Japo hawakuzaliwa pamoja wala hawakuchangia
damu, lakini machoni mwa watu walionekana ni
kama mapacha kutokana na ukaribu wao wa
kuambatana kama kumbi kumbi huku kila mmoja
akimuita mzazi wa mwenzake baba au mama. Hakuna aliyetaka wala kusikia mwenzake
akisemwa vibaya na watu wengine huku ukaribu
huo ukipendwa na wengi japo wengine
waliumizwa na ukaribu huo na kuwatupia matusi
na maneno ya kejeli kwenye mitandao ya kijamii,
lakini ilikuwa ni kama ‘sisimizi kumbeba tembo’ jambo ambalo lisingewezekana kirahisi. Nimeamua kuanzia mbali ili niweze kukumbusha
miaka miwili au mitatu iliyopita uvute taswira ya
picha kwa kile unachokiona wakati Dully Sykes
alipoachia wimbo wa ‘Utamu’ na kuamua
kuwashirikisha wadogo zake Ommy Dimpoz na
Diamond Platnumz kipindi ambacho ungeambiwa utaje wasanii watatu wanaofanya vizuri kwenye
muziki usingeacha kuyataja majina ya wasanii hao
wote wawili. Nakumbuka miaka miwili iliyopita mwezi Juni,
Dimpoz aliiambia Bongo5 kuwa kuna kolabo kati
yake na Chibu inakuja na aliweza kusifia sana kwa
kupamba huku akisema, “Watu kwanza najua
wanasubiria kwa hamu sana lakini trust me
nakuambia siku utakayosikia moto umewaka basi itakuwa ni balaa na unaelewa kwamba
wamanyema kwanza hawakosei. Sijui itakuwaje,
lakini ni balaa. Halafu projects zipo nyingi tu lakini
watu wasubirie tu waone itakuwaje lakini
nakuambia ukweli itakuwa hatari sana.” Siku zimepita na miaka imekwenda hakuna kolabo
tuliyoiona lakini “ukistaajabu ya Mussa utayaona ya
Firauni,” ndio tuliyoyaona. Ndipo nikaukumbuka
wimbo malkia wa muziki wa Bongo Fleva, Lady
Jaydee ‘Siku Hazigandi’ baada ya kuona urafiki
uliogeuka undugu wa damu ukiteketea na kugeuka majivu baada ya kuunguzwa na mwanga
wa tochi – ni kitu cha kushangaza na
kisichowezekana lakini kwa hapo kiliwezekana. Nilifurahi sana kuna busara iliyotumika kwa kila
mmoja kukaa kimya bila ya kumshtumu mwenzake
kwa lolote na kila mmoja akifanya kazi kivyake
lakini ghafla nuru ya mwanga uliopo kugeuka giza
baada ya usiku wa Jumanne hii mtandao wa
Instagram ukigeuka uwanja wa ‘Kitchen Party’ kwa Ommy na Diamond kutupiana vijembe vya maneno
ya kashfa na kuanza kutoleana siri ambazo kwa
mashabiki hatuna uhakika nazo labda wao
wenyewe wanajua juu ya ukweli wausemao kwa
jamii. Diamond alianza kwa kuandika kwenye kipande
cha video ya wimbo mpya wa Rich Mavoko
aliyoiweka kwenye mtandao huo, “Kushindana na
Wasio Jua Raha sana hahahahahaha …….” Ommy Dimpoz alijibu kwa kuandika: Wazee Wa Kupanik Mbona Kama Povuuu
Linawatoka [HASHTAG]#TeamMzikiMzuri[/HASHTAG] VS #
TeamUjanjaUjanja
[HASHTAG]#Kajiandae[/HASHTAG]
[HASHTAG]#KabaliYao[/HASHTAG]
[HASHTAG]#WeDontBuyViews[/HASHTAG] [HASHTAG]#MeNilijuaTunafanyaMzikiKumbeVitaaa[/HASHTAG]
[HASHTAG]#NawajuaWazeeWaKuchambaNataniaTu[/HASHTAG]
[HASHTAG]#PiaNawajuaKwaMitusiLakiniNishajiandaa[/HASHTAG]
[HASHTAG]#NawaachiaUwanjaMweupeeeWalaSiblokuMtu[/HASHTAG]
[HASHTAG]#NachangamshaBarazaKidogoooo[/HASHTAG] Diamond alishindwa kuvumilia naye aliandika,
“Mtoto wa Kiume kumchukia Mwanaume Mwenzio
kisa Kakataa kukupumulia nayo ni [HASHTAG]#KOKORO[/HASHTAG].” Kwa watu wanaofahamu zaidi maneno ya mitaani
wanaweza kufahamu kilichoandikwa ndani kina
maana gani tena hayapaswi kuandikwa na wasanii
wakubwa kama hawa kwenye hadhira hii. Wakati
huo huo siku hizi mitandao ya kijamii
inatembelewa mpaka na watoto wadogo, je watoto wao au hata ndugu zao wadogo wanaowalea na
kuwategemea wakiona mtu anayemuheshimu
nyumbani amefanya hivyo mitandaoni unafikiri
itakuwaje? Kumbukeni mlipotoka kwa kuwa ‘Adui yako wa
leo ndio rafiki yako wa kesho, na rafiki yako wa leo
ndio adui yako wa kesho’.
SOURCE: BONGO5