Mkuu wala usinitake radhi kwani huwa sichoki kusoma mabandiko yenye pointi za msingi kama hili lako, hata liwe refu vipi. Mkuu haya mabadiliko yameanza ya kuzuia elimu ya uraia kipindi hiki Magufuli alichokuwa rais. Ni kama wananchi wameshurutishwa kuamini kuwa elimu ya uraia ni adui wa maendeleo. Taratibu kwa sasa tunaanza kwenda kwenye nchi ambayo viongozi wanafanya wanachoona ni sawa, na sio wanachoona wananchi ni sawa. Wananchi wamesadikishwa kuwa mtatuzi wa matatizo yao ni rais na wale anaowamini tu.
Kwa sasa ni ngumu kutoa elimu ya uraia bila kukutana na vyombo vyenye udhibiti kwa nia ya kudhibiti elimu gani inatolewa kwa wananchi. Ni kweli kwa sasa wananchi wanaweza wakakaa kimya, kwa huu uhuni unaofanywa na taasisi za kimamlaka dhidi ya kundi fulani wakidhani watakuwa salama, ila athari za kuwa na viongozi ambao hawako kwa ridhaa ya wananchi lazima itawarudia tu, tena sio muda mrefu kutoka sasa. Kutaanza kutoka amri za shuruti kwa wananchi, kwani hawana tena uwezo wa kuhoji, na hapo ndio kilio kitashika kasi. Unapoanza kuona kwenye kampeni burudani ndio kivutio cha mkutano na sio sera za mgombea, kuwa makini sana.