Baadhi ya hospitali binafsi zilizotangaza kutotoa huduma kwa wateja wa NHIF kuanzia 1/3/2024

Baadhi ya hospitali binafsi zilizotangaza kutotoa huduma kwa wateja wa NHIF kuanzia 1/3/2024

TikTok2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2022
Posts
1,816
Reaction score
3,150
IMG-20240301-WA0000.jpg
IMG-20240301-WA0001.jpg

IMG-20240301-WA0002.jpg

Baadhi ya hospital binafsi zimeshaweka matangazo kama yanavyosomeka hapo juu

Nini sulihisho la hili?tiririka ili serikali ipate madini na kuyafanyia kazi inawezekana kabisa hawajui nini cha kufanya kunusuru hilo suala nyeti la afya.
 
Salaam,

Mgomo uliotangazwa kuanza na hospitali binafsi dhidi ya bima za NHIF umeanza rasmi ilipotimu tar. 1.3.2024.

Hii inamaanisha ukienda na bima yako ya NHIF kwenye hospitali binafsi hupatiwi huduma, na wagonjwa mahututi wameongezewa masaa 48 (siku 2) tu kuendelea kupata huduma hizo kama mambo hayatabadilika.

Hali ikoje kwenye hospitali binasi karibu yako? Vipi upande wa serikali?
 
Uwezi mpa mgonjwa mahututi masaa 48 huko ni kukosa busara na medical ethics. Lazima umalizie huduma uliyokwisha anza kuitoa.

Ndugu zake wangeyajua hayo wasingempeleka huko, nchi zingine utaingia kwenye mgogoro mkubwa wa kisheria kwa maamuzi hayo watu wakipoteza maisha.

Hiyo ni medical negligence, worst unaweza pewa kesi ya manslaughter, malizia huduma uliyoanza kutoa; na uwezi kukatisha mkataba wa huduma katikati. Hao mahututi wakipata madhara hospitali aiwezi shinda kesi ndugu au serikali ikiwashitaki.
 
Nashauri wafute bandiko lao, waombe kukaa dawati moja na mamlaka, waone wanatatuaje?, kusitisha huduma kwa ghafla, ni uuwaji dhahiri wa waziwazi.
"mgomo wa walimu, mgomo wa wafanyakazi migodini hii huwa haisababishi vifo, lakini mgomo mahospitalini huu ni kuua watu waziwazi.
 
Ummy na bosi wa NHIF waliwe vichwa, kazi imewashinda. Alafu ndio huyuhuyu anakimbilia kutaka bima ya afya kwa wote, kama hii tu ya wafanyakazi inawashinda hiyo ya walala hoi wataiweza? Upumbavu mtupu.
Swala la poor calculation litakuwa linahusika hapa, kinachoingia kidogo, madai yanakuwa makubwa triplex, nadhani ndio tatizo hapa, uchumi wa watu ni mdogo mno kuweza kulipia bima stahili. Pamoja na serekali kuweka viwango vyake!, Mambo ya bima huwa hayapatani na nchi zenye uchumi duni hasa kwa wananchi wake walio wengi.
 
Back
Top Bottom