Baadhi ya kina kaka/baba acheni kelele na ukorofi

Baadhi ya kina kaka/baba acheni kelele na ukorofi

Sijui hata nseme nn anyway ngoja nkapitie vgezo huenda nikawa navyo!
 
Hebu fanya mpango wa elfu 2 hapo nisogee kwa mama ntilie, nijibless mchana huu.
 
Kila nikisoma nyuzi zako, ubongoni huwa najiwa na picha ya Faiza

10613039_787398244667237_8120089490035739155_n%2B(1).jpg
 
Kila nikisoma nyuzi zako, ubongoni huwa najiwa na picha ya Faiza

10613039_787398244667237_8120089490035739155_n%2B(1).jpg
Tulia na acheni kelele, nimefunga mjadala leo. Lakini kwa kweli baadhi ya wanaume wa Wakitanzania mnapenda kubweka mnoo. 🙏🙏
 
Nilikaa kimpya sikujibu nilikuwa nawacha nisome maoni yenu kwanza halafu nikupeni update sasa. Na sasa nafunga huu mjadala na pia natumai mnaotaka mke sasa kama bado mmo sasa tulieni. Na mnao thani humu nimetowa pesa mimi sijampa hata shilingi nahisi ilikuwa ni kuchezeana akili.

Huyu mwamba tunamuengelea hapa nahisi hana shida lakini kaamuwa kunipima mimi kwa pesa. Au anataka nambari yangu kwa lazima baada ya kumkatalia,sasa katumia njia ya mimi kumkopesha.

Halafu alivyo kwenye level yake fulani mwenyewe kakaa kimpya anasikiliza tu, watu huku wakidata!!

Sasa nakupeni funzo sipimwi mimi kwa pesa na pimwa kwa integrity, mwanaume mwengine asirudie tena. Sithani mimi kama alikuwa anataka pesa nahisi alikuwa na papara tu la kunizalimisha mimi kutowa nambari yangu kwa lazima basipo mimi kuwa tayari.

Sisi huku hatupimani kwa pesa bali kwa mtu kuwa mkweli na muaminifu kwa sababu maisha ya huku ni 50:50 kuwa mnasaidiana majukumu. Na kama mtu hufanyi kazi serikali wanakupa pesa za kuishi.

Nasema hana shida kabisa nahisi hivi kwa sababu pesa alosema nimkopeshe ni ndogo mnoo. Ambayo mimi huku nanunulia kahawa au chai ya asubuhi tu na kama angekuwa na shida kweli angeomba zaidi.

Halafu kafanya hivi baada ya siku 2/3 kumjua hapa jukwaani ndio kabisa nahisi alikuwa ananipima mimi pesa au labda kunizalimisha kwa kila namna kutaka kuipata nambari yangu na kushindwa kuvumilia.

Nimetowa hii mada nje makusudi kuwafunza baadhi ya wanaume humu waache hii thana potofu kwamba kila mwanamke wanataka pesa zao, ambayo sio kweli na nahisi wazowee tu kwa sababu sasa wanawake tunajitegemea na hatutegemei waume.

Vile vile kama baadhi ya wanaume humu pia muna papara niwacheni kuwa mimi sitaki papara wala kelele nilisema tangu mwanzoni mimi ni mtu ninaependa amani/utulivu na furaha wakati wote.

Amefanya utumbo huu baada ya kutaka urafiki na mimi baada ya kumkatalia ndoa baada ya kudai kwamba ana vigezo vyote na kutaka nambari yangu.

Nimemkatalia ndoa hata kumpa nambari yangu kwa sababu hakutaka kusema mambo yake hapa na kila ninachomuuliza hapa jukwaani hataki kujibu lazima nimpatie nambari yangu na tuongee kwa WhatsApp.

Nilikwazika mnooo kwa kutotaka kufunguka na kuwa muwazi sasa. Wakati mimi nimesema kila ninachoulizwa hapa jukwaani kuwa niko muwazi.

Narudia tena nahisi hana shida kabisa na hapa sasa nakujuzeni kuwa, anabiashara yake na huwa anakuja huku London kila mara na hukaa huku nusu mwaka.

Kayasema haya yote baada kujuwa kwamba siwezi kuendelea na yeye asiponijibu maswala yangu hapa jukwaani, mbali ya kutomkopesha pesa aliyotaka.

Na baada ya yote yanayoendelea hapa jukwaani wala habari hana na bado anaendelea kunikera hapa jukwaani kwa kutaka sasa kunitia kwenye biashara yake huku London, kama vile mimi nilisema niko hapa kutafuta urafiki au kazi/biashara ya kufanya.

Simuelewi na nawaombeni sasa baadhi ya wanaume humu kama muna vigezo vyangu vyote, kwanza muwe watulivu, pili muwe wawazi (acheni ukorofi), tufahamiane na mimi nambari yangu nitatowa nikiwa tayari.
Daah Bibie aisha assalaaam aleikum, waislam tunafichiana aibu Bibie! Je kulikuwa na haja gani nikuexpose mie humu jukwaani? Si tuliongea tukayamaliza? Daaah
 
Back
Top Bottom