Baada ya Yanga kujitenga, Familia ya Yusuph Manji yahitimisha msiba bila ya Yanga!

Baada ya Yanga kujitenga, Familia ya Yusuph Manji yahitimisha msiba bila ya Yanga!

Mkuu, hii thread sijawaongelea wahindi na waarabu wa mtaani kwenu, hapa namuongelea Yusuph Manji aliyekuwa kiongozi na mfadhili wa Yanga kwa takribani miaka 10, get your facts right.
MAISHA NI HADITHI, UKISHA FARIKI HADITHI YAKO HUISHIA HAPO.
 
Mpaka familia wanafikia hatua ya kutokuihusisha Yanga kwenye dua ya mpendwa wao sio jambo dogo, wamezingua.
Kwanini usiwaulize familia ya Yusuf Manji kwanini hawajaiweka Yanga kwenye ratiba ya matukio ya shughuli yao?
 
View attachment 3035616
Ndugu wanajukwaa, leo familia ya Manji wamehitimisha msiba wa mpendwa wetu Yusuph Manji uliotokea Jumamosi ya wiki iliyopita kwa Dua maalumu iliyosomwa na viongozi mbalimbali wa kidini wakiongozwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika viwanja vya Karimjee.

Katika jambo lililowashangaza wengi ni ratiba rasmi ya dua hiyo iliyotolewa na familia hiyo ya Manji kutokuonekana kwa Klabu ya Yanga ambayo marehemu aliifadhili kwa miaka mingi!

Ratiba imeweka wazi kwamba atakuwepo mwakilishi kutokea tasnia ya mpira na sio kama ambavyo ilipaswa kuwepo Yanga, mwakilishi kwenye soka anaweza kuwepo yeyote hata kutokea kwa watani zetu, Simba.

View attachment 3035619View attachment 3035620

Yanga, tumefikaje hapa?
Hadi familia kufikia hatua hii lawama zote wanabeba uongozi wa Yanga chini ya Eng. Hersi. Tokea kutangazwa kwa kifo cha Manji macho yetu tulio wengi yaliigeukia Yanga, kinyume na matarajio ya tulio wengi Yanga walitoa pole kwa familia pekee kisha wakaendelea na mambo mengine bila kuupa uzito msiba huu wa kiongozi muhimu zaidi kutokea kwenye historia ya mpira nchi hii.

Hersi na wenzio, mnajua kwamba hadi leo hii hakuna mwekezaji yeyote aliyefadhili klabu yoyote kwa pesa zake mwenyewe bila nia ya kujineemesha kibiashara zaidi ya Manji?

Mnajua kwamba hadi sasa ufadhili wenu GSM hapo Yanga haujafikia hata nusu tu ya aliyoyafanya Manji kwa Yanga bila shinikizo wala mabandiko ya bidhaa zake kwa kutumia nembo ya Yanga?

Kwanini mmemtenga Manji kiasi hiki? Mnafikiri yote haya aliyoyafanya mtatusahaulisha kwa kuupuza msiba wake? Manji aliwakosea nini hadi kuvunjiwa heshima aliyoijenga kwa dhati hapo Yanga? Kweli Manji anafariki hadi kuzikwa na hadi leo hii dua hamjihusishi kwa lolote?

Mashabiki wenzangu tumemwamngusha Manji!
Tukiachana na GSM ambao wana maslahi yao binafsi tofauti na sisi wapenzi na mashabiki wa Yanga, pia tunabeba lawama.

Kwanini tulishindwa kuushinikiza uongozi kumuenzi Manji baada ya kuona wameupuuza msiba wa Mwananchi mwenzetu? Leo hii tumesahau alikotutoa Manji? Popote linapotajwa jina la Manji Yanga haikosi kuwepo, kwanini tumeshindwa kumpa heshima? Tumekosa fadhila kiasi hiki kwa mtu aliyetutoa kwenye mabakuli na kutupa heshima tulipokuwa dhalili?

Nimeumizwa sana, lakini nimekatishwa tamaa na uongozi niliouona makini na kuusifu mara nyingi waziwazi chini ya Hersi. Huu ni udhalimu na hakika Manji hatotusamehe!

Nikitokea hapa Karimjee, ndimi mnazi wa Yanga niliyeumizwa…

Nifah
B... umeandika vizuri sana na umetoa hoja makini mno. Ila kwa kuwa media zote 'zimetekwa' na hao unaowakosoa hoja hii haiwezi kupewa nguvu.

Utaratibu wa kutoa heshima kwa waliofanya makubwa kwenye vilabu vya soka ni wa kudumu na uko duniani kote. Ni makosa kwa Yanga kutotoa heshima kwa Manji.

Kwa wakati huu ambao Hersi alisema anaanza mchakato wa kuandika historia ya Yanga, anadhani itatimia vipi historia ya Yanga bila kumtaja Manji?

Labda zile hasira za Manji kufika ghafla kwenye mkutano mkuu wa Yanga na akashangiliwa na members kuliko wao ndiyo zimeendelea hadi akiwa marehemu.

Ova
 
Asante b…

Kuna waliokuja na hoja dhaifu ya kusomewa dua! Kweli kwa aliyofanya Manji pale Yanga ni wa kusomewa dua pekee? Tena dua ya uchochoroni ambayo hawakuishirikisha familia ya marehemu.

Mimi hadi leo nitamchagua Manji over GSM, period.
 
Hata CCM waliachwa, wakati alikuwa diwani wetu Mbagala.
Kabisa unaitaja CCM bila aibu? Waliyomfanyia hukuyaona?

Mimi familia ya Manji wamenikosha sana, sio wanafiki. Kama uliwahi kuzinguana na mpendwa wao hawana habari na wewe, safi sana.

Ni kama ambavyo familia ya Lowassa hawakumtaja Mr. Smile kwenye salamu zao za shukrani.
 
Asante b…

Kuna waliokuja na hoja dhaifu ya kusomewa dua! Kweli kwa aliyofanya Manji pale Yanga ni wa kusomewa dua pekee? Tena dua ya uchochoroni ambayo hawakuishirikisha familia ya marehemu.

Mimi hadi leo nitamchagua Manji over GSM, period.
Dua ya kutoshirikisha familia ya marehemu ni janja janja tu.

Ova
 
Kabisa unaitaja CCM bila aibu? Waliyomfanyia hukuyaona?

Mimi familia ya Manji wamenikosha sana, sio wanafiki. Kama uliwahi kuzinguana na mpendwa wao hawana habari na wewe, safi sana.

Ni kama ambavyo familia ya Lowassa hawakumtaja Mr. Smile kwenye salamu zao za shukrani.
Niliongeza tu kwa sababu nao hawakutajwa kama Yanga.
 
Back
Top Bottom