Baada ya Yanga kujitenga, Familia ya Yusuph Manji yahitimisha msiba bila ya Yanga!

Ingekuwa hawapendi mambo mengi wala hii dua wasingefanya mwaya, ila wameifanya na list imejaa wawakilishi kibao ila Yanga tu ndio hawapo!
 
Uongozi umetutia aibu.
Sawa ushindani wa kibiashara juu ya Yanga ulikuwepo.
Ila ndo ivo Manji kashafariki hafufuki hakuna haja ya visasi.
Wangeupa msiba uzito
Ile siku uliyoanzisha thread nilichangia na nikapinga vikali, kumbe yalikuwa makubwa kuliko tulivyodhani!

Hersi nimemvua vyeo, yeye ndiye anayebeba lawama ya uongozi.
 
Nashukuru Mkuu, umesema yote.
 
Naheshimu mawazo yako mkuu
Ila ukichunguza unaona kulikuwepo nia mbaya kumfifisha Mwenyekiti wa zamani Manji
Hata ukiangalia kwenye mitandao page ya Yanga wapo tu kama Bora liende
Mambo mengine yanayaendelea tokea walipopost ile taarifa juu ya msiba wake waliishia hapo. Wakati mambo mengine wanapost mara 10,10!
 
Ile siku uliyoanzisha thread nilichangia na nikapinga vikali, kumbe yalikuwa makubwa kuliko tulivyodhani!

Hersi nimemvua vyeo, yeye ndiye anayebeba lawama ya uongozi.
Hakika mkuu Eng Hersi Said katuangusha.
Manji ilitakiwa awe sehemu kubwa ya historia ya club yetu
 
Manji kazikwa Marekani, Yanga wanaweza kutoa tu pole kwa familia na mashabiki. Pia bado haijaisha, yanga wanapenda sana matukio ya supu supu wanaweza itisha siku ya supu kwa ajili ya manji. RIP
 
Watu walipiga kelele GSM kumuweka kibaraka wake Hersi pale Yanga leo hii naona walikuwa sahihi.

Kibaraka anaogopa kumuenzi boss wa zamani asimkwaze mpya. Lakini angekuwepo Msola tusingeonga huu ujinga.
Sasa dear nani hataki kumuweka kibaraka ktk taasisi yake? Hata ungekua wewee, ishakua ni lazimaa.

Sema Yanga wamezingua sanaa. Daaah.
 
Watu walipiga kelele GSM kumuweka kibaraka wake Hersi pale Yanga leo hii naona walikuwa sahihi.

Kibaraka anaogopa kumuenzi boss wa zamani asimkwaze mpya. Lakini angekuwepo Msola tusingeonga huu ujinga.
Nilipendekeza siku ya mwananchi iwe rasmi Kwa ajili ya kumuenzi Manji japo itakuwa ni Kwa kuchelewa.

Au huo uwanja utaojengwa uitwe
Manji Yanga complex
 
Nipo hapa tushakula ubwabwa..tunaondoka. hivi marehemu si alikuwa anakesi mahakamani na bakwata wakigombea Ardhi iliishia wapi ..? Nakumbuka ule ugomvi hadi marehemu R.Mengi aliingia kati .. Ardhi inabeba watu .. ardhi uliyogombea ndio inayokumeza
 
Attachments

  • 17203498551898433852675873321155.jpg
    3.1 MB · Views: 4
Manji kazikwa Marekani, Yanga wanaweza kutoa tu pole kwa familia na mashabiki. Pia bado haijaisha, yanga wanapenda sana matukio ya supu supu wanaweza itisha siku ya supu kwa ajili ya manji. RIP
Hatuwezi kutegemea lolote la maana kutoka kwako katika hili.
 
Nilipendekeza siku ya mwananchi iwe rasmi Kwa ajili ya kumuenzi Manji japo itakuwa ni Kwa kuchelewa.

Au huo uwanja utaojengwa uitwe
Manji Yanga complex
Kama kumuenzi tu kwa kuupa heshima stahiki msiba wake pale Klabuni wameshindwa ndio yaje kuwa hayo makubwa? Labda waone aibu baada ya watu kupiga kelele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…