BlackPanther
JF-Expert Member
- Nov 25, 2015
- 9,185
- 8,715
Majibu ni kama ifuatavyo kutokana na maswali yako, hii ni kwa mujibu wangu mimi mdau wa soka:
1. Swali la kwanza naweza kusema Maradona kwa sababu zifuatazo: Pele alicheza soka na kuwika sana miaka ya 50 mpaka 60 mwishoni. Kutokana na mbwembwe zake za kipindi kile alionekana ni mchezaji bora duniani kwa sababu alikuwa anacheza na wapinzani ambao walikuwa more pedestrian than himself na mpira wa kipindi kile ulikuwa hauna utaalam zaidi ya kufuata formation na kila mchezaji alimkaba mtu wake.
2. Swali la pili nafikiri Messi ni zaidi kwa sababu ni mchezaji anayecheza kitimu zaidi kuliko CR7 anayejali zaidi rekodi binafsi na hachezi kitimu.
3. Kwa swali la 3 naweza kusema CR7 kwa sababu alileta changamoto zaidi kwa timu pinzani japo wote uliowataja walikuwa hatari.
4. Ugomvi wa hawa jamaa ulitokana na Materazzi kutukana dada wa Zizzou na kutukana familia yake.
5. Swali la 5 jibu ni Barca kwani Brazili ya 1970 ilikuwa inaishia ukingoni na timu nyingi za kipindi kile zilikuwa hoehae.
6. Ile kombinantion ni ya kijinga kwani jamaa waliwika sana kwenye vilabu vyao ila katika timu ya taifa hawakuweza kutamba na dunia iliwashangaa.
7. Mkuu wacha utani, hata kwa akili yako unaweza kuniambia kuwa Gaucho alikuwa fundi zaidi ya Zizzou? Zizzou ni mrusha mabomu ya uhakika, jamaa ni computer wa karne ijayo. Nawakilisha.
Fact