Baadhi ya maswali yaliokosa majibu Kwenye Soka

Kwanza tueshimiane sijazaliwa 1994
Pili wewe ni shabiki wa mesi na maradona
Tatu mimi sio mshabiki wa wachezaji kupigiwa kura mimi ni mpenzi wa rekodi zilizomo
So pelle anabaki kua namba 1na vyura wengine wanafuata
 
Kwanza tueshimiane sijazaliwa 1994
Pili wewe ni shabiki wa mesi na maradona
Tatu mimi sio mshabiki wa wachezaji kupigiwa kura mimi ni mpenzi wa rekodi zilizomo
So pelle anabaki kua namba 1na vyura wengine wanafuata

Poa mkuu! Sasa why unakataa Diego si mchezaji bora wa dunia kumzidi pele? Kwani hizo kura alizopata yeye Diego kutoka kwa mashabiki wanaomkubali duniani, na fifa ikamtangaza kutokana na hizo kura alizopata =asilimia 58 je ni za uongo?
 
Ndio maana nikasema rekodi ndio zinamjua alie bora na tukuweka rekodi za kila mmoja hapa pele anabaki kua namba 1
Shabiki kupiga kura sawa na inawezekana hawajamkuta pelle akiwa katika ubora wake
Mwaka 1970 wakati pele akionyesha kiwango cha juu kabisa katika soka hapa alikua na miaka 30
Wakati akiipatia ubingwa wa dunia brazili kwa mara ya tatu
Sikatai maradona ni bora ila pelle ni zaidi ya ubora katika soka la dunia hii
 
Hata kwa kigezo cha magoli Pele goli 1000 maradona ngapi?.
 
1. Gaucho ndo mchezaji bora wa wakati wote (japo hujampambanisha)
7.Gaucho ni bora zaidi ya Zidane
 


Kati ya wachezaji wanao heshimika Brazil ni pamoja na Garrincha, ila ni kwanini dunia ya mpira haimpi heshima hiyo??
 



  1. Diego maradona
  2. King Messi
  3. Cr7 and Berkamps
  4. Maneno machafu
  5. Barcelona
  6. Nothing
  7. Ustazi zinedine hakuwa na mpinzani labda Requelme kwa mbali though hukumweka

Sina swali my friend Mussolin5! Maana mpaka sasa bado sijaona wa kumfikia Messi wala Diego! Thank you
 
eti magic messi.....lol
 
kwangu mimi hapo kwa messi na ronaldo namchukua ronaldo....why...takwimu hazidanganyi ronaldo ni lethal mnoo akiwepo uwanjani anaweza kukupoteza saa yoyote kuhusu kipaji sijui asili.... kwa tunaocheza mpira tunajua kama mpira hujui ni hujui tu....and the guy his age pia inanifanya nimheshimu ....massive . respect from 4-1 to 5-5 . ballon d' ors si haba....
 
kwa zidane, ahhahahaha, hujaangalia enzi zake nini,? Toa discipline, ila mbungi alikuwa nayo. Discipline mbovu haikuanzia kwa materazi, hakuwa na uwezo wa kudhibiti hasira, na aliahibu waziwazi maru za hivo lukuki.
 
Jifunze kutofautisha kati ya Ronaldo na Cristiano Ronaldo

Ukiandika tu Ronaldo basi unamaanisha DE Lima
 
hakuna wa kumlinganisha na ronaldinho mpaka sasa, unaweza kumlinganisha kwa baadhi tu, mfano ufungaji wa ronaldinho na mchezaji fulani lakini sio kipaji chake, alikua na kipaji cha pekee huyu super
ndio baba umemaliza vingine ni kulazimishana
 
wewe shabiki kitumbua wakati wewe unapokea vigezo vilivyowekwa ufahamu pia hao unaojadiliana nao wana vigezo vyao pia.MTOA MADA NI MWENYE AKILI NYINGI ALIPOSEMA MASWALI YALIYOKOSA MAJIBU,kunapokosekana kukubaliana kwa watu katika jambo fulani ndio kukosa majibu kila mtu na mpenzi yake.
 
5. Barcelona ya 2009-2011 ndio bora zaidi kama klabu maana ilibeba vikombe vingi kuliko Brazil ya 1970 kama timu ya taifa
Hahahaha acha utani mkuu Brazil ya mwaka 70 ya kina Tostao, carlos alberto, rivelino, Jairzinho,pele n.k ndio ulinganishe na hao watoto wa juzi

Kwa ufupi goli bora katika historia ya mpira limetokana na timu hiyo ya mwaka 70 kma hujawahi liona basi una haki ya kuwashabikia hao watoto wa juzi

Moja ya goli la ajabu la pasi ya timu nzima bila wazungu kugusa mpira

 
Kwamba pele kakuta offside hakuna?? Mbona husemi alikuta red card hamna?? Mbona husemi alikuta hakuna penalty za baada ya extra time?? Mbona husemi alikuta hamna sub ukivunjwa mguu mnabaki 10 pekee ??

Tuache ushabiki pele hana mfano wake alistaafu hata kabla hajafikisha miaka 30 ila aliweza kubeba world cup 3 na makombe kibao santos huyo maradona kastaafishwa akiwa ameshazidi miaka 34 ila hajafikia hata robo ya mafanikio ya pele ndio umlinganishe naye

Maradona kawaida sana alipokuwa barca alikua mzigo tu nashanga mnamwagia sifa kibao

Kingine kwamba barca ndio timu bora?? Labda nirudie tena kwa kura za FIFA timu bora zaidi katika historia ni Brazil ya mwaka 1970 ikifuatiwa na Timu bora zaidi ambayo haikuwahi kubeba world cup yaani brazil ya 1982 yenye socrates na zico sasa cjui mnapowapaisha hao watoto wajuzi mnatoa wapi takwimu zenu.....

Hao barca walicheza mpira mzuri ila bado hawajafikia vigezo vya Brazil ya enzi hizo unamlinganishaje beki kisiki carlos alberto na carles puyol au gerald pique?? Unamlinganishaje iniesta na gerson
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…