Uchaguzi 2020 Baada ya Vyombo vya Habari kuminywa kutoa habari za CHADEMA, wagombea Ubunge wabuni mbinu mpya ili kuwafikia wapiga kura

Kama ndio hivyo SASA naanza kuelewa ni Kwa nini vyama vingi ndivyo uchagua mgombea na kumpandikiza Kwa wananchi ili wampigie Kura...Wenye uelewa katika Siasa hasa Viongozi hawana Imani na machaguo ya wananchi au uwezo wao wa kujichagulia Viongozi Bora.
 
Kupita bila kupingwa ipo tangu siasa za vyama vingi mkuu!! Kuna uwezekano ulikuwa bado kinda ndiyo maana hujui kuwa kupita bila kupingwa ilikuwapo!

Kwa sasa chini ya Magufuli imekuwa ni fashion kwa wanaccm. Kabla ya Magufuli kuwa rais, ukiacha Magufuli mwenyewe akiwa mbunge kuhujumu uchaguzi ili apite bila kupingwa, ni wagombea wachache sana walikuwa wanapita bila kupingwa. Chaguzi karibia zote chini ya awamu hii zimetawaliwa na wagombea kupita bila kupingwa, yaani tabia binafsi ya Magufuli kupita bila kupingwa, ndio imegeuka kuwa tabia ya wanaccm wote kwenye chaguzi zote za nchi hii.
 
Ila sio fear kwa anachofanya rais wetu? Sasa hivi ukitaka kupigwa faini na TCRA we rusha vipindi vya wapinzani.
ANANICHUKIZA HAPA TU
Kama hakuna maneno ya chuki na matusi wewe rusha tu ,hakuna atakae kusumbua
 
Sema CCM kwa sasa imekubalika zaidi kuliko awamu ya nne. Huo ndiyo ukweli uliona watia nia tu walikuwa 44 elfu hivyo wagombea wazuri walikimbilia CCM. Siku za nyuma wakikosa CCM walikuwa wanakimbilia upinzani mwaka huu siyo sana. Hivyo wagombea wengi wa upinzani ni magalasha hata kujaza fomu ni shida. Angalia hapa chini
 
Kama hakuna maneno ya chuki na matusi wewe rusha tu ,hakuna atakae kusumbua

Mwenye tafsiri ya chuki na matusi ni mgombea urais wa ccm, vichekesho hivi viko Tanzania tu.
 
Unafikili mimi mgeni kwenye hii awamu ya kishindo? Vyote vilenga kuua upinzani hata sisi CCM tunakwazwa na hii tabia mbaya.TUNATAKA KUSHINDANA MBIO NA MTU MWENYE MIGUU MWENZETU SIO MUMKATE MIGUU THEN MUMUITE NI MSHINDANI HALALI
 

Kwa sasa kila mtu anajua ukiwa ccm una uwezo wa kutangazwa mshindi, sio kwa sababu ccm ina nguvu au kukubalika sana, bali ni kwakuwa mwenyekiti wake anaweza kuiagiza tume ya uchaguzi imtangaze mgombea wa ccm. Achia mbali mazingira ya kuweza kupita bila kupingwa. Ni vigumu kwa sasa wagombea kutoka ccm kwenda upinzani, kwani kuwa upinzani ni kutaka kudhalilishwa na vyombo vya dola, kuhujumiwa shughuli zako za kukuingizia kipato, kutekwa na hata kuuwawa. Ni mwanaccm gani anaweza kumudu madhila hayo?
 

Yaani wewe ndio unajua haya leo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…