Baadhi ya Lecturers wa Mzumbe wana degree Feki - VC wao naye FEKI

Baadhi ya Lecturers wa Mzumbe wana degree Feki - VC wao naye FEKI

Nimesikitika sana kuona serikali zetu bado linaendelea kuwa na kigugumizi katika maswala muhimu ya elimu nilisoma Commonwealth Open University maelezo yake nikaona kuwa wanaweza kufanya customazation ya degree kutokana na mahitaji yako hii sentensi iliniboa sana na ndio maana unaweza kuwa unasoma master degree wakati huo unasoma phd katika vyuo tofauti sijaweza kuona kitu kama hiki. lakini kwa wale wanaotaka kupata just phd huna haja ya kupoteza muda hata bila first degree through Commonwealth Open University unaweza kupata phd. kwa maelezo zaidi wanotaka kusoma zaidi weka kwenye google Commonwealth Open University soma maelezo yake.

Anyway hili kuokoa taifa letu kuna haja ya kuangalia hivi vitu upya. Katika University of DSM nakumbuka zamani walikuwa wanaangalia vitu hivi sana kama kuna watu wanajulikana wana feki degree wewe mwaga tu nafikiri utapata majibu yake.

Pia lazima tukumbuke kitu kimoja kinachokabili taifa letu la tanzania tumekuwa muno wanasiasa watu wenye collification ambazo ni mara chache sana kuzipata wanakwenda kwenye siasa maana policy zetu zimeelekezwa sana kwenye siasa kuliko utaalamu ndio maana utakuta vyuo vinashindwa kupata watalamu hivyo vinaamua hata kuweka hao tu.

Natabiri kutokana na kasi hii ambapo vijana wanaona kuwa mwalimu wa chuo ni kama kujipigilia msumali, na wazee tu ndio wako vyuo vingi(halafu asilimia kubwa ni wa enzi za mwalimu na wanaelekea kustaafu) baada ya miaka kumi ijayo tutaitisha UPE kwenye vyuo vikuu vyetu.
 
Hivi, Mwalimu akiwa na feki degree, unategemea mwanafunzi anayetoka hapo anapata kitu gani kama siyo feki x feki= FEKI, . Ndiyo maana watu kama akina Mchimbi wanamaliza mzumbe baadaya ya mwaka mmoja they claim to be called Dr. ??????? from advanced diploma to PhD holder in 1year !!! How comes, ??? Degree is not just a matter of clicking on the internet on pages GET YOUR DEGREE right NOw. Then u claim to be degree man/women.

Hatutafika kwa mtindo huu. Nilitegemea Prof. Msola angeanza nalo hili but still is too queit, Why, I dont know!! May be some of you knows. Lakini we need to fight for this, other wise our degree will be disregarded international wise in very short time to come.
 
Matatizo ya sekta ya elimu hayapaswi kutazamwa mahali fulani peke yake, mfumo mzima umeharibika kabisa ni kama vile watu wameacha kufikiri na pia sasa ni vipofu, na pia hawajali kabisa kwani watoto wao hawaguswi kabisa na tatizo lililopo kuanzia Shule ya awali hadi Chuo Kikuu , na mbaya kuliko wazazi wameingia kwenye dhambi ya wizi wa si fedha tu makazini kwao bali sasa wanashirikiana na watoto wao kuiba hata mitihani.

Mwisho wa siku ( na hapa sina haja kusema kwa nguvu sana) wanaopata nafasi za kuendelea na masomo ya juu na kupata kazi nzuri( zinazolipa vizuri) ni wao waliotengeneza namna ya mtandao ambao kwao si dhambi bali kwetu sisi ambao hatufaidiki nao.

Ukifanya sensa ya haraka haraka WAKUBWA karibu wote, nashangaa Ridhwan kasoma Tanzania mpaka kupata shahada yake, watoto wao wote wamesoma nje ya Tanzania na wakirudi ndiyo wanaopata kazi kwenye taasisi zenye uwekezaji wa nje kama vile Celtel, Vodacom, Barclays, Tanzania Breweries, Citi bank, CRDB, na mashirika ya Umoja wa Mataifa.


Ukitaka kupambana na hali hii jambo napendekeza mambo yafuatayo:
1. Mchakato wa kumpata Rais wa nchi ubadilishwe.
2. Isiwe lazima kugombea uongozi wowote kwa tiketi ya chama fulani.
3. Si vema sana Mawaziri kuwa au kutokana na Wabunge.
4. Mgawanyo wa Madaraka ya nchi uheshimiwe yaani kati ya Ikulu, Mahakama na Bunge.
5.Rais aache kufanya uteuzi peke yake wa viongozi nyeti wa nchi kama vile IGP, CDF, CNS, Chief Justice, CAG, AG, Accountant General, Makatibu Wakuu wa Wizara wote na wengine ambao sijawataja hapa, wote hawa wachekechwe na chombo maalum , kisha na Bunge na inapotokea utovu wa maadili wajibu tuhuma zao mbele ya Bunge.
 
Naomba kuuliza hivi Benki Kuu na hasa Idara ya Usimamizi wa Mabenki- Bank Supervision kama wanafanya kazi yao kwa umakini wa kweli ama nao ( pamoja na mishahara minono na marupurupu) yote wameamua kula mezani kwao, mabenki ya kigeni yanawanyonya sana wafanyakazi wazalendo na mbaya kuliko miongoni mwa hao wafanyakazi wa kigeni ambao wanalipwa mishahara minono wamekuja kujifunzia kazi hapa Tanzania. Wanasikitisha sana na miongoni mwao jamaa hawa tumesoma nao hata tukiwauliza wanajing'ata tu ulimi hawana hoja ni kama vile hawakwenda shule!!
 
Wakati wote wa Utekelezaji wa Mkataba wa IPTL - JK alikuwa pale Wizarani yaani Nishati, wakati huo Patrick Rutabanzibwa wala hakuwa Katibu Mkuu bali Afisa Mwandamizi, kwa bahati njema wote wapo mbona hawazungumzi kwa uwazi kulikuwa na makosa gani kwenye mkataba ule na NCHI ilijilinda vipi. Kwanini leo Waziri Mkuu anakuwa kama Waziri wa Nishati na Madini, hivi Nizar Karamagi anajionaje , anatamani bila shaka kurudi kwenye biashara yake ya Stock Broker eeh.
 
Wizara ya Fedha mnasubiri tasnifu ipi ili Chuo Cha Usimamizi wa Fedha kuw Chuo Kikuu ? je ni suala la hoja au hoji mbona IDM, Nyegezi na Chuo Cha Ushirika wamevuka hatua hiyo haraka sana. Leo Kuna vyuo Vikuu ambavyo ukivilinganisha na IFM kama umri wa chuo ni hoja basi hata visingestahili kuwa vyuo vikuu, pale IMTU kwa maana halisi hapafai kuwa chuo kikuu cha tiba wakati hawana hospitali, Aga Khan wamevuka hatua hii kirahisi mno.

Kujivuta kwenu hakuna mustakabili mwema kwa nchi yetu.
 
Hivi Mheshimiwa Andrew Chenge, huyo CEO wa Tanroads aliyemaliza muda wake ametimiza malengo aliyopewa alipoomba kazi? Usianze visingizio kuwa wewe wakati huo hukuwepo, maana ndiyo cheap excuses mnazotoa wanasiasa. Ukishindwa kujibu swali hili rudi Bariadi ukalime kwani si umepata Ubunge na Uwaziri baada ya kustaafu serikalini. Ukikaa Bariadi mwaka mzima ndiyo utatia akili juu ya shida ya Usafiri unavyowafanya watu kupanda lori na ng'ombe kuwa sawa na kusafiri daraja la kwanza kwenye ndege ya masafa marefu.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya unatia aibu kuwa ulikuwa hujui kuwa kulikuwa na malengo ya upimaji viwanja kwa fedha toka serikali kuu, hii ni aibu kwako na viongozi wote wa mkoa wa Mbeya . Kwa taarifa yako Halmashauri ya Jiji la Mbeya ni ya pili nyuma ya Kinondoni kwa utapeli wa viwanja Tanzania. Watu Idara ya Ardhi hapo wamekubuhu kuliko kawaida, najua wewe ni mwenyeji wa mkoa huo hvyo kwa namna moja au nyingine na kwa nafasi uliyonayo toka hapo nyuma ulishakwenda hapo Ardhi-Jiji, niambie ukiwa umeshika Biblia mkononi ulishughulika wewe mwenyewe kama ndiyo ulipambana na hali gani?
Acha uzembe, timiza wajibu wako wananchi wala hawataki kwamba lazima wewe uwe Mkuu wa Mkoa, kama huwezi kaa pembeni. Hivi naona kwanza kama huna mchango kwenye maendeleo ya mkoa, upo upo tu, unapelekeshwa kama tela la gari kubwa. Fanya kazi , mshahara wako unatokana na kodi yetu!!
 
Mimi sitaki kuwa upande wowote, nafahamu MU imepewa hadhi ya kuwa Chuo Kikuu, pengine ni muhimu kufahamu timu iliyokaa na kupendekeza na chombo kilichoridhia juu ya hatua hiyo. Kwa upande wa wanataaluma wa MU, nilipata habari kuwa hata HEAC walikuwa na mashaka na baadhi yao na kwa bahati mbaya udhaifu wa uhakiki wa mashaka haya umekuwa mgumu kwani Kiongozi wa Juu wa Taasisi anaguswa na shida hii! Ni kama kashfa si tu kwa MU bali hata kwa Wizara ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia.
Imekuwa kama msemo maarufu usemao funika kombe mwanaharamu apite.
 
Sasa naona HEAC/TCU wanataka kutuletea kiini macho kuwa suala la bogus degrees ni rampant kwenye private universities only, Mzumbe na vyuo vingine vya serikali wanafanya kama mambo poa!

Siri ya wahadhiri wasiofaa yafichuka
Rehema Isango
HabariLeo; Monday,January 01, 2007 @00:05

KUAJIRIWA kwa wahadhiri katika baadhi ya vyuo vikuu bila kuhusisha Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ni moja ya sababu za kuwa na wahadhiri wasio na sifa za kufundisha vyuoni. Pia upungufu wa wahadhiri nchini, umesababisha baadhi ya vyuo vikuu binafsi kuajiri wahadhiri wa kigeni bila kufuata taratibu zilizopo.

Katibu Mtendaji wa TCU, William Sabaya aliiambia HabariLeo hivi karibuni kuwa kama Tume yake ingekuwa inashirikishwa, basi kusingekuwa na matatizo hayo. "TCU imeshuhudia tatizo hilo kwa baadhi ya vyuo binafsi vilivyoanzishwa kwa kuwa vilikosa wahadhiri wa kutosha na wenye sifa kutoka nchini , hivyo kuingia gharama ya kuajiri wahadhiri na waendeshaji kutoka nje ya nchi" alisema Sabaya.

Sabaya alifafanua kuwa ,hatua ya kuajiri wahadhiri hao ilifanyika kwa kuzingatia taratibu zilizopo za Serikali, lakini vilishindwa kuihusisha TCU ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kuhakiki ubora wa elimu ya juu na vyuo vikuu nchini.

Sabaya alisema kuwa ,baada ya kubainika kwa tatizo hilo, hivi sasa TCU inashirikishwa katika shughuli za kutathimini sifa za wahadhiri kutoka nje ya nchi wanaoomba vibali vya kufundisha katika vyuo vikuu nchini.

TCU imetaja sababu za wahadhiri wasio na sifa na uwezo wanaodaiwa kuwepo katika vyuo vikuu vya binafsi kuwa hali hiyo inatokana na upungufu wa wataalamu wenye sifa za kufundisha masomo ya vyuo vikuu katika soko huria.

Hivyo kusababisha kutegemea wahadhiri wachache wanaopatikana katika vyuo vya umma, kwa mpango wa ajira ya muda mfupi au kuajiri wataalamu wasio na sifa za kufundisha masomo ya vyuo vikuu.

Sababu nyingine ni uwezo mdogo wa wenye vyuo binafsi katika kupunguza gharama za uendeshaji, kwa kushindwa kulipa mishahara na marupurupu ya kuwavutia wahadhiri wenye taaluma na uzoefu kutoka ndani na nje ya nchi.

Sabaya alisema kuwa ,baadhi ya wamiliki wa vyuo katika kulinda mambo yao kadhaa kama vile imani, maadili na pengine siri za biashara na mwelekeo mzima wa chuo, kumekuwa na hali ya kutokuwa huru kuajiri wahadhiri na wafanyakazi ambao wanaweza kuwa tishio kwa mambo ambayo mmiliki ana wasiwasi nayo.

Sababu nyingine imetajwa kuwa ni kukosekana kwa uzoefu wa kuendesha vyuo vikuu kwa baadhi ya wamiliki, hivyo kushindwa kutafsiri vema katiba ya Jamhuri ya Muungano, sheria na kanuni za miongozo ya TCU hususan zile zinazoelekeza taratibu za kuajiri na udahili wa wanafunzi.

Alivitaja vyuo vilivyowahi kukabiliwa na upungufu huo kuwa ni Chuo Kishiriki cha Zanzibar, Chuo Kikuu cha Bukoba ambacho kimesitishwa toka mwaka 2000 na Chuo cha Kimataifa cha Teknolojia ya Udaktari (IMTU).

Sabaya alifafanua kuwa, TCU ilibaini kuwa IMTU ilikuwa na wahadhiri wasio na sifa za kufundisha baadhi ya masomo tangu mwaka 2003, na ilikiagiza kusitisha udahili wa wanafunzi katika kozi hizo kwa muda wa miaka miwili ili kupata muda wa kujiandaa kutafuta wahadhiri aliotakiwa.

Hata hivyo, HabariLeo imeshuhudia kuwepo na wahadhiri kadhaa katika vyuo binafsi ambao hawana sifa za kufundisha katika Chuo Kikuu maarufu kilichopo mkoani Iringa(Jina tunalo) na wengine wanaofundisha katika Taasisi ya uandishi wa habari na masuala ya biashara ya jijini Dar es Salaam.
http://www.dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=179
 
Asalam aleyikhum ndugu wana JF.
Mimi ni mgeni wa kuchangia japo nimekuwa nafuatilia kwa karibu michango yote na hakika JF ni tumaini jipya kwa nchi yetu hasa katika zama hizi ambapo "muhimili wa nne" wa serikali kwa kiasi kikubwa umehodhiwa na wanasiasa wachoyo kwa manufaa yao binafsi.Kwa hiyo ndugu wana-JF tuendelee kupiga kelele na ni dhahiri siyo kelele za chura; la impact ya hizi kelele inaonekana wazi.

Baada ya utangulizi huo mororo, napenda kumwuliza ndugu moderator ni wapi alikotupa thread ya Fake degrees aliyoianzisha ndugu Mtz hivi karibuni. Kama ameiunganisha na ile ya "Baadhi ya lecturers wa mzumbe..." basi michango mingi sana haionekani. Na thread hii ilikuwa inatia matumaini sana katika kupambana na hii saratani inayonyemelea mfumo wetu wa elimu.

Elimu makini yenye kutafsiri nadharia katika vitendo ndio msingi wa maendeleo.Na hilo haliwezi kufikiwa kwa kuchonga vyeti online!! Hivo ni lazima tuanze kusafisha mfumo na mwelekeo wa elimu yetu tukianzia na hii saratani ya "vyeti vya kuchonga". Ndugu moderator turudishie thread yetu tujimwage...

N.B Changamoto kwa JF: Pamoja na mapungufu ya bwana Es katika uchangiaji wake, kuondoka kwake kunaweza kufanya hiki kijiwe kudorora kiasi.Hapa sina maana kuwa hii forum ni one man forum; la hasha ila jamaa alikuwa "anakeep forum busy" kwa insider's info na hivo alikuwa anaamsha ari ya kusaka habari zaidi. That said notwithstanding, JF ni chombo muhimu sana katika kuhakikisha checks and balances na Bravo to all JF community
 
Shukrani kwa kuonesha kuwa huwa unafatilia kila linaloandikwa hapa JF, ila nafurahi zaidi kuwa kutoonekana kwa thread ile kumekufanya ujisajili ili kuweza kuhoji iliko.

Ni kwamba hii thread ni ya ki-elimu hivyo niliihamishia kwenye elimu. Hata hivyo na hii uloanzisha naiunganisha pamoja nayo ili kuleta maana sawa.

Karibu na usisite kutoa katika kuhakikisha pengo la ES halipo. Siamini kama ES anaondoka moja kwa moja ila tutakuwa nae vipandevipande.

United we can!
 
Hapa naona wasomi mlivyopoteza mwelekeo baada ya kuingiza ukabila, inaonyesha wazi bwana NUNGWI ulivyo na chuki na wahaya kama Nyarere. Hakuna njia aliyekutangulia kaenda!!1

Kwa sasa UDSM Chancellor ni Kazaura, VC in Mkandara nenda National University of RWANDA VC ni Prof. Rwakabamba Unamkumbuka?? Kwa ufupi wanatoka kijiji kimoja, upo? Bado Uhaya umetumika? Mtatawaliwa tu. Hata huyo Dr. Kamala atakutawala na PhD yake ya PWU.
 
mhhhh.... hili suala la degree feki ni global issue na MU is just a mere instance of that issue. Nadhani hili suala litazamwe kitaifa na wala si kuliharalisha kwenye siasa, kampeni..... ohhh bra bra...... Kenge ni kenge tu huwezi kumbadilisha Ngozi kumwita Mjusi ili aikidhi hadhi yako.. Sidhani kama UDSM inaweza kutumika kama SI unit ya academic excellency...PHDs.....
 
Matata22,

Inashangaza kuona watu kama Nungwi anatetea uozo!

FD
 
Assalam aleikum ndugu zangu watanganyika. Kwa kweli nimeguswa sana na hili suala la degree feki. Cha kushangaza ni kwamba kuwa watu wanaoshabikia mambo bila kutathmini athari zake za muda mrefu..Nawaomba wahusika walitupie macho suala hili.
 
Hivi ni degree gani iliyobora na ipi iliyo feki?
je tunaweza kuzitambua kwa kumsikiliza mtu wmenye degree fulani anayedhani degree yake ni bora kuliko aina yingine?

mimi nafikiri siku zote ubora wa elimu ya mtu hauonekani kwa kuangalia kasomea wapi bali kwa matunda yake. mtu anajisifia degree yangu ni nzuri, nimesomea sehemu fulani lakini nini alichofanya hakuna.

Siku zote mtu anayejisifia kwa kusema mimi ni bora kwa sababu nimepitia sehemu fulani na fulani si bora kwa sababu kapitia sehemu fulani huwa ni dalili ya mtu kukosa ubora mwenyewe na hivyo anataka kujifanya ana ubora. Kama una ubora hatuhitaji kujua umepitia wapi bali tuone matunda ya ubora wako na tukubali.

Ubora wa elimu unapimwa kwa kuangalia elimu hiyo inaboreshaje maisha ya walengwa. sasa mimi nadhani ni kukosa fikra kwa mtu kusema elimu ya Marekani sio bora. Tuangalie wamarekani wenye elimu hiyo wako wapi leo hii. Elimu si sayansi ya kwenye daftari tu bali na aplication yake.

katika jamii kunapokuwa na wasomi wachache, wale walio soma huwa wanakuwa na heshima kubwa kwenye jamii hiyo. lakini kama karibia kila mtu kasoma hakuna wakumuona mwenzake wa maana kwa elimu yake.
Kwa Tanzania tumetoka katika zama za wasomi wachache ambapo hao waliosoma wamekuwa wakiheshimika kwenye jamii. hao walio soma wamekuwa wakitafuta kila njia kupunguza kasi ya wasomi wakihofia kupoteza heshima yao kwenye jamii. Nenda chuo kikuu cha Dar mtu anasoma masters miaka kumi wakati mda wa masters ni miaka miwili lengo ni yule ambaye anamfundisha kuchelewesha watu kama yeye kuwa wengi zaidi.

Soko la products za watu wanaotoka vyuo vikuu ndilo linaweza kuchambua nani kafundishwa na mwalimu mwenye sifa na nani kadanganywa, cha msing tuweke ushindani wa ubora kwenye soko la ajira na kuweke mazingira ya watu wanaojiunga na vyuo kuwa na uhur wa kuchagua vyuo huku vyuo vianze kujiendesha vyenyewe. kama watashindwa kutoa elimu bora ya ushindani sokoni wakose market, lakini sio kwa watu wa chuo fulani kujigamba wao ni bora zaidi kuliko wengine.
 
Julian,

Je unajaribu kutueleza nini? je ni sawa mtu ambaye anafundisha kwenye chuo kikuu ambacho ni kitovu cha elimu kuwa na digrii kutoka chuo kisichotambuliwa? wengi wa walimu wa Mzumbe wana degree nzuri za pili, nina maana kutoka kwenye accredited universities, kwa nini wasiendelee kutumia degree zao genuine? kwa nini wahangaike na digrii "feki" na kujiharibia cv zao? For instance I do not doubt capability of Prof. Warioba and I think he is doing a great job, why jump into this bandwagon of unaccredited degrees, what message is he sending to the mass. I know there could be a pressure from MU regulation to have a PhD, why not change those regulations. In some universities it is not necessary to have a PhD in the university, such a person will be given a title of teaching fellow, and these guys are great, and in some instance they perfom better than PhD holders. To me its better to have a Professor with MSc rather than the same with a bogus PhD.

So ndugu Julian, lets follow rules of the game tusitetee udhaifu, a degree from unaccredited university haina nafasi kwenye vyuo vyetu.
 
mTz
Your point may be right
but my point as well is that kwenye nchi yetu bado tunahukumu ubora wa vitu kwa perception bila kuangalia ni vigezo gani vnatakiwa.

Unajua wengi wa watu wanaotuongoza nchi hii walisoma enzi hizo, ambapo mtu alijiplaud kwa kusema mimi nasomea sehemu fulani na kutokana na siasa zetu za enzi hizo zilitupatia nafasi za masomo kwenye common wealth tukajikuta tukidhani only universities in commonealth are wealth education wise.

and as you know kwamba craetivity (ubunifu) ya mwanadamu hukua anapokuwa mdogo kuelekea ujana na ukomaa na anapozeeka huwa hawezi kuwa mbunifu tena bali huanza kutumia uzoefu.

kwa sasa mambo yamebadilika, lakini wazee hawa bado wanataka kuturudisha enzi zao. sio kosa loa sababu ndio experience walio nayo ndio maana utasikia eti mtu anakataliwa sio kwa kujaribiwa akaonekana hafai bali amechukua degree nchi ambayo wanaotoa maamuzi wanafikiri haifai. Utakuwa leo hii watu wajeariwa mwenye degree ya Uingereza analipwa mshahara mkubwa mwenye degree ya tznzania mshahara mdogo hata kama mwenye degree ya ki Tz anachapa kazi na anaijua lakini yule mwingine ubabaishaji tu.

Ni wakati sasa vijana kubaili mitizamo hii iliyopitwa na wakati. kwamba uwezo wako wa kufanya kazi ndio kiwe kipimo chako.

Leo hii unakuta wasomi wa degree kutoka chuo kikuu wanapinga kuwepo UCC (university computing center) pale mlimani kisa eti hadhi ya chuo kikuu inashuka maana mtu alikua anajisikia mitaani akisema nimesoma University of Dar sasa akiona mtu ana Certificate in Computer na anasema amesoma UDSM anaona hadhi yake imeshuka. Ni wakati watu hawa watambue kuwa thamani yao sio kwa sababu wamesoma UDSM bali thamani ni kile walichonacho kichwani na UDSM wamepata sehemu ndogo tu ya kile kinachowafanya wawe na thamani au wasiwe nayo.

HOJA YANGU NI KWAMBA UKIWA NA DEGREE HATUHITAJI KUJUA NI YA CHUO GANI ILI TUONA KAMA UNAFAA BALI TUTATAKA KUJUA KAMA UNAJUA YALE AMBAYO MWENYE HIYO DEGREE ANATAKIWA KUJUA
that your degree is neither a certificate you were awarded nor your attendance at your university but a knowledge you got in your head.
 
Kwani ni ipi dhana ya shahada feki? Mbona hizo zipo kila sehemu! Ntatolea mifano miwili ya vyuo ambavyo mimi navifahamu. Kwanza ni Taasisi ya usimamizi wa Fedha(IFM),kwa wingi wa wanafunzi walionao IFM imeshindwa kudhibiti wizi wa mitihani na badala yake Taasisi imeamua kuwaongezea wanafunzi alama 5 kila somo kama fidia ya usumbufu! je wahitimu wa hapo kwa nini wasiwe feki?Kama baadhi yao wataajiriwa kama "tutorial asistants" kwa nini wasiwe feki?
Vivyo hivyo kwa chuo kikuu cha Dar es Salaam,wanafunzi wengi,miundombinu haikidhi mahitaji, kwa nini wanafunzi wasaiibie pale wanapofanya mtihani watu mia saba(700) kwenye chumba chenye uwezo wa kuchukua watu mia nne hamsini(450)?Na hali wanataka kufaulu? je hawa wakiajiriwa kama wahadhiri kwa nini wasiwe feki?
 
Back
Top Bottom