Uchaguzi 2020 Baada ya watanzania kumchagua Magufuli kwenye Uchaguzi Mkuu hakika huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa Upinzani

Uchaguzi 2020 Baada ya watanzania kumchagua Magufuli kwenye Uchaguzi Mkuu hakika huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa Upinzani

Tuliambiwa mpaka 2020 upinzani utakuwa umekufa kabisa... na Meko hatahitaji kufanya hata kampeni. Mmesogeza mbele tarehe ya msiba?
 
Imani tuliyonayo watanzania kwa jemedari wetu wa mapambano dhidi ya ufisadi, rushwa, uhujumu uchumi na uzembe ni wa kiwango kisichotiliwa shaka yoyote hususani kwa tukio lilipo mbele yetu la uchaguzi. Binafsi , mimi ni mmoja wa waumini safi wa kazi na misimamo ya Rais Magufuli kwa rasilimali zetu , sina shaka na maoni haya hata kwa walio wengi.

Tulianza naye safari pamoja na kwa hakika safari ya kuelekea nchi ya ahadi mwaka 2020- 2025 tutakuwa naye pamoja. Ahadi ya elimu bila malipo, kudhibiti upotevu wa mapato, matumizi bora na sahihi ya kodi za watanzania, miundombinu rafiki ya kuchochea uchumi na maendeleo ndio sababu ya imani kubwa tuliyonayo watanzania kwa Rais Magufuli. Si rahisi hata kidogo kufanya anayofanya Rais Magufuli bila kuwa na uthubutu

Ni mengi sana mazuri aliyofanya kwa nchi yetu na yale ambaye hajafanikiwa kuyafanya ni changamoto zinazohitaji muda zaidi na ndio maana tunasema miaka 5 ijayo Tanzania itaonesha maajabu makubwa sana kimataifa na wengi kustaajabishwa na uthubutu wa kiongozi huyu. Ni mitano tena kwa Magufuli

Awamu ya pili ya Rais Magufuli kwa waliojaliwa kuangalia mambo kwa jicho la tatu watakubaliana nami kwamba ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa upinzani kwa sababu kuu mbili: mosi, upinzani utakuwa umeshuhudia nguvu na uwezo halisi wa CCM na kwa kuwa watakuwa wametumia nguvu na uwezo wao wote kuitoa CCM madarakani na wakashindwa basi mwisho wa upinzani ni dhahiri. Pili, katika awamu ya pili ya Rais Magufuli yatafanyika makubwa sana katika taifa hili ambayo watanzania wataachana na fikra zote na mawazo yote ya upinzani kushika dola na kukubali CCM itawale milele.

Nawashauri wapinzani na upinzani kwa ujumla wajiandae kwa mwisho huu wenye maumivu makali lakini hakuna namna wa kurudisha wakati nyuma kuwashawishi watanzania kuikataa CCM.


Hayo mbona mapya? mlisema upinzani utakufa kabla ya 2020 leo tena mmebadilika ninyi hamnazo
 
Nasikitika kusema kwamba mwisho Wa upinzani umeonekana dhahiri, hii inatukumbusha wakati ambao watu hufuata hisia zao za ndani ni wakati Wa kuamua
 
Back
Top Bottom