wa stendi
JF-Expert Member
- Jul 7, 2016
- 25,190
- 27,434
Yaani wanapaki pembeni na barabara au karibu na kituo cha daladala wakipata abiria mnaelewana vizuri tuu na anakupeleka lakini akifika sehemu iliopo bar anasimama anatoa simu yake kujifanya anampigia mtu halafu anairudisha mfukoni kisha anakuambia "naomba simu yako nimcheki jamaa"hapo anataja jina la mhudumu mojawapo wa hiyo bar.
Ukimpa simu anapiga halafu anashuka kwenye boda yake anazima kabisa na ufunguo anachomoa halafu anaenda na simu yako mle ndani bar yeye anakuacha na boda yake sasa hapo ukijichanganya umfuate mle ndani yeye kumbe ameshakusoma unaingiaje yeye anatoka fasta anaenda washa pikipiki yake anapotea na simu yako wewe unabaki unaulizia lile jina alilotamka.
Nimeoana niwaambie maana jamaa yangu juzi tuu leo siku ya 3 simu yake imeondoka kwa style hiyo .
Ukipanda pikipiki jitahidi upande kwa unayemjua au kama yuko kijiweni kwake hakikisha kavaa reflector ile yenye namba ya kijiwe hata ikitokea tatizo inakuwa rahisi kulitatua.
Jumapili ikiwe njema kwenu.