Baada ya walimu walio kuwa wamejificha kwenye Ofisi za Elimu Msingi, Sekondari na TSD ndani ya Halmashauri kutimuliwa sasa Idadi ya walimu Waongezeka

Baada ya walimu walio kuwa wamejificha kwenye Ofisi za Elimu Msingi, Sekondari na TSD ndani ya Halmashauri kutimuliwa sasa Idadi ya walimu Waongezeka

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Nianze kwa kumpongeza Prof Adolf Mkenda kwa kazi nzuri aliyoifanya Baada ya walimu walio kuwa wamejificha kwenye Ofisi za Elimu msingi, sekondari na TSD ndani ya Halmashauri kutimuliwa sasa Idadi ya walimu wa kufundisha madarasa ni Waongezeka.

Hii ni baada ya malalamiko mengi kuandika Jf sasa Hali imetulia na walimu wa kufundisha darasani msingi na sekondari wameongezeka na Hata serikali ikiajiri itaajiri walimu wachache.

Kazi iliyobakia ni kupunguza Idadi ya maafisaelimu waliopo imara ya Elimu msingi na sekondari ikiwa ni pamoja na kufunganisha hizo idara na kuunda idara moja ya Elimu ndani ya Halmashauri moja.

Prof Mkenda kasi unayokwenda nayo inaridhisha na Uko vizuri.

Pili muundo mpya wa Elimu mkuu wa idara aside na kiwango cha chini ya PhD Ili aweze kusimamia Elimu ipasavyo.

Kuna walimu walikuwa wamefichwa kwa afisaelimu Mkoa ambao walikuwa hawana barua Za uteuzi nao warudishwe madarasani haraka iwezekanavyo.
 
Kwani zile ajira za waalimu zimeyeyuka?
 
Eti serikali itaajiri walimu wachache. Kwamba walimu sasa wamepatikana. Ni kichekesho. Inaonekana mleta mada hujui kwa kina tatizo la upungufu wa walimu lilivyo.

Pili, Waziri Kama ana uthubutu na anataka shule ziwe na uwiano mzuri wa walimu maeneo ya vijijini basi AHAMISHE WALIMU WALIOLUNDIKANA MAENEO YA MIJINI awapeleke vijijini. Kwa hili utaona jinsi ambavyo nchi hii haina upungufu mkubwa wa walimu, Namaanisha tatizo siyo kubwa km tunavyodhani.

Mara nyingi upungufu unaoimbwa references inayotumika Ni shule za vijijini wakati mijini unakuta mwalimu ana vipindi 6 KWA wiki Kati ya vipindi 40. Baadhi ya maeneo Vijijini walimu wana vipindi hadi 60.

Waziri aangalie suala la walimu kupangwa vijijini na baada ya muda mfupi wanahama kinyemela kwenda mijini, kwa barua zinazotoka moja kwa moja TAMISEMI. TAMISEMI imekuwa sehemu ya tatizo.

Serikali iangalie kwa kina na kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza bila kusahau stahiki za walimu zilizoko kisheria.

Mimi bado naona uhitaji wa afisa elimu kuwa wawili kwasababu mtu mmoja kudili kwa mfano na shule 160 za msingi na pengine 40 za sekondari ktk halmashauri moja Ni kazi nzito tofauti na mtazamo wa watu nje ya ufahamu wa jinsi elimu inavyoendeshwa.

(Nimewahi kufundisha sekondari kwa miaka 15 saba kati ya Hiyo nikiwa Mkuu wa shule)
 
Ajirini,acheni siasa nakusubiri Mei mosi,mpate sifa uchwara.Mnakopaje hela nyiiingii,halafu mnazitumia kujenga madarasa tena kwa upigaji Mkubwa bila kuajiri pia?
 
Hapo kwenye mkuu wa mambo ya elimu kwenye halmashauri ndo umechemka yaani PhD holder badala ya kwenda kufundisha awe desk office. Mmh
 
Kuna jambo moja lilinishangaza sana kuhusu fedha za uviko zilizotumika kujenga madrasa. Kuna shule hazikuwa zinahitaji madarasa, walimu hawana ofisi, shule haina jengo la maabara, Kuna shule changa hazina hata vyumba viwili vya kulala walimu.

Kwanini matumizi ya hizi fedha hayakuangalia mahitaji ya msingi ya shule? Siyo kila shule ilikuwa inahitaji madarasa. Mfano Kuna maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro wanaoandikishwa darasa la la kwanza hawazidi 15.

Unakuta shule ina mikondo 8 na Ina vyumba vya madarasa 12,Wana ziada ya vymba 4,halafu bado wanajenga mengine 2 au matatu.

Siasa inaathiri Sana MAENDELEO ya nchi hii.
 
Mitaala elimu iboreshwe, masomo mengi na topic zisizo na tija tuachane nazo, aunde jopo la Wataaluma kufanya Rejea.
Tuwe na masomo machache yenye mashiko na fursa mahitaji yetu.

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
Kweli kabisa,km history,Mambo ya wangoni nk,tuachane navyo sasa
 
Back
Top Bottom