza kurithisha ipasavyo, pia calculations zake zinahitaji umakini kidogo.