Baada ya zuio la miaka 21, Tanzania yaruhusiwa rasmi kupeleka bidhaa ya nyama nchini Saudi Arabia!

Kweli mama anajitahidi kutafuta masoko, mikopo, fursa mbalimbali, tatizo mianya kibao, kujichotea mtindo wa mabilioni, watumishi kujilundikia mipesa bila kazi ya ziada!
Hizo stories zako za kusadikika za kujichotea mabilioni una ushahidi?
 
kwa iyo na maisha yako ya kawaida huendi hospitali? hutembelei barabara za lami? huna mtoto anayesoma bure la kwanza hadi form 6? Unadhani hela ya yote hayo inatokana na nini?

Kweli utakuwa ni msukule na sio binadamu!
Kuna nchi zinaendesha uchumi wake kwa kuexport ndizi tu huko america ya kusini,na waanchi wanaishi vizuri tu,sisi tuna madini,gas,utalii,bandari karibia 4 n.k,na bado mwananchi amebanwa na tozo kila sehemu,halafu unajisifia eti kuna elimu bure!on ground life ni ngumu hatari wewe lamba tu asali uendelee kusifia
 
Mama yupo kwa Wajomba hawawezi kumwangusha! Anaupiga mwingi
 
Chuki zako zimeshakupa ukichaa!
Nenda page ya East African TV Facebook kuna habari kamili. Jana wamefanya mahojiano na balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia
Jibu swali kwa mtiririko sasa nimchukie Samia ananilisha ananitibu au ndio kuropoka wengine hatuna vyama
 
Maisha magumu kivipi? Tafuta kazi jitafutie kipato ! hata marekani na China kwenye chumi kubwa kuna watu wana maisha magumu!

Mie nimejiajiri nafanya kilimo na maisha yanaenda Mungu ananisaidia! nalamba asali kwa kujishughulisha
 
Sababu ya kuzuia ilikuwa kuenea kwa ugonjwa wa miguu na midomo...
Taarifa iliyosomwa Jana nadhani,inasema imeruhusiwa baada ya jitihada za muda mrefu za wataalamu kwa hiyo miaka 21.

Lakini hata ukiamua kutumia akili za kawaida, haiwezekani zuio la miaka 21, kwa sababu za kitaalamu za ugonjwa Kama unavyosema, ziondolewe kwa maongezi ya siku 1 tu za wanasiasa, labda Kama sababu za ugonjwa unazosema zisiwe za kweli, lazima ziwe harakati za muda mrefu za wataalamu kujiridhisha kuwa ugonjwa uliokuwa unahofiwa haupo Tena.

Ila gonja aupige mwingi maana ndiyo mafanikio ya wananchi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Watakua wanapelekewa na mwekezaji wa Ngorongoro ,kwan KWa zuiyo Ilo la miaka 21 kwani tumepata shida GANI?

Mnasifia mpaka ujinga, alafu fuatilia ksmpuni izo mbili then urejee hapa, izo ni za kifisadi tu
 
Jibu swali kwa mtiririko sasa nimchukie Samia ananilisha ananitibu au ndio kuropoka wengine hatuna vyama
Mtitiriko gani? Nimejibu sehemu ninazoona naweza kukusaidia! Mengine nimeona ni upuuzi wako tu unaotokana na kujaa sonona dhidi ya mama wa watu
 
Watakua wanapelekewa na mwekezaji wa Ngorongoro ,kwan KWa zuiyo Ilo la miaka 21 kwani tumepata shida GANI? Mnasifia mpaka ujinga, alafu fuatilia ksmpuni izo mbili then urejee hapa, izo ni za kifisadi tu
Endelea kuishi kwa nadharia na mambo ya kusadikika

Samia anazidi kufungua uchumi tu
 
Ukweli atukuwa na HALAL Council Tanzania kwa miaka mingi hii ndo ilikuwa sababu kubwa(imeanzishwa 2 ago) Mchakato umeanza muda tu! Tuache kumpa sifa mtu asizostahili .Akuna kuupiga mwingi wala nini Ukweli lazima usemwe tuache cheap politics
 

Attachments

  • 71955084-8822-4201-89E0-305C4AAC8030.jpeg
    28.7 KB · Views: 7
Hata Bwawq la Nyerere mchakato ulianza siku nyingi ila sifa imepewa awamu ya 5 kwa kuufanya na kuufanikisha

Samia kafanya mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya nje wa Saudi na akawasilisha hili, Mwezi Machi mwaka huu aliwatuma Mawaziri Mulamula na Waziri wa mifugo kwenda Saudi kushughulikia hili na juzi alipotoka Oman alipitia Saudi akakumbushia hili. Jana Serikali ya Saudi ikatoa zuio lake kwa Tanzania

Kubali tu! Samia ni habari nyingine!
 
Naona bidhaa nyingi hasa za Bakhressa zina haka ka nembo au nadanganya ndugu
 
Nampongeza Rais kwa kutufungulia hii fursa
 
Ngorongoro inahusika hapa.
 
Shida ilikuja kwa kutokuwa na Tume ya Kucertfy Muslim HALAL foods Council- ata kama Rais angeomba tupewe export permit ya Nyama Msaudi asingeweza toa kwa sababu ya ishu ya Kulishana Vibudu!! Ikimbukwe mpa USA machinjio yote wachinjaji ni Muslims! Na kote huko zipo Halal Council's
 
Naona bidhaa nyingi hasa za Bakhressa zina haka ka nembo au nadanganya ndugu
Kweli kabisa- Na Kote Duniani Waislam wanasisitizwa kutumia bidhaa zenye hii Halal Logo! Wahindi (Hindus)pia wanayo yenye kuonyesha bidhaa zisizotumia mazao yatokanayo na nyama ya Ngombe. Na sio eti anaupiga Mwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…