Mchezo wa soka ni moja kati ya michezo yenye mvuto na msisimko mkubwa, lakini pia ni mchezo wenye matukio mengi mazuri, mabaya na hata ya kuhuzunisha.
Yafuatayo ni baadhi ya maswali ambayo kwa namna fulani yamekosa majibu ya moja kwa moja.
1. Pele na Maradona ni nani Mchezaji bora wa wakati wote
2. Ronaldo na Messi ni yupi Mchezaji bora kuliko mwenzake?
3. Kati ya Ronaldo, Thiery Henry na Denis Bergkamp yupi ni mchezaji bora zaidi wa kigeni kucheza EPL?
4.Nini chanzo cha ugomvi baina ya Zidane na Marco Materazzi katika fainali ya world cup 2006?
5. Barcelona ya 2009-2011 na Brazil ya 1970 iliyochukua ubingwa wa dunia, ipi ni timu bora zaidi katika historia ya soka?
6.Kombinesheni ya Frank Lampard na Steven Gerrard katika timu ya taifa ya England imewahi kuwa na mafanikio?
7.Nani alikuwa fundi zaidi kati ya Zidane na Gaucho?
Weka na wewe Maswali yako unayohisi hayajawahi kuwa na majibu halisi.
Yamekosa majibu au huna weye majibu?
1. Technical maradona alikua zaidi ya pele.
2. Kumfananisha messi na ronaldo, ni kudhalilisha mchezo wa mpira. Messi ni classy kwa kila idara.
3. Hivi kwanza ronaldo aliingiaje kwenye list ya all time uchezaje bora wa kigeni EPL? anakipi kikubwa alichofanya pale? Unafaham nini Henry, Zola,Pires, Beckamp, Silva, Cantona wamefanya ndani Epl?
4. Hilo kweli ni pekee kati ya hayo lililokosa majibu.
5. Brazil ya 1970 ilikua ni something else. (Plus pia jaribu kutafuta Brazil ya 1982 mkuu.)
6. Hivi weye uliyaona hayo mafanikio kwani?
7. Zidan alikuwa better player than Ronaldinho ilo halina ubishi.