Baadhi ya madereva pikipiki (bodaboda) ni wezi, chukua tahadhari

Baadhi ya madereva pikipiki (bodaboda) ni wezi, chukua tahadhari

Kuna watu wazembe kupita kiasi. Unakodi bodaboda, anafika katikati ya safari anasimama, na wewe unaona sawa, anapiga simu na wewe unaona sawa, anaomba simu na wewe unaona sawa, anaondoka na simu na wewe unaona sawa! Jamani huu ni zaidi ya upunguani. Navyojua ukikodi gari au boda, mwendeshaji anatakiwa akupeleke moja kwa moja bila kuingiza mambo yake ya binafsi, hata kutumia simu haitakiwi. Mteja una haki na wajibu wa kumuonya iwapo unaona anafanya mambo mengine ya binafsi!
Tatizo watu wanachukulia "hutu si mwana?hana shada huyu na vile akiachiwa boda nje ndio kabisaa anaona haina shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi katika mambo ambayo huwa nayapinga na kusema ni ujinga ni hili la kusema wanatumia dawa kupumbaza! Hakuna dawa ya kupumbaza. Matapeli siku zote hucheza na ubongo wako na kukufanya uamini kwa muda kile wanachokuambia ni kweli japo baadae ukija kutafakari utajiona ulikuwa mjinga kupita maelezo. Unachotwa kiakili tu na hakuna la zaidi.
Kabisa mkuu maana jamaa anasema wala hakuwa na mawazo kama jamaa anaweza fanya kama alivyofanyiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli huu ni uzembe wa hali ya juu. Simu ni article personal. Kukupa simu labda uwe mama yangu. Yaani mtu baki tu nikupe simu yangu. Simu siku hizi ni benki pia. Utampaje mtu baki tu kifaa chenye taarifa zako za benki?
Jamaa hakujua kinachotokea maana aliachiwa boda kwanza na alipoona suka hamwoni akashuka kwenye boda eti anamfuata jamaa alieingia na cm yake kule bar basi boda katoka kawasha boda safarii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakujua kilichotokea? Kweli? Kwa hiyo alitoa simu akiwa nusu kaputi? Elewa ninachokisema. Hakutakiwa kutoa simu kwanza. Achana na mambo ya kuingia bar.
Jamaa hakujua kinachotokea maana aliachiwa boda kwanza na alipoona suka hamwoni akashuka kwenye boda eti anamfuata jamaa alieingia na cm yake kule bar basi boda katoka kawasha boda safarii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani wanapaki pembeni na barabara au karibu na kituo cha daladala wakipata abiria mnaelewana vizuri tuu na anakupeleka lakini akifika sehemu iliopo bar anasimama anatoa simu yake kujifanya anampigia mtu halafu anairudisha mfukoni kisha anakuambia "naomba simu yako nimcheki jamaa"hapo anataja jina la mhudumu mojawapo wa hiyo bar.

Ukimpa simu anapiga halafu anashuka kwenye boda yake anazima kabisa na ufunguo anachomoa halafu anaenda na simu yako mle ndani bar yeye anakuacha na boda yake sasa hapo ukijichanganya umfuate mle ndani yeye kumbe ameshakusoma unaingiaje yeye anatoka fasta anaenda washa pikipiki yake anapotea na simu yako wewe unabaki unaulizia lile jina alilotamka.

Nimeoana niwaambie maana jamaa yangu juzi tuu leo siku ya 3 simu yake imeondoka kwa style hiyo .

Ukipanda pikipiki jitahidi upande kwa unayemjua au kama yuko kijiweni kwake hakikisha kavaa reflector ile yenye namba ya kijiwe hata ikitokea tatizo inakuwa rahisi kulitatua.

Jumapili ikiwe njema kwenu.
Huo ni ujinga, mleta hoja na jamaa yako ni wazembe. Unampaje mtu simu yako? Japo nakubaliana nawe juu ya bodaboda kutokuwa waaminifu, si baadhi, wengi wao.
 
Huo ni ujinga, mleta hoja na jamaa yako ni wazembe. Unampaje mtu simu yako? Japo nakubaliana nawe juu ya bodaboda kutokuwa waaminifu, si baadhi, wengi wao.
Mi hapo nahusikaje .
Mi nimeleta hoja kisa cha rafiki yangu alichofanyiwa.unaniita mzembe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom