Baada ya Yanga kupoteza Kesi CAS, Mwanasheria Simon Patrick ajiuzulu rasmi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Baada ya klabu ya Yanga Sc kuangukia pua kwenye kesi yake dhidi ya Shirikisho la soka Tanzania TFF, Bodi ya Ligi na klabu ya Simba Sc, Mkuu wa Kitengo cha Sheria klabuni hapo, Simon Patrick ametangaza kuachia ngazi kama Mwanasheria wa Mabingwa hao wa kombe la Muungano 2025.


Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Adv Simon Patrick ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Mawakili Tanzania (Tanganyika Law Society) pamoja na Chama cha Mawakili cha Afrika ya Mashariki (East African Law Society) amebainisha kuwa sasa anasalia kuwa mwanachama mtiifu wa Yanga kuomba aruhusiwe aendelee kupumzika kwenye soka la Bongo.

"Vita dhidi ya wahuni haijawahi kuwa rahisi. Wanayanga wenzangu, najua maamuzi madogo ya CAS yamewaumiza, ila tuwapongeze viongozi wetu kwa kupinga uhuni kwa vitendo na nina uhakika hawajakata tamaa." Simon Patrick amesema

"Najua hawawezi kujitokeza kuwaeleza wanayoyapitia nyuma ya pazia, ila ipo siku mtawaelewa. Niwaombe wana Yanga muendelea kuwapa moyo na kuwaunga mkono kwa nguvu. Kwa muda niliotumikia klabu, nimejionea jinsi ilivyo changamoto kuiongoza klabu ya Yanga."

"Mwisho, nitumie fursa hii kuwaomba radhi ndugu zangu waandishi wa habari. Nimekuwa sipokei simu zenu, si kwamba sipendi kuzungumza nanyi, bali kwa sasa mimi ni mwanachama mtiifu wa Yanga, Nawaombeni mniruhusu niendelee kupumzika soka la Bongo, Yanga ina watu makini wengi na wenye weredi tuwape muda waendelee kutupambania" amesema Simon Patrick
 
Hahahahahah ni kazeze...yani umewaingiza chaka weee hao utopolo..
Kesi zote za wanamichezo umefeli kesi za kina kagoma umefeli..kesi zimekukataaa...wakili kaa kwa amani
Sio kuwaingizia tu chaka dada..kapiga pesa zao nyingi tu kwenye hizo kesi...ni tapeli na muhini tu kama matapeli na wahuni wengine.
 
Simba ndiyo aliyekimbia mechi lakini sasa makolo wanajitahidi ionekane Yanga ndiyo amekimbia mechi
Kama mlikua mnaitaka sana mechi wahuni nyie msingewazuia wenzenu kufanya mazoezi,hivyo ni kweli kabisa nyie ndio mmeikimbia mechi na ndio maana mnasisitiza derby hamchezi na ndio maana pia CAS wamewakataa
 
Amefeli tenaa? Kwani huyu Simon Sheria alisomea chuo gani? Vipi na LS alifaulu vipi?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kule CAS hakuna longolongo,ni hoja kwa hoja,gazeti lao la maelezo meengi halijaeleweka kabisa,🀣🀣🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…