Baadhi ya mama ntilie wanatulisha uchafu

Baadhi ya mama ntilie wanatulisha uchafu

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Hii ni sekta moja wapo inayowapati kina mama wengi sana kipato, lakini tatizo limekuwa kwenye kuboresha mazingira yao ya kazi.

Hii imenitokea zaidi ya mara tatu maeneo tofauti tofauti, nimeagiza msosi kabla bado sijala nikasema ngoja nikague kijiko aiseeeh ni aibu, nimeletewa kijiko kinaonekana kimetoka kutumika muda si mrefu bado kina mabaki ya chakula. Kwa maana hiyo hakijasafishwa vizuri

Maeneo ya kulia chakula hasa mezani, nzi kibao unakula chakula mara nzi kadondokea kwenye chakula inatia kinyaa.

Mama ntilie kama mpo humu naomba mbadilike mnatulisha uchafu, jitahidini kuwa wasafi.
 
Upo sahihi mkuu lkn kama umelijua hilo ni vema ukaanza kupanda bei kwa kuanza kula sehemu zenye ubora(classic) mimi ni muhanga kama wewe na nimejaribu mara kadhaa kuwaambia kasoro ninazoziona lkn majibu yao yamekuwa sio mazuri

Sasa iyo tisa kumi ni pale unapobahatika kuwaona wanapoandaa hivyo vya kula🤭nakuhakikishia huwezi kula kuanzia maandalizi ya viungo mpk ugali
 
Sehemu nyingi za vyakula ukienda jikoni na unakinyaa hutakula hata haya mabaa au vijimighahawa tunaita "hotel" usithubutu kwenda wanapoandalia msosi we rizika na unachokiona mezani.

"Ukimchunguza sana bata hutamla"
 
Hapa kila mtu atasema yeye hali kwa mama ntilie sababu ni wachafu!
JF bwana!
 
🤔🤔🤔 Hatari sana. Ila cha ajabu wanaume wengi wameshaadopt huo uchafu na vijidudu vya magonjwa. Hukuti wakichunguza, Hukuti wakilalamika wala kuwasikia wakiumwaumwa matumbo au kuharisha kila siku 😂
 
Umasikini wako ndio tatizo, ukiwa na hela ya kutosha huwezi kuleta huu upuuzi muda huu hapa jamvini
 
Wenzio walizoea kula hapo wanaona kawaida kikubwa washibe,
Wewe ukitaka mazingira safi basi nenda sehemu za wali nyama elf 7 uone kama utakuja kuandika thread hapa!
Usafi hauna gharama yoyote kuosha kijiko na kitunza vyombo kwa usafi havihusiani na bei ya chakula
 
kumaintain hali ya usafi ni gharama,
msosi wenyewe buku unategemea nini
 
Kuna zile kachumbari zao huwa wanatengeneza kwa kuminya vitunguu na mikono, wakati huo katoka kubadili pedi bila hata kunawa, poleni mnaokula kwa hao watu
Daah wewe jamaa umenifanya nifikirie sana, thou sio mshiriki wa hizo sehemu.
 
Kuna zile kachumbari zao huwa wanatengeneza kwa kuminya vitunguu na mikono, wakati huo katoka kubadili pedi bila hata kunawa, poleni mnaokula kwa hao watu
Kuna siku nilienda kunywa chai,basi chapati zikawa za kusubiri!Hapo chai nilishawekewa mezani,nikaona Namalizia chai chapati hazifiki!Ikabidi ninyenyuke nizifate huko huko jikoni,lahaula si nikamkuta mama anayepika vyapati Yuko anamtawaza mtoto wake aliyejinyea pembeni tu kidogo na anapopikia,yaani kama ni jambo la kawaida!Wala hata hakustuka,akaniambia wewe ndiye uliyetoa oda ya chapati 3,nikamwambia ndio!Akasema ndio anamalizia ya mwisho,hapo ndio anamvali bukta mtoto wake!Nikasubiri Ili nione basi kama atanawa na sabuni!Haikuwa hivyo,yaani pale pale wakati anamtawaza mtoto,alivyosuuza tu mikono ndio akawa amemaliza!
Basi nikamwambia naenda kusubiri,niliondoka Moja Kwa Moja hata cheji sikudai maana nilikuwa nimeshalipia!
Tokea hapo nikaanza kupanga bajeti yangu vizuri walau niweze kula sehemu za kueleweka pale nilipokuwa Sina nafasi ya kupika!
Hapo Ilikuwa 2015 ndio kwanza nimepanga geto na hata mishahara miwili Bado haijafika!
 
Wenzio walizoea kula hapo wanaona kawaida kikubwa washibe,
Wewe ukitaka mazingira safi basi nenda sehemu za wali nyama elf 7 uone kama utakuja kuandika thread hapa!

Wenzio walizoea kula hapo wanaona kawaida kikubwa washibe,
Wewe ukitaka mazingira safi basi nenda sehemu za wali nyama elf 7 uone kama utakuja kuandika thread hapa!
Umasikini wako ndio tatizo, ukiwa na hela ya kutosha huwezi kuleta huu upuuzi muda huu hapa jamvini
Punguza makasiriko kama mkeo ni mama ntilie mwambie azingatie usafi.
 
Back
Top Bottom