Baadhi ya madereva pikipiki (bodaboda) ni wezi, chukua tahadhari

Baadhi ya madereva pikipiki (bodaboda) ni wezi, chukua tahadhari

Bajaji na tax bubu za usiku ni za kuchukua tahadhari pia...unaeza kuta wote watatu wanajuana na wanazuga kama wamekutana kituoni kama abiria....

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
huo wizi wa ki hivyo uko tabata tabata huko yaani ukikodi boda dereva anakupeleka alafu akifika njiani anaenda kusimama sehemu waliko boda wengine (kumbe wote ni wamoja ni kituo hewa)wanakukaba wote kila kitu kinachukukiwa na wao wote wanatambaa na boda zao.
Na sio hivyo tuu waanaa boda pembeni ya barabara alafu anatoka jama mmoja (mmoja wao)anenda mbalii huko anakodi boda mnaelewana vizuri tuu unapanda ukifika pale waliko boda kituoni anakuambia "niache hapa waliko boda wenzako"sasa ile dereva anasimama tuu wale wale pale wanamrukia wanapiga u asukumiziwa mtaroni au chaka pikipiki yako ina chukuliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Why umpe mtu simu yako dah hapo ndipo tunatofautiana,labda wapore ila kumpa mtu simu hapana kwa kweli
 
Yaani wanapaki pembeni na barabara au karibu na kituo cha daladala wakipata abiria mnaelewana vizuri tuu na anakupeleka lakini akifika sehemu iliopo bar anasimama anatoa simu yake kujifanya anampigia mtu halafu anairudisha mfukoni kisha anakuambia "naomba simu yako nimcheki jamaa"hapo anataja jina la mhudumu mojawapo wa hiyo bar.

Ukimpa simu anapiga halafu anashuka kwenye boda yake anazima kabisa na ufunguo anachomoa halafu anaenda na simu yako mle ndani bar yeye anakuacha na boda yake sasa hapo ukijichanganya umfuate mle ndani yeye kumbe ameshakusoma unaingiaje yeye anatoka fasta anaenda washa pikipiki yake anapotea na simu yako wewe unabaki unaulizia lile jina alilotamka.

Nimeoana niwaambie maana jamaa yangu juzi tuu leo siku ya 3 simu yake imeondoka kwa style hiyo .

Ukipanda pikipiki jitahidi upande kwa unayemjua au kama yuko kijiweni kwake hakikisha kavaa reflector ile yenye namba ya kijiwe hata ikitokea tatizo inakuwa rahisi kulitatua.

Jumapili ikiwe njema kwenu.
Yalisha kukuta?
 
Kama sikufahamu na hatuna mazoea sikujui kwa lolote unaanzaje kushika simu yangu kwa mfano?!

Sio tu simu mimi mwenyewe huwezi nigusa nitakulamba kofi. Unaanzaje kuomba simu za watu upige upuuzi huo.

Niliwahi kukutana na mdada kwenye basi ya mkoa akanambia anaomba kupiga simu kuwacheki ndugu zake huko anakokwenda. Hapo ni ile tunakaribia kushuka sehemu ya msosi ule muda mnajiandaa kushuka kwenye basi ili mkapate chakula kwenye hoteli.

Nikamwambia maliza shighuli zako kwanza tukirudi kwenye basi ndio utawapigia.

Yaani alitaka nimuachie simu kwa kigezo kuwa tupo siti majirani. Yaani ni zile basi za siti za mkao wa 2 by 2. Yeye alikaa upande wa korido abiria mwingine alikaa ya dirishani. Na kwa upande wangu mimi nilikuwa upande wa dirishani halafu kuna mshikaji alikuwa pembeni yangu upande wa korido.

Tumefika kauchuna ile ya kusubiria watu waliosimama washuke mimi nimetulia nashangaa mtu ananiongelesha.

Nikaona hapa huyu changamoto. Inaweza shangaa maongezi marefu au akakutoka hapo bila kujua......

Tumerudi kapiga kimya nikamwambia vipi umeshaongea nao akasema basi..... nikasema ona sasa. Mtu aliesema anashida ya kupiga simu ghafla kachenji mind baada ya gari kuanza kuondoka.
 
Back
Top Bottom