Baadhi ya hospitali binafsi zilizotangaza kutotoa huduma kwa wateja wa NHIF kuanzia 1/3/2024

Mkuu ni kawaida ya CCM kutengeneza matatizo, ili baadaye waje wayatatue wasifiwe...

Hata hili muda si mrefu utasikia wametatua ili wapate sifa...
Umewaza kama mimi.

Watakuja na suluhisho na majigambo juu mithili ya kuwa hilo tatizo lilianzishwa na serikali nyingine kabisa.
 
Serikali ndio imetufikisha hapa na sidhani kama ina namna ya kujinasua kutoka kwenye hili janga. Huu ujinga wa serikali kuweka bei elekezi kwenye masuala ya msingi kama afya, litatufikisha mahali pabaya sana. Wameweka bei elekezi kwenye sukari watu wameshindwa kunywa chai. Sasa wamehamia kwenye afya ili kuua raia wasiokuwa na hatia. Sijawahi kuona serikali yenye mambo ya kipimbavu kama hii.
 
Kinachouma na kukera zaidi, mbali ya kuwa na huduma za kusuasua kwa watumiaji wa NHIF, pesa zetu hawajaacha kuzichukua.

Ukienda hospitali zao sasa hizo za Serikali, huduma mbovu kupita maelezo.
 
Tatizo kwani ni nini, tiririka mleta mada ili tuelewe, umetuwekea mgomo lakni haujasema chanzo ni nini.
Tatizo lako vyanzo vyako vya habari unavipata kwa Lucas, sasa unategemea Lucas atakupa update gani ya maana inayoendelea kwenye uhalisia wa huu ulimwengu? Kama kila saa anaandika na kumsifia mama anaupiga mwingi na yeye ndio chanzo chako cha kuaminika basi sahau ya duniani
 
Serikali ndio imetufikisha hapa na sidhani kama ina namna ya kujinasua kutoka kwenye hili janga. Huu ujinga wa serikali kuweka bei elekezi kwenye masuala ya msingi kama afya, litatifikisha mahali pabaya sana. Wameweka bei elekezi kwenye sukari watu wameshindwa kunywa chai. Sasa wamehamia kwenye afya ili kuua raia wasiokuwa na hatia. Sijawahi kuona serikali yenye mambo ya kipumbavu kama serikali hii ya CCM.
 
Nhif walisema wenye shule ipeleke package ya wanafunzi miamoja shule imefikisha watoto mia moja kuwapelekea wanakataa wanataka wenye shule wawalipie wanafunzi wote walionao shuleni na hawajatoa waraka kwa wananchi
 
Umi Mwalimu bado yupo Ofisini tu, hataki kujiuzulu kwa kushindwa na kusababishia serikali lawama Toka kwa wananchi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Hapo bila kumtaja Naibu wake Dr Mollel ambaye hana tofauti na Suphian au Mpoto kwa kuwa vuvuzela kazi ni kumsifia Rais Samia badala ya kumsaidia ushauri
 
Nashauri wafute bandiko lao, waombe kukaa dawati moja na mamlaka, waone wanatatuaje?, kusitisha huduma kwa ghafla, ni uuwaji dhahiri wa waziwazi.
Wewe kichwa maji kweli!!Upo nchi hii kweli?Barua yao ya awali inayosema wamekaa meza moja na wameshindwa kupata mwafaka umeisoma???Tatizo lako ni UMALAYA wa KISIASA ulionao .
 
Mbona vyawa hatuwaoni wakiitetea serikali kwenye hili.

Pumzi imekata au wanaandaa nondo.
 
Hiyo ni medical negligence, worst unaweza pewa kesi ya manslaughter, malizia huduma uliyoanza kutoa; na uwezi kukatisha mkataba wa huduma katikati.
Nadhani hapo wametoa huduma ya awali kwa siku mbili.
Kumbuka nao wanafanya biashara tatizo nikwamba hawajafikia muafaka. YAANI SERIKALI IMEANGALIA MASLAHI YAKE KWAHIYO UNATAKA HOSPITALI BINAFASI NDIO ZIGHARAMIE MATIBABU YA WANANCHI?
 
hizi hospitali ni za ajabu wamehusishwa mwanzo mwisho,kwenye mchakato mzima wa kutengeneza kitita hicho
Hata wewe unaweza kuhusiahwa kwenye mazungumzo lakini usiridhike na maamuzi. Rejea hata kesi zinavyofanyika na matokeo ya hukumu halafu angalia lawama na vilio
 
Nashauri wafute bandiko lao, waombe kukaa dawati moja na mamlaka, waone wanatatuaje?, kusitisha huduma kwa ghafla, ni uuwaji dhahiri wa waziwazi.
Unafikiri nani anatakiwa aanze kuwajibika?
Waziri siku zote anaziruratu ameshindwa kuweka mambo sawa kisha leo ndio iwe lawama upande mmojatu?
Lawama zaidi kwa waziri
 
hizi hospitali ni za ajabu wamehusishwa mwanzo mwisho,kwenye mchakato mzima wa kutengeneza kitita hicho
Na wao walitoa mapendekezo yao, lakini yamepuuzwa na Nhif na serikali, unategemea wafanye nini!!? Wakikaa kimya muda si mrefu watafunga vituo kwa kushindwa kuendesha, ndio maana wameona ni afadhali kuacha kutoa huduma ili iwafanye Nhif na wizara wakubali kukaa chini kuweka sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…