Uchaguzi 2020 Baada ya watanzania kumchagua Magufuli kwenye Uchaguzi Mkuu hakika huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa Upinzani

Uchaguzi 2020 Baada ya watanzania kumchagua Magufuli kwenye Uchaguzi Mkuu hakika huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa Upinzani

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
2,789
Reaction score
4,951
Imani tuliyonayo watanzania kwa jemedari wetu wa mapambano dhidi ya ufisadi, rushwa, uhujumu uchumi na uzembe ni wa kiwango kisichotiliwa shaka yoyote hususani kwa tukio lilipo mbele yetu la uchaguzi. Binafsi , mimi ni mmoja wa waumini safi wa kazi na misimamo ya Rais Magufuli kwa rasilimali zetu , sina shaka na maoni haya hata kwa walio wengi.

Tulianza naye safari pamoja na kwa hakika safari ya kuelekea nchi ya ahadi mwaka 2020- 2025 tutakuwa naye pamoja. Ahadi ya elimu bila malipo, kudhibiti upotevu wa mapato, matumizi bora na sahihi ya kodi za watanzania, miundombinu rafiki ya kuchochea uchumi na maendeleo ndio sababu ya imani kubwa tuliyonayo watanzania kwa Rais Magufuli. Si rahisi hata kidogo kufanya anayofanya Rais Magufuli bila kuwa na uthubutu

Ni mengi sana mazuri aliyofanya kwa nchi yetu na yale ambaye hajafanikiwa kuyafanya ni changamoto zinazohitaji muda zaidi na ndio maana tunasema miaka 5 ijayo Tanzania itaonesha maajabu makubwa sana kimataifa na wengi kustaajabishwa na uthubutu wa kiongozi huyu. Ni mitano tena kwa Magufuli

Awamu ya pili ya Rais Magufuli kwa waliojaliwa kuangalia mambo kwa jicho la tatu watakubaliana nami kwamba ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa upinzani kwa sababu kuu mbili: mosi, upinzani utakuwa umeshuhudia nguvu na uwezo halisi wa CCM na kwa kuwa watakuwa wametumia nguvu na uwezo wao wote kuitoa CCM madarakani na wakashindwa basi mwisho wa upinzani ni dhahiri. Pili, katika awamu ya pili ya Rais Magufuli yatafanyika makubwa sana katika taifa hili ambayo watanzania wataachana na fikra zote na mawazo yote ya upinzani kushika dola na kukubali CCM itawale milele.

Nawashauri wapinzani na upinzani kwa ujumla wajiandae kwa mwisho huu wenye maumivu makali lakini hakuna namna wa kurudisha wakati nyuma kuwashawishi watanzania kuikataa CCM.
 
Njaa ni mbaya sana. Hivi upinzani utaishaje kwa Meko ambaye analalamikiwa na kila kundi la kijamii kwa kusababisha hali ngumu ya maisha na kuongezeka kwa umaskini kwa mwananchi mmoja mmoja kutokana na sera zake za kijinga za kiuchumi.
 
Muda ni mwalimu na hakimu mzuri sana wa historia. Tukutane Oktoba
 
Njaa ni mbaya sana. Hivi upinzani utaishaje kwa Meko ambaye analalamikiwa na kila kundi la kijamii kwa kusababisha hali ngumu ya maisha na kuongezeka kwa umaskini kwa mwananchi mmoja mmoja kutokana na sera zake za kijinga za kiuchumi.

Shida CCM wanatumia mbinu chafu na nguvu kubwa ya mamlaka kuua upinzani... Ukweli CCM imechokwa Sana....
 
Mlisema hivo miaka mingi Sana, kwamba sasa upinzani mwisho, matokeo yake upinzani unaenda kukamata dola mwaka huu.
 
Kwahiyo zile nyimbo zenu kwamba upinzani umekufa tusiziimbe Tena? Tusubiri Tena au sio😂😂😂😃😃😃
 
HAYA MAUNABII KILA SIKU MNAYATOA! MLISEMA CHADEMA 2020 HAITAKUWEPO HAYA ONA INAVYOWAHENYESHA SASA IVI.
 
..wewe hujui maana ya siasa.

..You should not be in politics.

..Kuna Maraisi wamefanya mambo makubwa kumzidi Jpm lakini hawahangaiki kuwakomesha wapinzani wao.
 
Nimesoma message ya Joe Trippi ambaye ana research center inaonyesha upinzani umeongezeka Tanzania sasa sijui wewe una ndoto gani! Watanzania hasa vijana tatizo ni ma mbumbumbu sana na Dunia hii ya washindani wanatutisha
 
Njaa ni mbaya sana. Hivi upinzani utaishaje kwa Meko ambaye analalamikiwa na kila kundi la kijamii kwa kusababisha hali ngumu ya maisha na kuongezeka kwa umaskini kwa mwananchi mmoja mmoja kutokana na sera zake za kijinga za kiuchumi.
Wewe uliyeshiba unatafuta nini hapa tz?
Nenda kaishi huko walikoshiba tuache wenye njaa tujenge nchi kwanza
Hatutaki ujinga wa kusifia nchi zingine kama sisi hatuna akili.
 
Nimesoma message ya Joe Trippi ambaye ana research center inaonyesha upinzani umeongezeka Tanzania sasa sijui wewe una ndoto gani! Watanzania hasa vijana tatizo ni ma mbumbumbu sana na Dunia hii ya washindani wanatutisha
Sio mbumbumbu ni mfumo tu,unafikiri Warusi ni mbumbu?Au Korea kaskazini ni mbumbu,au China ni mbumbu.
Weka akiba ya maneno yawezekana hata wewe unakariri kama kasuku.
 
1598543972176.jpeg
 
Hii kauli alianza kuiongea Wassira miaka 10 iliyopita. Akaitumia mpaka kiki ya kuwania urais ila kafa yeye kauacha upinzani ukiwa strong kabisa. Mlisema kuwa 2020 hakutakuwa na upinzani ila sasa mumehamisha goli. Nyie ni WAJINGA
 
Rais wa Tanzania ni Mhe. Dr. Magufuli.
 
Wenzako walikwisha tabiri kifo cha upinzani matokeo yake wao ndio waliotangulia mbele za haki.
 
Back
Top Bottom