PreGE2025 Baadhi ya G-55 wakiwemo Benson Kigaila, John Mrema, Catherine Ruge na Salum Mwalimu wajiondoa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
mkuu john kaanzia mbali, kubeba spika na kubandika mbao za matangazo, leo unamfukuzaje ka mbwa kisa alikuwa right man wa mbowe
Sema ukweli, hajafukuzwa kwa sababu ali msupport Mbowe. Alifukuzwa kwa sababu ka misbehave.
 
ameshindwa kuyaunganisha makundi. If it were me, I would have created some positions for a few individuals who had administrative roles from the outgoing administration.........
Nadhani hao viongozi walio achwa wao ndo walipanic mapema. Definately kama wangekuwa watulivu na kuendelea ku support chama eventually wangetafutiwa nafasi fulani fulani. Lisu asingewaacha wafe njaa.

Lakini wao ndo hawa kumpa Lissu nafasi ya kuwaamini na ku create hizo nafasi.

Uongozi mpya hata haujamaliza mwezi tayari wamesha anza kuupinga kwa kuitisha press conference na kuongea vibaya kuhusu Lissu.

Wangejifunza kwa wenzao wa CCM pindi wanapovuliwa uongozi kama uwaziri wana kaa kimya hata kama imewauma lakini wanakaa kimya na kuendelea na maisha eventually wanatafutiwa nafasi zingine au kurudishwa.

Sasa wao waachwa leo, Kiongozi mpya bado anajipanga tayari wameanza kumgeuka. Acha waende. Hawakuwana nia ya dhati ndani ya Chadema zaidi ya masilahi.
 
Benson Kigaila ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara amesema yeye na Wanachama wenzake wamejitoa katika chama hicho kutokana na kutoridhishwa na yanayoendelea

Ametangaza uamuzi huo akiwa pamoja na aliyekuwa Makamu wa CHADEMA Taifa - Zanzibar, Salum Mwalimu, aliyewai kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita

View: https://www.youtube.com/live/Z_apgr0qkZM?si=Lj9DabbYPf6LP8KC

View attachment 3326774
===

Updates

Katika mkutano huu na waandishi wa habari wajumbe wote wa sekretarieti ya CHADEMA Taifa iliyopita wapo isipokuwa watu wawili ambao ndiyo hawakuwepo hapo kwa mujibu wa John Mrema. Ambao ni;
  • Catherine Ruge - Aliyekuwa Katibu Mkuu BAWACHA-Taifa
  • Julius Mwita - Aliyekuwa katibu wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa
  • John Mrema - Aliyekuwa Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje
  • Salum Mwalimu - Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu CHADEMA, Zanzibar
  • Benson kigaila - Aliyekuwa Naibu katibu mkuu CHADEMA, Bara
Wanaeleza kuwa baada ya ushindi, Freeman Mbowe alikubali maridhiano yawepo mara baada ya makundi yaliyopo wakati wa kampeni, ila walishangazwa na kumuona aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti Tundu Lissu aliendelea kumshambulia Freeman Mbowe kama vile kampeni bado zinaendelea, ameeleza Benson Kigaila.
View attachment 3326841
Kigaila anaendelea kueleza kuwa Kuna makundi ngazi ya chini kwenye chama wana vikao vya kuwaengua ama kuwafuta uanachama wanachama waliokuwa wanamuunga mkono Freeman Mbowe.

Wanaeleza pia kuwa ndani ya Chama kuna udikteta uchwara na hivyo wapo kwa ajili ya kuupinga udikteta huo ndani ya chama. Aidha hakuna haki ya kusikilizwa ndani ya chama wala hakuna haki ya watu kuhoji na wanaofanya hivyo wanaitwa wasaliti, njaa. Wanahoji Je, kati ya wao na aliyepinga maridhiano chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe nani msaliti?

G-55 wanasistiza kama unataka kuzia uchaguzi na hakuna mkakati wa kuzuia uchaguzi maana yake umeamua CCM wapite bila kupigwa.

Rasmi wamesema wamejiondoa CHADEMA lakini hawatokwenda CCM, muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia. Sababu kubwa ni kutokutaka kuwa sehemu ya kifo cha CHADEMA kutokana na yanayoendelea. Hayo yamesemwa na Benson Kigaila aliyekuwa Naibu katibu mkuu Chadema (Bara)
View attachment 3326835

Soma pia:

Benson na Mrema kuna majibu yenu huku hahahaa
 
Back
Top Bottom