Baada ya zuio la miaka 21, Tanzania yaruhusiwa rasmi kupeleka bidhaa ya nyama nchini Saudi Arabia!

Hizo kampuni utakuta moja ina hisa za msoga by 80% nyengine hisa za Mzee Hassan kwa 80% halafu wabongo mnaimbiwa ngonjera za nchi kufunguka na mnapiga makofi.

Tuwaone mbuzi wa Vingunguti wakipelekwa Oman hapo huenda ika make sense.
Hata we unaweza kupeleka nyama huko mkuu

Ova
 
Swali: Kwani soko la nyama ya Tanzania ni Saudi tu? Au ni baadhi ya hayo masoko? Au quality standard ya nyama? Najua middle eastern na maghreb wanahitaji Halal, lakini soko la nyama si haba duniani
 
Swali: Kwani soko la nyama ya Tanzania ni Saudi tu? Au ni baadhi ya hayo masoko? Au quality standard ya nyama? Najua middle eastern na maghreb wanahitaji Halal, lakini soko la nyama si haba duniani
Ukiona hivyo kuna mambo washayaweka sawa
Huko Saudi tu kupeleka vyakula
Si kazi ndogo,wanangalia sana ubora na vigezo nk
Taratibu soon tutarudi pia kwenye soko la ulaya

Ova
 
Ukiona mtu analeta habari za kipambe namna hii ni chawa mwenye midomo miwili.
Unaowapa pole wameshiba na wana dola zao sio za kichawa.
Rais Samia kufanya juhudi ni sehemu ya majukumu yake na sio lazima asifiwe kwani analipwa pesa ndefu na masurufu ya kufa mtu.
 
Kwani akisifiwa we inakuuma nini?
 
Sisemi vibaya utajiri Tanzania hua unapatikana Rais akiwa Muislam wakiingia wapagani na wagalatia watu wanalimia meno
 
Asante Rais kwa Jitihada za kufungua nchi. Kila linalozalishwa Tanzania kingepata soko halisi popote duniani, tungeongeza idadi ya wa-Tanzania wenye uwezo mkubwa wa kununua (relatively high purchasing power) tukaongeza uwezo wa kukusanya kodi, japo kiwango kidogo tu tungeweza kukusanya Tzs. Trilioni 10 kwa mwezi. Kwa mwaka Trilioni 120 tu, automatically hatuhitaji kuomba kokote, bali tungekopesha mataifa mengine baada ya kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati. Ni hilo tu
 
Mjomba ni mama! Kama ukienda ujombani utakubaliwa tu 😁
 
Mimi namuamini SSH na JPM kwani wote wanatekeleza ilani ile ile.

Kuamini kwamba Magufuli mwingine atarudi ni sawa na kuamini kuwa jua kuna siku linatoka asubuhi magharibi halafu jioni lizame mashariki.

Pia kumbuka kuwa kuna watanzania waliumizwa sana na awamu ya tano, walipoteza kazi, baadhi wakabomolewa nyumba zao na baadhi yao wakakosa kabisa matumaini wakaamua kujiua.

Hivyo SSH licha ya kuzungukwa na wahuni ni mama mwenye huruma hivyo hana hulka ya kuona mtu anateseka yeye akaendelea kushikilia msimamo huku akiumiza mamilioni ya wanaomtegemea huyo anayeteseka.

Mama kama mzazi hana kiburi kisichokuwa na sababu zenye kuingia akilini, hana zile hulka za kuonea tu bila ya sababu. SSH na udhaifu wake wote anakwenda kuipaisha nchini kiuchumi.

Ni msikivu mwenye kupenda kujifunza kutoka kwa wengine, pia ni mtetezi wa vitendo wa wafanyabiashara.

Kudhani kuwa Magufuli ndio kigezo au alama au ndio rais mwenye kutakiwa kufikiwa na wanaomfuatia kushika ofisi ile ni kujidanganya tu.
 
Hizi ruhusa zina gharama zake ..sio bure bure tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…