Kupitia ukurasa wake wa X, John Mrema ametangaza leo kuwa na mkutano na waandishi wa habari Golden Tulip, Masaki.
View: https://www.youtube.com/live/Z_apgr0qkZM?si=Lj9DabbYPf6LP8KC
View attachment 3326774
===
Updates
Katika mkutano huu na waandishi wa habari wajumbe wote wa sekretarieti iliyopita wapo isipokuwa watu wawili ambao ndiyo hawakuwepo hapo kwa mujibu wa John Mrema. Ambao ni
Catherine Ruge - Aliyekuwa Katibu Mkuu BAWACHA-Taifa
Julius Mwita - Aliyekuwa katibu wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa
John Mrema - Aliyekuwa Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje
Salum Mwalimu - Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu CHADEMA, Zanzibar
Wanaeleza kuwa baada ya ushindi, Freeman Mbowe alikubali maridhiano yawepo mara baada ya makundi yaliyopo wakati wa kampeni, ila walishangazwa na kumuona aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti Tundu Lissu aliendelea kumshambulia Freeman Mbowe kama vile kampeni bado zinaendelea, ameeleza Benson Kigaila.
Kigaila anaendelea kueleza kuwa Kuna makundi ngazi ya chini kwenye chama wana vikao vya kuwaengua ama kuwafuta uanachama wanachama waliokuwa wanamuunga mkono Freeman Mbowe.
Wanaeleza pia kuwa ndani ya Chama kuna udikteta uchwara na hivyo wapo kwa ajili ya kuupinga udikteta huo ndani ya chama. Aidha hakuna haki ya kusikilizwa ndani ya chama wala hakuna haki ya watu kuhoji na wanaofanya hivyo wanaitwa
wasaliti,
njaa. Wanahoji Je, kati ya wao na aliyepinga maridhiano chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe nani msaliti?
G-55 wanasistiza kama unataka kuzia uchaguzi na hakuna mkakati wa kuzuia uchaguzi maana yake umeamua CCM wapite bila kupigwa.
Rasmi wamesema wamejiondoa CHADEMA lakini hawatokwenda CCM, muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia. Sababu kubwa ni kutokutaka kuwa sehemu ya kifo cha CHADEMA kutokana na yanayoendelea. Hayo yamesemwa na Benson Kigaila aliyekuwa Naibu katibu mkuu Chadema (Bara)
Soma pia: