Baada ya walimu walio kuwa wamejificha kwenye Ofisi za Elimu Msingi, Sekondari na TSD ndani ya Halmashauri kutimuliwa sasa Idadi ya walimu Waongezeka

Hapo kwenye mkuu wa mambo ya elimu kwenye halmashauri ndo umechemka yaani PhD holder badala ya kwenda kufundisha awe desk office. Mmh
Masters elimu hawaitambui, Sasa wanataka na PhD awe mkuu wa idara.

Kwenye sekta nyingine hao PhD wamedeliva nn Cha maana?
 
Rais aliposema kwamba watabadili muundo wa Elimu hukumpongeza ila Waziri anapofafanua utaratibu ndio unampongeza 😆😆😆.

Ukipenda boga ..............
 
Unajifichaje Halmashauri ofisini kufanya kazi bila kupangiwa. Hii mada ni usanii.
 
Mkuu tafadhali leta habari kamili ni nini Prof kafanya na kwa namna ipi. Habari yako umeileta kama mwendelezo hivi,si kila mmoja yuko huko kwenye masuala ya walimu?.
 
Kweli kabisa,km history,Mambo ya wangoni nk,tuachane navyo sasa
Taifa lolote ambalo watu wake hawajui historia ya Nchi yao na nchi nyingine basi ni Taifa mfu.
Taifa kama la marekani somo la historia ni lazima kama ilivyo kwa mathematics na Biology kwa hapa kwetu (O-LEVEL).

UZALENDO amabao Mh. Rais anasisitiza bila watu kujua historia ya Nchi yao ni bure.
Kiufupi historia ni maisha ya kila siku it's inevitable to escape.
 
Mkuu tafadhali leta habari kamili ni nini Prof kafanya na kwa namna ipi. Habari yako umeileta kama mwendelezo hivi,si kila mmoja yuko huko kwenye masuala ya walimu?.
Amewafukuza ofisini na kuwa Rudisha darasani, walimu wote ambao walikimbia kufundisha darasani wakiwa wajiriwa wa serikali wakaende kufanya kazi kwenye Ofisi Za maafiselimu msingi, sekondari na TSD bila kuwa na barua Za uteuzi kutoka kwa Katibu mkuu Tamisemi,
 
Duu, nimeamini adui wa walimu ni mwalimu mwenyewe.
 
Na kuna shule toka uhuru hazijawahi kupata darasa jipya au kufanyiwa ukarabati ukionyeshwa hizo shule unaweza sema hii sio tanzania
 
Unashangaa unajifunza eti Zao la Buni Ghana au ulimaji wa mahindi Tennessee ili inisaidie nini. Mtu unaulizwa Umri wa Juma ni mara 3 ya umri wa Sofia je miaka sita iliyopita walikua na umri gani, kwann usimuulize maswali ambayo application yake ndo hizo saundi. Kuna vitu katika elimu ni vya kutoa kabisa. Elimu ya kilimo na ufundi iwe kuanzia darasa la 5
 
Kumbe hiki kinachoonekana kama upungufu wa walimu ni kwa sababu walimu wengi wamelundikana shule za mijini........serikali sasa iweke uwiano sawa wa walimu kwenye shule za mijini na vijijini ili iweze kuajiri pia watu wa kada nyingine..........maana kelele zimekuwa nyingi kwamba kuna uhaba wa walimu na kupelekea serikali kutoa ajira za walimu wakati kimsingi uhaba huo haupo, bali walimu wamelundikana kwenye shule za mijini.
 
Kurudishwa Walimu waliokuwa ofisini kwenda kufundisha mashuleni bado hakutatui Sana changamoto ya upungufu Wa Walimu.Idadi Yao ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya shule na upungufu Wa Walimu uliopo.Dawa ya upungufu Wa Walimu ni kuajiri Walimu wapya.Hata hivyo endapo hizo ofisi za halmashauri zina upungufu Wa maafisa elimu, watateuliwa tu Walimu Wa kujaza hizo nafasi.
 
Hayo yote uliyopongeza wala sio waziri wa elimu ni waziri wa tamisemi

teuzi nyingi za halmashauri zinatoka tamisemi kasoro zile chache ambazo wanateuliwa na wizara husika.

kwa sasa wizara ya elimu inateua wathibiti ubora wa elimu halmashauri wengine wengi teuzi zao zinatoka tamisemi.
 
Ushauri

Hebu jaribu kusoma majukumu ya wizara ya elimu na wizara ya tamisemi,,,kwenye mada zako unachanganya haya majukumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…