Mda utasema, ila kwa hali ilivyo na namna ambavyo hata Mbowe amekuwa si kitu kwa wanaChadema, itabidi wafikirie mara 2Mbowe,Sugu,Boni hawa ipo siku tu,,
Wajinga wameenda kuharibu chama kubwa CHAUMMA, lilikuwa ni chama lenye nia ya dhati kuwashibisha ubwabwa watanzania na kupeleka maji ya Bahari kule Dodoma na kuleta midege ya umwagiliaji ingesambaa nchi nzima. Wametuharibia chama hawa wapuuziCHAUMMA ulikuwa ni mradi mbaya kuwahi kutokea. Nadhani hata waliokwenda huko sasa hivi wanajilaumu na kusema ni bora wangeenda CCM. Hata Wenje angeenda CHAUMMA kama wangefanikiwa lakini alichezwa machale akaamua kusubiri na kupima upepo kwanza. Mwanamama kama yule Catherine uge alikuwa ni mwanasiasa mzuri sana lakini sasa hivi hasikiki hata kidogo. Nadhani ni suala la muda tu na yeye atakimbilia CCM.
Dunia haina watu wapumbabu kama unavyoweza kufikiri. Wanajua kuwa kuna petty political parties affiated to CCMChauma siyo mradi mbaya kwa CCM kama unaiangalia kwa mtazamo wa CCM. CCM wanacheza na hesabu za arithmetics (hesabu simple za kujumlisha na kutoa tu). Ukitoa Chadema unaweka Chauma; tayari unakua na ushahidi mbele ya wamataifa kwamba idadi ya vyama vya upinzani nchini bado ni kubwa na ni nzuri sana tu. Kinacho matter hapo ni idadi tu ya vinavyoitwa vyama vya upinzani. Siyo ubora wa chama. Halafu unaanzaje kusema Catherine Ruge ni mwanasiasa bora? Huyu hajawahi kushiriki fair competition mahali popote kisiasa akashinda.