Baadhi ya maswali yaliokosa majibu Kwenye Soka


Kwa messi umeongea point big up sana:

Mkuu Hili swali huwa nakosa jibu lake kila napouliza kwa wapenzi wa gaucho na ndio wanaosumbua humu na ni wachache mno hawazidi watano!

Naomba unijibu kitaaram ira usisepe tu mkuu kama wengine.

Kama ni kweri gaucho ni mchezaji wa muda wote
Naomba unipe evidence kama ifuatavyo;
Je yumo katika top 30 ya wachezaji bora? Na kama yumo naomba utuonyeshe sasaiv

Je huyo gaucho ana ubora upi wa kumzidi Zinedine Zizzle? naomba facts,evidence and statistics....Ukienda top 10 ya mabest players utakutana na Zidane, lakini huyo Gaucho humpati!

Naomba uniletee majibu mazuri yalioenda shule
 
Kula rike mukuu twende sawa
Timu ya Taifa ndani ya miaka 4 inagombania vikombe 2 au 3 while Klabu kwa msimu mmoja tu inagombania makombe 4 kwa miaka 4 klabu ina posibility ya kugombania vikombe 20 while timu ya Taifa inagombania vikombe 3
 

Namba 1 huo ni mtazamo wako wewe:
Maradona hakuna wa kumfuata kwanzia soka liripoanza hapa duniani hadi wakati huu wa-messi,messi kafananishwa na maradona rakini sio kwamba kamzidi maradona!

Maradona ndiye “mwanasoka bora wa muda wote” wa Shirikisho la Kandanda la Dunia (FIFA). Alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Karne iliyofanyika kwa uwazi mwaka 1999 na kumtupilia mbali Pelé.



Mchuano huo uliendeshwa na mtandao rasmi wa FIFA, jarida la shirikisho hilo na mfumo wa kisheria. Alikusanya asilimia 53.6 akifuatiwa na Pelé aliyepata asilimia 18.53 tu kati ya kura zote zilizopigwa.

mshambuliaji aliyekuwa na kila ujuzi anaopaswa awe nao mwanasoka mwenye kipaji kilichopitiliza.

Alichukua mpira kutoka umbali wa mita 60 upande wa timu yake, akaanza kuwachambua mabeki mmoja baada ya mwingine hadi wote watano walipokwisha, kisha akahitimisha kwa kipa naye kumlamba chenga na kubaki akiangaliana uso kwa uso na goli lililo wazi.
Mwanasoka huyo wa zamani bado anakumbukwa jinsi alivyokuwa akiuchezea mpira anavyopenda, akapiga chenga anavyotaka yeye mwenyewe, akapenya mahali popote, wakati wowote na kuwadhalilisha mabeki kama alivyowafanyia wa timu ya taifa ya England katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1986.

Fuatilia video mbali mbali za maradona utajionea mwenyewe, angalia alizocheza timu yake ya taifa (Argentain),barcelona,napoli,boca juniors, sevilla na argentinos juniors ujionee mwenyewe, achana na huyo mwehu magoli yake mengi ya offside na hayana mvuto, pia hakucheza ulaya akakutana na matimu makubwa, bali aliendelea kuchezea vitimu vya brazil visivyokuwa na mvuto wowte na isitoshe ligi zenyewe ni nyepesi, hakuna cha defensi wala nini..In-short hakukuwa na sheria ngumu kama ilivyo kipindi cha maradona hadi sasa
 

Huo ni mtazamo wako mkuu....

kama umemsoma vizuri mleta mada, amesema ni maswali yaliyokosa majibu ya moja kwa moja....sasa hayo uliyotoa ni kwa mtazamo wako ukichagizwa zaidi na ushabiki....
 
kuna wengine wanadai Barcelona ya 2009-2011 ilikuwa hatari zaidi kuliko Brazil ya 1970
Wewe ile brazily ya 1970 iache kama ilivyo hapa kila mchezaji alikua kwenye kiwango chake ila pelle alikua star wa ukweli sehemu hii 1970 hapa alichaguliwa kua mchezaji bora wa kombe la dunia mwaka huo huku brazili ilkitwaa ndoo hiyo
 
hakuna wa kumlinganisha na ronaldinho mpaka sasa, unaweza kumlinganisha kwa baadhi tu, mfano ufungaji wa ronaldinho na mchezaji fulani lakini sio kipaji chake, alikua na kipaji cha pekee huyu super

Kwa kigezo kipi? Ninyi mashabiki mandazi huwa mnatusumbua mno kwenye hili jukwaa, Huwa sipendi kumsifia flan without evidence! Naomba uje na facts,evidence and statisticts kama we ni kidume haswaaa, na kama itaonyesha amewapita akina Maradona,Messi,Zidane,Redondo,Pele,cr7,Henry naomba mods wani-ban hii leo. ni hilo tu
 
Pele halinganishwi na yeyote mpaka sasa
Messi amefika robo tu ya uwezo wa pele
 
Tangu nimeanza kuangalia nafurahi Sana kuwa mmoja ya watu walioshuhudia kumuona fundi gaucho katika soka binafsi hakuna Kama gaucho.

Kwa kigezo kipi? Lete ushaidi hapa, kila anaemsifia mchezaji kwa ubora wake pls alete facts na evidence
 
good point, ingawa nina tofautiana na ww kwenye suala pele na diego
 
Pele halinganishwi na yeyote mpaka sasa
Messi amefika robo tu ya uwezo wa pele

Wewe ni shabiki mandazi...niambie diego alipata asilimia ngapi katika uchaguzi uliofanyika 1990, na huyo babu yako anaye muhusudu messi mwenye roho ya korosho kapata asilimia ngapi naomba jibu sitaki majibu ya mdomoni.
 
ww zizzou noma, huyo anayesema gaucho ni bora kuliko zizzou labda hajui vitu muhimu kwenye mpira, yy anapenda madoido, muulize aliangalia world cup france vs brazil, zizzou aliwafanya vibaya kaka na gaucho
 
Ha ha ha haaa Zidane alipiga watu kanzu hiyo cku, alianza na gaucho then ronaldo, in-short aliwadhalilisha brazil
kaka kumbe uliona ,achana na zizzou, we unafikiri Italy wajinga mpaka wakafanya sabotage kumtumia materazi hili zizzou atolewe,
 
Wewe ni shabiki mandazi...niambie diego alipata asilimia ngapi katika uchaguzi uliofanyika 1990, na huyo babu yako anaye muhusudu messi mwenye roho ya korosho kapata asilimia ngapi naomba jibu sitaki majibu ya mdomoni.
We ndio maandazi mi nazungumzia ubora wa uwanjani rekodi bora kuliko wote huyu ni pele tu hakuna nwingine
 
ww zizzou noma, huyo anayesemagaucho ni bora kuliko zizzou labda hajui vitu muhimu kwenye mpira, yy anapenda madoido, muulize aliangalia world cup france vs brazil, zizzou aliwafanya vibaya kaka na gaucho

Hahahaaa mkuu hawa tunawaita (shabiki mandazi wafuata mkia) hapa tanzania kuna tabia moja, huwa wanaangalia majina ya wachezaji na si ubora wa mchezaji. Huyo gaucho kashika nafasi ya 31 katika best players....lakini kuna mijitu isiyojitambua inatuambia eti gaucho ni zaidi ya zidane huwa nashindwa kuwaelewa! Ukiwaomba, facts, evidence and statisticts hawaleti bali wanang'ang'ania tu gaucho weka mbali na watoto.hawa ni wakuwapuuza si washabiki haswaaa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…