Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali

Anawatumia kukufikia wewe be wise. Kuna mtu namjua alikuwa anawatumia watoto kumpgia mwenza ili aweze kurudi
Bas atakua hajafanya calculation zake sawa sawa. Japo hii kitu kwasasa siipendi. Sitaman hata kuzungumza na wanangu kwasasa maana naona ni kama anataka kuwatumia ili kujitonesha maumivu, anajua jinsi bond ya mimi na wanangu ilivyo.
So nimehis may be alivyoona nimemkataa vibaya mahakaman akahis nimeshakata shauri la ku move on hivyo anataka kuanza kuni tesa kihisia na kunipa mawazo.
Maana anajua siwez kuwawaza wanangu nikaacha kumuwaza na yeye.
Hili naliona kama mtego na kiukwel sijalipenda, nalitafutia ufumbuzi
 
Kwani huko anakokwenda kuchakata yeye hakujachakatwa na wanaume wenzie?
Sio kuchafu?
Ni kheri shetani unayemjua kuliko Malaika usiyemjua.

Kama kuna uwezekano wa kurudiana na nafsi zao zimeridhiana warudiane tu.
Personally ,sitaweza.
Niseme sikuwahi kuwaza hiki nachikifanya kwasasa kama kingenisaidia kumuondoa mawazoni haraka, ila kuna jamaa akanilazimisha ku join Gym, ku lift heavy weights, aisee imasidia sana ku concerntrate kwenye kile unachokifanya kwa muda huo, ukitoka hapo hoii jion unafikia kula na kulala.
Maisha mazuriii.
Sasa naendelea vizuri ndio huyu mtu anaanza kusumbua tena πŸ˜‚
 
Madam alishakuwa mke Kisha akaenda akafanya uasi na kwenda kuchakatwa huko hastahili msamaha hata ukimsamehe atakuona dhaifu sana na unamsamehe ili iweje?
Labda umsamehe ili akuue mazima. Maana mission was aborted, never completed
 
Kama umeweza kumove on mapema hivyo hongera kwako…Wengine inachukua miaka na miaka.
 
Aliteleza, aidha kwa kukusudia ama kwa bahati mbaya, matokeo yake yamemfanya agundue udhaifu wake na kuamua kujirudi.

Hata Ex mume anaonesha dhahiri kuwa bado anampenda.
Kusema ule ukwel, nikisema simpendi nitakua najidanganya πŸ˜‚. Huo utakua uongo, ila tu kwasasa nimeamua acha iwe hiv. Kumpenda mtu sana ni pamoja na kuwa tayari kumuacha aende aka explore other life choices.
Acha aende tu
 
Ni yeye! Narudia, ni yeye. Mimi hizi situation nazijua sana. Mwanamke akishajua unawapenda sana watoto wako, kwenye hali kama hiyo ni lazima atawatumia kutaka kurudisha uhusiano wenu. naonekana huyo mama hana plan yoyote bali ni wale wanawake mapepe wanaofuata mkumbo. Alipata bwana wa pembeni akamdanga'nya ndiyo akaleta dharau. Subiri tu utakuja kuleta mrejesho hapa ameanza kujipendekeza kwako.
 
Am still observing what is going on.
 
You never know Mheshimiwa. Hasira zikiisha huwa sometimes tunajiona wajinga kwa mambo tuliyo yafanya wakati tumekasirika. Give her the space she wants for now. Lakini nakwambia huyo atarudi tu; huko duniani atakutana na mengi na soon atakukumbuka.
Ni kweli ulivyosema. Unajua mwanamke anapokuwa ameolewa, akipita njiani na kusemeshwa na wanaume wengine (pengine wenye maisha mazuri kuliko mumewe), hudhani kuwa anapendeka sana na akiondoka hatapata shida. Shida inaanza anapoomba talaka na kukuta kumbe mambo siyo marahisi kama alivyodhani. Waswahili husema ukiumwa na nyoka..... mwanamke wa aina hiyo siyo wa kurudiane naye kirahisi rahisi hata kama unataka kumsamehe. Inatakiwa umwache maisha yamnyooshe mpaka aimbe po akikuona apige magoti na kulamba miguu yako.
 
Shukran. Taratibu nitakaa sawa tu. Konde boy anasema " hata kama mapenzi yamekwisha, yanabaki mazoea".πŸ˜‚.
Na mazoea ndio yanaletaga tabu
Sasa mtu uliyemzoea for 15 years, sio kirahis hivyo kumsahau
Ni kweli kabisa.
 
Hebu kuwa mwanaume Mkuu, yani uache kuwasiliana na watoto wako sababu ya mpuuzi mmoja?

Huyo mkeo kwa sasa ni zamu yake kuumia na ninakwambia sasa hivi zamu yake kukesha kwa mawazo. Waswahili walisema penzi hugeuka leo kwangu kesho kwako! Sasa hivi ndio ataona reality ya alichokitafuta
 
Shukran. Taratibu nitakaa sawa tu. Konde boy anasema " hata kama mapenzi yamekwisha, yanabaki mazoea".πŸ˜‚.
Na mazoea ndio yanaletaga tabu
Sasa mtu uliyemzoea for 15 years, sio kirahis hivyo kumsahau
Ni kweli kabisa. Na ndio mana Mwenyezi Mungu kwenye Quran amesema kama wana ndoa wanataka kurudiana msiwakataze waacheni warudiane. Ndio mana katika Uislamu kuna Talaka rejea. Hapo kila mtu kuna lake amejifunza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…