Baadhi ya Lecturers wa Mzumbe wana degree Feki - VC wao naye FEKI

Baadhi ya Lecturers wa Mzumbe wana degree Feki - VC wao naye FEKI

Hapo tunawapa hongera vijana, naona wanaanza kuandokana na minyonyoro ya kukosa self confidence!
 
Makala
Mzumbe: Tumedhihirisha elimu ya Tanzania ni bora A. Mashariki


*Wawaangusha Makerere katika shindano la Celtel
*Wafuata nyayo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Na Joster Mwangulumbi

HATA kabla ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, kuondoka nchini kwenda Nairobi, Kenya kwa shindano la Chemshabongo ya Celtel Afrika maarafu kama Celtel Africa Challenge, kulikuwa na hali ya woga na kukatishwa tamaa na wenzao.

Hiyo ilitokana na fikra zilizojengeka miongoni mwa watu, hata wasomi, kwamba elimu ya Tanzania iko chini ya kiwango ikilinganishwa na Kenya na Uganda. Kwa mtazamo huo pambano la chemshabongo kati ya chuo hicho na Makerere cha Uganda ilichukuliwa kuwa sawa na pambano la Daudi na Goliath katika Biblia Takatifu. Mzumbe hawakupewa nafasi ya kuwaangusha Makerere (kilianzishwa mwaka 1922) sawa na Daudi ambavyo hakupewa nafasi ya kumuangamiza Goliath.

Lakini akitumia silaha aliyoiamini ya kombeo, Daudi alilenga shabaha barabara jiwe likampata sawia na kumua papo hapo jemedari mwenye majigambo na silaha nzito Goliath. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Mzumbe dhidi ya Makerere na mmoja wa washiriki hao, Noel Benjamin Mazoya anaeleza hali ilivyokuwa.

"Hata wakati tunaondoka chuoni maswali kama haya yalianza kutolewa. Hivi ninyi mnakwenda kushindana na Wakenya? Ninyi mtawaweza Waganda? Hivi ninyi mnawafahamu Wakenya," anaeleza Mazoya katika mahojiano na mwandishi wa makala hii wiki iliyopita.

"Maswali haya ni kilelezo cha fikra potofu. Kwa hiyo ukiacha ushindi tulioupata, lengo letu lilikuwa kufuta fikra kama hizi, kuondoa hali hii ya sisi Watanzania kujiona watu wa chini mbele ya Wakenya na Waganda, kuonyesha kuwa si kweli kwamba elimu ya Tanzania iko chini," alisisitiza Mazoya kijana mwenye umri wa miaka 21.

Kazi ya kuthibitisha hilo ilikuwa ngumu kwani baada ya kufika mjini Nairobi kwa ajili ya shindano hilo vibweka na kelele za washiriki wa Makerere zilikuwa nyingi na hata vyuo vingine vya Kenya na Uganda washiriki wao walikuwa na mbwembwe na kauli za vitisho dhidi ya washiriki kutoka vyuo vya Tanzania.

"Tulifika kwa pamoja na Waganda. Waganda walianza kuonyesha ujuaji na majigambo na kujiona wao bora zaidi yetu, lakini nasi tulionyesha ari. Kwa kweli sisi hatukuwa na mbwembwe lakini tulijiamini na kocha wetu Profesa Faustin Kamzora alitujengea uwezo, ari na kujiamini," anasisitiza Mazoya ambaye alikuwa mchezaji wa akiba.

Hadi wakati Mzumbe wanashiriki tayari Tumaini na Zanzibar walikuwa wametolewa kwa hiyo ilipofika zamu yao, walijiona na wajibu mkubwa wa kufanya marekebisho kufuta dhana kwamba hata washiriki wengine kutoka Tanzania wangeburuzwa.

Siri ya mafanikio ya Mzumbe
Mambo matatu makubwa ndiyo yaliyochangia timu ya Chemshabongo ya Mzumbe kufanya vizuri katika shindano lile.

"Nafikiri kwanza mafanikio yetu yamechangiwa na vitu viwili vitatu hivi. Kwanza ni mchango wa kocha wetu Profesa Kamuzora, alikuwa msaada mkubwa kwetu. Tangu mwanzo alikuwa mtu aliyejitoa kwa dhati kuhakikisha tunafanya vizuri katika shindano hili kwani muda wote alikuwa nasi anatuhamasisha na kutupa mbinu za kufanya vizuri," anaeleza Mazoya.

"Pili tulikuwa tumedhamiria kuonyesha na kuondoa fikra potofu kwamba wenzetu wa Kenya na Uganda, kielimu wako mbele yetu, kwa hiyo tulijipanga sawia ili tuweze kufuta fikra hizo na tunamshukuru Mungu tuliweza japokuwa mashindano bado yanaendelea.

"Tatu ni mazoezi ya kutosha tuliyofanya. Tulifanya mazoezi kwa muda wa wiki mbili. Wiki ya kwanza ulikuwa muda wa kutafuta timu ya kushiriki ambapo wanafunzi wengi walishiriki. Tulifanya mtihani wa kwanza wa kuandika tukachujwa hadi tubaki 20 na hatimaye tukabaki wanne na wiki ya mwisho ilikuwa ya maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya shindano," anafafanua mchakato ulivyokuwa.

Wanafunzi mbalimbali, bila kujali mwaka au shahada walishiriki katika mchakato wa kupata timu ya kushiriki na hatimaye Mazoya, kijana wa mwaka wa kwanza anayesomea shahada ya Uhasibu akateuliwa pamoja na Deogratius Kibona aliyeko mwaka wa pili akisomea shahada ya Uongozi wa Biashara.

Washiriki wengine ni Lusekelo Kasongwa aliyeko mwaka wa tatu akisomea shahada ya Uhasibu na Fedha na Evarist Alphonce ambaye pia yuko mwaka wa tatu akichukua shahada ya Uhasibu na Fedha. Timu ilitakiwa kuwa ya mchanganyiko lakini kwa bahati mbaya washindi wakawa wanaume tu. Kibona, Kasongwa na Alphonce ndio walijibu maswali huku Mazoya akiwa mchezaji wa akiba.

Katika shindano la Celtel Africa Challenge, washiriki hupimwa si kwa mambo waliyosoma darasani pekee bali uelewa mpana wa mambo mengi tofauti katika jamii kuhusu maisha ya kawaida.

Kitu ambacho Cetltel Africa Challenge inataka kuonyesha ni ushirikiano wa timu katika kujibu maswali badala ya kutegemea uwezo au akili ya mtu mmoja tu.

Wanafunzi huulizwa maswali ya kawaida kuhusu fasihi, sayansi, historia, jiografia, dini, sanaa, sayansi ya jamii, na ufahamu wa kawaida na hasa masuala ya maisha ya kawaida kama utamaduni na michezo.

Kila timu inakuwa na washiriki/ wachezaji wanne lakini mshiriki mmoja huwa wa akiba, washiriki watatu ndio hukaa mbele kushiriki. Timu ikiulizwa swali la msingi humteua mshiriki mmoja kujibu, wakipata hupewa swali la bonasi ambalo lina alama nyingi zaidi.

Timu mbili ndizo hushindana na katika kila shindano kuna raundi tatu ambazo hutoa fursa kwa kila mshiriki kujibu. Mchezaji anayekuwa mbele kujibu maswali ikiwa atapata jibu katika swali la msingi lenye alama 10 ataongezewa swali la bonasi lenye alama 20 ambalo timu hujadiliana na mmoja kujibu.

Kikubwa katika shindano hili ni muda unaotumika katika kujibu maswali. Muda uliopangwa katika raundi ni dakika sita. Baada ya kumaliza raundi tatu, timu zote mbili hushiriki katika awamu ya mwisho ya kujibu maswali 10 kwa sekunde 60 tu.
Mzumbe walimudu yote hayo na wakashinda kwa pointi 700 dhidi ya pointi 540 walizopata Makerere. Hadi tunakwenda mitamboni juzi Jumapili, Chuo Kikuu cha Sokoine kilikuwa kinachuana na Nkumba cha Uganda.

"Uelewa wa wanafunzi wetu ni mkubwa sana, labda kama kuna kitu wanachokosa ni kujiamini tu. Kwa hiyo nilichofanya mimi nilijaribu kuwajengea hali ya kujiamini katika kujibu maswali," anasema Profesa Kamuzora alipoelezea alivyowaandaa vijana wake.

Profesa Kamuzora anashauri watoto wafundishwe jinsi ya kujiamini kuanzia nyumbani, wasikatishwe tamaa, wafundishwe kuwa watu wenye kujiamini kila wanapofanya jambo fulani na wapewe moyo.
Anashauri pia wafundishwe namna ya kujifunza na kwamba si kila kitu kitapatikana kutoka darasani, wafundishwe kusoma vitabu mbalimbali kwa ajili ya kupata ufahamu wa kawaida.

Mazoya anaafiki ushauri wa Profesa kamuzora akisema: "Kama kuna kitu tunakikosa sisi kwenye mitaala yetu labda hatujaingiza masuala ya mtandao tu, humo yanapatikana mambo mengi ya masomo, historia na ufahamu wa kawaida."

Akaongeza: "Nilimwelewa vizuri kocha wetu na nikajitahidi kutoa ushirikiano huo kwa wenzangu. Wakati wa mashindano kocha alitoa mchango mkubwa sana kwani alituambia kwamba shindano hilo ni la kucheza na akili, hakikisha akili zenu zimetulia, msipaparike wala msisumbuliwe mkiona wenzenu wamejibu vizuri na hakika ushauri huo ulitusaidia, kwani alikuwa sehemu ya ushindi."

Mbali ya Mzumbe na Sokoine, vyuo vingine kutoka Tanzania ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, Tumaini na Zanzibar. Uganda ni Chuo cha Kiislam Uganda, Makerere, Mbarara, Ndejje na Nkumba wakati wenyeji ni Chuo Kikuu cha Katoliki, Egerton, Kenyatta, Moi, Chuo Kikuu cha Nairobi na Chuo Kikuu cha Uhusiano wa Kimataifa cha Marekani cha mjini Nairobi.

Kamati maalum iliyoundwa kwa ushirikiano na Baraza la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki (IUCEA) iliketi na kuteua vyuo hivyo kutoka Afrika Mashariki, lakini miaka ijayo Celtel inatarajia kuvishirikisha vyuo vikuu vya Afrika nzima.
 
Si wameshatolewa na chuo cha Kenyata au???!!!

Wanafunzi sio wabaya, tatizo letu ni baadhi ya waalimu wao kujipa Phd feki!!!!

FD
 
yes wametolewa na kenyata ila wameonyesha jitihada za hali ya juu sana sana,kwa hilo nawapa pongezi. Nungwi hongera chuo ukipendacho kimeonyesha kujiamini
 
Kuna mtu alitaka kujua Phd feki asome hii thread.atajua PWU ni chuo cha namna gani.
 
Kama Kuna Malecturer Feki Then Ni Bora Selikari Itathimin Ilo,kwa Suala La Ufeki Wa Degree Limetapakaa Sehemu Nyingi.wahusika Wanalifahamu Ila Wanalinda Maslai Ya Wenzao.

Pamoja Na Tetesi Izo Za Ufeki Wa Baadhi Ya Malecturer Pale Mu Product Za Mzumbe Sokoni Zinatisha.so Vijana Wa Mu Msikate Tamaa Na Wale Wanaotaka Jiunga Na Mu Wasikate Tamaa Kwani Samaki Waliooza Ni Wachache.
 
Mwakasege.
Ngumu kuamini kuwa samaki waliooza ni wachache. hujui mhadhiri gani ataingia darasani kwako.na VC ndio hivyo hili linaharibu credibility ya Chuo kabisa.
na hawa watu kuendelea kukaa madarakani ni kuhalalisha uozo huo.kweli kabisa ukimalza Mzumbe hivi sasa unakuwa huna Confidence kabisa.
 
Wandugu,
Prof. Nkunya (Then Chief Academic Officer-UDSM) - is now working with Tanzania Commission of Universities (TCU)as CEO. http://www.tcu.or.tz. Former Higher Education Accreditation Council (HEAC). He is a renowned Professor in Chemistry. He is a man of quality- hope he will seek to ensure that our Universities have Qualified Staff. Juzi ametoa 'Mkwara' IMTU kile ya Wahindi- watafute waalimu qualified or else hakuna new students enrolment 2007! This should also apply to other institutions! Je tunao waalimu wa kufundisha new Universities?
 
HIlo ndiyo swali la msingi haswaa. Tunao waalimu wa kufundisha vyuo vipya, wakati sasa hivi tu vijana wanaofanya vizuri kwenye masomo yao wanang'ang'aniwa na vyuo walivyosomea, that means huko mtaani hawapo watu wenye sifa zao! Zaidi sana vyuo haviangalii hata uwezo wao katika kufundisha, inawezekana jamaa alimeza halafu vikatoka alivyomeza!
 
Labda Professor anaweza akaamsha ari, lakini asije kuwa kama Msola kwani tulijua anzijua shida za wanafunzi vyuoni anaweza akasaidia zaidi pale alipochaguliwa na Mh. Kikwete kuwa waziri wetu, look at what happened, ndiyo amekuja kutumaliza kabisa na board ya ke y mikopo yenye masharti kibao ikiwepo hata kupangiwa rate ya mkopo bila kujali mtu alikotoka na uwezo wake!
 
Labda Professor anaweza akaamsha ari, lakini asije kuwa kama Msola kwani tulijua anzijua shida za wanafunzi vyuoni anaweza akasaidia zaidi pale alipochaguliwa na Mh. Kikwete kuwa waziri wetu, look at what happened, ndiyo amekuja kutumaliza kabisa na board ya ke y mikopo yenye masharti kibao ikiwepo hata kupangiwa rate ya mkopo bila kujali mtu alikotoka na uwezo wake!

Janusqml,
Hii thread inaongelea Waalimu wenye PhD feki MU. Katika Elimu Vyuo Vikuu tunaongelea Quality including well qualified Staff. Nkunya is a full Professor with Quality Publications and Management Experience!
Ili tuondokane na hiki kizingumkuti cha PhD or degree feki- tunahitaji watu kama Nkunya ili kuensure high standard! Ndo maana UDSM is ranked 13th best University in Africa- naye amekuwa Chief Academic Officer UDSM for some years!
Je uko hapo?
 
Je tunao waalimu wa kufundisha new Universities?

..na vyuo vipya ndo vyajengwa kwa kasi!

..itabidi tutafute nje ya nchi!ama sivyo tuajiri wa kubabaisha kitu ambacho itakuwa afadhali tusingejenga hivyo vyuo!

..kazi ipo na si ndogo!
 
..na vyuo vipya ndo vyajengwa kwa kasi!

..itabidi tutafute nje ya nchi!ama sivyo tuajiri wa kubabaisha kitu ambacho itakuwa afadhali tusingejenga hivyo vyuo!

..kazi ipo na si ndogo!

DarsiLamu,
Hata hiki Chuo Kikuu Dodoma- ambacho tunasema kitakuwa na wanafunzi 40,000- where do we get GPA 3.8 and above kama ilivyo kwa UDSM? Or we shall compromize the quality
As a strategy,
1. Higher Learning kwa sasa UD, MU, SUA n.k waanze mpango to retain all undergraduate students with GPA 3.8 and above ili waje wawe waalimu in existing and new Universities- this should be a very urgent matter! Sijui kama Msolwa tayari hili ameliona!
2. Serikali iwahamashishe wenye Masters (who qualify with GPA 3.5 in ungergraduate & above) PhD na waanze na kupenda kufundisha at Universities. New incentives are needed!
 
IMTU isaidiwe kurekebisha kasoro zilizopo (Maoni)-MWANANCHI

TUME ya vyo vikuu Tanzania (TCU), wiki iliyopita ilikizuia Chuo cha Kimataifa cha Tiba (IMTU) cha dar es Salaam kusajili wa wanafunzi wapya wa fani ya udaktari, kutokana na kushindwa kutimiza baadhi ya masharti waliyopewa.

Kutokana na uamuzi huo, chuo hicho kinashindwa kuwachukua wanafunzi ambao walitakiwa kuanza mwaka wa kwanza chuoni hapo kusomea taaluma ya udaktari.


Uongozi wa chuo hicho unalalamika kuwa barua ya TCU waliyopelekewa haijafafanua vigezo ambavyo wanatakiwa kuvikamilisha, ukiachilia mbali maelezo ya jumla waliyopewa awali na tume hiyo.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya IMTU, Srinivasa Rao, chuo hicho kilitakiwa kuonyesha sera ya mpango wa elimu, kuongeza madarasa, viti pamoja na kujenga jengo litakaloweza kuchukua wanafunzi 150, mambo ambayo alisema tayari wameyakamilisha kwa asilimia 50.


Ni kweli kwamba katika kipindi kama hiki ambacho watu na taasisi binafsi zinaanzisha shule na vyuo kila kukicha, kuna umuhimu mkubwa kwa serikali kupitia taasisi zake mbalimbali kuhakikisha kuwa inasimamia utoaji wa elimu kwa Watanzania.


Usimamizi unahitajika kwa sababu endapo kila kitu kitaachiwa kwenda holela, upo uwezekano mkubwa wa Watanzania kulishwa elimu duni isiyozingatia vigezo vinavyohitajika na matokeo yake kutoa watalaam wababaishaji katika sekta mbalimbali.


Lakini ni kweli vile vile kwamba katika kipindi hiki cha utawala wa serikali ya awamu ya nne, mkazo mkubwa umewekwa katika uimarishaji wa elimu, kuanzia ngazi ya chini ya shule za msingi hadi katika vyuo vikuu.


Chuo Kikuu cha IMTU ni miongoni mwa vyuo vichache Tanzania vinavyotoa elimu ya udaktari, inayohitajika mno katika jamii yetu.


Pamoja na matatizo yaliyojitokeza miaka ya nyuma, chuo hicho kimeweza kutengeneza madaktari ambao hadi sasa wnafanya kazi katika hospitali mbalimbali hapa nchini, na hivyo kuchangia juhudi za serikali za kuongeza idadi ya madaktari nchini.


Wakati juhudi zinazofanywa na Tume ya Vyuo Vikuu katika kudhibiti utoaji wa elimu sahihi na katika mazingira yanayotakiwa zinatakiwa kupongezwa, lakini serikali na taasisi nyingine katika jamii zinao wajibu mkubwa wa kusaidia taasisi kama IMTU ili ziboreshe mazingira yake na kuzidi kuendelea na kazi ya kutoa taaluma hiyo muhimu kwa Watanzania.


Mpaka sasa tunao Watanzania wengi wanaokosa kupata nafasi ya kusoma katika vyuo vya elimu ya juu kutokana na uhaba wa nafasi zilizopo katika vyuo vya umma na vile vya binafsi.


Taarifa za karibuni kabisa kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma zinasema kuwa jumla ya watu 15,000 waliomba kujiunga na chuo hicho kinachoanza kutoka mafunzo ya shahada ya kwanza Septemba mwaka huu.


Hata hivyo, kati ya waombaji hao, ni waombaji pungufu ya 2,000 tu ndiyo waliofanikiwa kupata nafasi ya kuanza masomo katika chuo hicho, hii ikiwa na maana kwamba jeshi la watu zaidi ya 13,000 wamekosa nafasi katika chuo hicho peke yake.


Katika mazingira ya namna hiyo linakuwa si jambo la busara kukitupa chuo ambacho tayari kimetoa watalaam kutokana na kasoro ambazo zimejitokeza.


Jamii nzima ya Watanzania wanaoitakia maendeleo nchi yetu, kila mtu katika nafasi yake, wanatakiwa kupigania kuhakikisha chuo kama IMTU kinatimiza vigezo vinavyotakiwa ili kiweze kuruhusiwa kusajili wanafunzi kwa ajili ya mwaka ujao.


Kwa mujibu wa uongozi wa chuo hicho, tayari Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu imekwisha kuwalipia wanafunzi 25 wanaotarajiwa kuanza masomo ya udaktari katika mwaka ujao wa masomo.


Kama serikali imeonyesha moyo huo wa kuwasomesha vijana wake taaluma hii muhimu, basi watu wengine katika jamii tunao wajibu wa kuhakikisha kuwa harakati za utoaji elimu sahihi kwa vijana wetu hazikwamishwi na matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa kwa pamoja baina ya chuo hicho na mamlaka zinazohusika.



TCU HII NI KAZI NZURI- KEEP THE SPIRIT- NAONA NI MATUNDA YA PROF. MAYUNGA NKUNYA
 
DarsiLamu,
Hata hiki Chuo Kikuu Dodoma- ambacho tunasema kitakuwa na wanafunzi 40,000- where do we get GPA 3.8 and above kama ilivyo kwa UDSM? Or we shall compromize the quality
As a strategy,
1. Higher Learning kwa sasa UD, MU, SUA n.k waanze mpango to retain all undergraduate students with GPA 3.8 and above ili waje wawe waalimu in existing and new Universities- this should be a very urgent matter! Sijui kama Msolwa tayari hili ameliona!
2. Serikali iwahamashishe wenye Masters (who qualify with GPA 3.5 in ungergraduate & above) PhD na waanze na kupenda kufundisha at Universities. New incentives are needed!

...mbona hilo linafanyika sana,at least kwa ud!

...labda waongeze juhudi.na ninadhani udasa wanalifanyia kazi hili kama bado,haya wake up call hiyo toka kwa mzalendo mwenzenu!

...ama sivyo sijui!

...halafu,walimu tumewatupa muda mrefu [nafahamu maslahi yao ni afadhali kuliko awali],sasa ni wakati wa kuangalia hilo nalo!
 
...mbona hilo linafanyika sana,at least kwa ud!

...labda waongeze juhudi.na ninadhani udasa wanalifanyia kazi hili kama bado,haya wake up call hiyo toka kwa mzalendo mwenzenu!

...ama sivyo sijui!

...halafu,walimu tumewatupa muda mrefu [nafahamu maslahi yao ni afadhali kuliko awali],sasa ni wakati wa kuangalia hilo nalo!

Dar Si Lamu,
Kama UD wana policy to retain best students as TA sijui- kuna wakati waliacha kuajiri na ndo maana kuna Maprofessor wengi watastaafu karibuni na kuna gap kubwa la replacement!
Swala hapa ni how to maintain quality in training so as to keep the high standards! Mimi bado naamini over quality ya Basic Training as entry point na siyo performance ya Masters- wengi waliofundisha UD wataafikiana nami! Cut off of 3.8 GPA and above nadhani ni nzuri!
Sijui kama MU na SUA have simila requiremens!
 
Hili linaonyesha viongozi wetu wamelala usingizi mzito or they just don't give a damn. Hili linazungumzwa mwaka wa tatu sasa na spika wabumnge alikabidhiwa majina ya wabunge wenye degree feki akasema atayafanyia kazi hakuna lolote lililofanyika. Baadaye akasema majina hayo yamekabidhiwa polisi, lakini hadi hii leo hatujasikia chochote. Tusishangae Watanzania tukianza kuogopwa duniani kwa kuwa na degree feki.
 
Back
Top Bottom