Baadhi ya Makosa Ambayo Watoto wa Zamani Tulikuwa Tukila Bakora.

Baadhi ya Makosa Ambayo Watoto wa Zamani Tulikuwa Tukila Bakora.

Dr Chi

Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
33
Reaction score
43
1. Usiposalimia wakubwa asubuhi, unapigwa.
2. Usiposalimia wageni, unapigwa.
3. Ukinawa kabla ya wageni, unapigwa.
4. Ukilia bila sababu, unapigwa.
5. Ukinyanyuka wakati wa kula kabla ya wakubwa kuinuka, unapigwa.

6. Wakubwa wakiwa wamekaa wewe ukaenda kusimana pembeni, unapigwa.
7. Ukikaa wakubwa wamesimama, unapigwa.
8. Ukitumwa dukani ukachelewa kurudi, unapigwa.
9. Ukichelewa kurudi toka shuleni, unapigwa.
10. Ukiwahi kurudi shuleni, unapigwa.

11. Ukililia wageni wakati wanaondoka wakitoka, unapigwa.
12. Kujipitisha pitisha wageni wakiwa wanakula, unapigwa.
13. Kujibu ovyo wakubwa, unapigwa.
14. Kutukana watu wazima, watoto au rika lako, unapigwa.
15. Ukiwa mbishi bila sababu, unapigwa.

16. Ukipigwa ukalia unapigwa ili unyamaze.
17. Ukipigwa umenyamaza unapigwa ili ulie.
18. Ukipigwa shuleni ukaenda kusema nyumbani, unapigwa.
19. Ukianza kula nyama kabla ya wakubwa, unapigwa.
20. Ukila kwa jirani ukabainika, unapigwa.

21: Ukianza kunawisha wenyeji badala ya wageni mkimaliza kula unaitwa chumbani, unapigwa.
22. Ukianza kunawisha watoto badala ya wakubwa, unapigwa.
23. Ukimkuta mtu nzima hujampokea, unapigwa.
24. Ukienda kusema kama umepigwa, unapigwa.
25. Mtu mzima akipita kama mnacheza hamjamshughulikia, unapigwa.

26. Ukienda nyumba za watu, ukaona kitu au ukasikia story ukaileta nyumbani, unapigwa.
27. Ukipewa hela na mtu asiefahamika au hata anaejulikana inategemea mazingira gani, unapigwa.
28. Ukianza kuchaguwa chakula hiki nakula hiki sili, unapigwa.
29. Ukianza kuwa na marafiki wasioleweka makwao, unapigwa.
30. Mtu mkubwa akija kukuchongea nyumbani hata kama sio cha ukweli, unapigwa.

31. Ukikaa na wakubwa halafu ukaanza kucheka bila sababu, unapigwa.
32. Ukimuuliza Baba/ Mama umetoka wapi unapigwa.
33. Ukilala bila kula, unapigwa.
34. Ukiitwa ukaja kimyakimya bila ya kuanza kuitika unapigwa.
35. Endapo umepigwa na ukasusa chakula, unapigwa.

Wahenga njooni tukumbushane matukio mengine
 
Baadhi ya mambo hapo yalituandaa tuwe kondoo wa .....
 
😭😭 zile fimbo hapana jamani,ukikimbia babu anakukimbizia mpaka anakukamata.
Tuzee twa sasa ni 🙄
 
Ukijamba wakati wa Kula unapigwa kibao!!!
 
Ukitumwa na ukakataa, unapigwa
Kulala bila kunawa miguu, unapigwa
Ukikataa kuoga, unapigwa
Ukidokoa mboga ukaonekana, unapigwa
Kama umekatazwa kucheza mpira, usicheze, ukicheza unapigwa
 
Ukifanya kosa, kisha ukaitwa "we fulani, njoo nikutume dukani" kaa chonjo, unaenda kupigwa
 
Ilikuwa ni kupigwa kupigwa kupigwa yaan kipigo kilikuwa hakikwepeki sijui kama shibela aliikuta hiyo.
Naijua Sana hiyo,kipigo nisichokisahau ni siku moja niliepua chakula na vipande vya shina la mgomba sufuria ikateleza chakula chote chini 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kama ni kweli maisha yalikuwa hivyo ni kazi kweli kweli
Kiufupi haikuwepo nafasi ya nyie kuwa binadamu

Kwa hiyo kwa sasa tabia zenu zimenyooka na hamkosei kabisaaa
 
Vijana wa sasa wanakiita kizazi cha mbumbumbu...
Lakini mambo mengi yanapaswa kubadilika kulingana na ulimwengu tuliopo...mfano namba 15
Ukiwa hujui utabishiwa tu hata uwe mzee vp
 
Ukitumwa na ukakataa, unapigwa
Kulala bila kunawa miguu, unapigwa
Ukikataa kuoga, unapigwa
Ukidokoa mboga ukaonekana, unapigwa
Kama umekatazwa kucheza mpira, usicheze, ukicheza unapigwa
Ukichelewa kurudi kutoka kucheza baada ya saa 12 jioni unapigwa...
 
Kama ni kweli maisha yalikuwa hivyo ni kazi kweli kweli
Kiufupi haikuwepo nafasi ya nyie kuwa binadamu

Kwa hiyo kwa sasa tabia zenu zimenyooka na hamkosei kabisaaa
Huu ni ukweli halisi,sijui wazazi wetu walikopi wapi hii tabia...
 
Back
Top Bottom