Baadhi ya Mawaziri Serikali ya Awamu ya Sita wamekuwa na Utajiri wa ghafla usio kifani

Hii sio habari. Ni sawa na kusema mbwa kabwekea vibaka.

Tangu Azimio la Arusha lilipoondolewa kupisha Azimio la Zanzibar, hakuna awamu ya utawala wa CCM ambayo viongozi wakuu hawakujihusisha na wizi, ufisadi na rushwa bila kuchukuliwa hatua. Kusaka utajiri binafsi ndio lengo kuu la watawala wa CCM. Ni suala la makundi, mitandao na wateule katika mtindo wao wa kula kwa zamu, kutesa kwa zamu na kuimba kupokezana.

Tangu enzi zile, hakuna kiongozi wala kada wa CCM aliye kwenye moral high ground kiasi cha kuweza kuwafokea wenzie kuhusu ufisadi. Hivyo, "utajiri wa ghafla" wa baadhi ya viongozi wa CCM sio habari. Hakuna kipya kuhusu hilo. Tujadili mambo ya msingi.
 
Tuna mshukuru mama kwa mara nyingine kwa hili
 
hii ni kweli
 
NI PAMOJA NA KULA KWA ULEVU WA KAMBA ZAO
PER DIEM KUPANDA
ZAWADI KWA KIONGOZI UKIFANYA VIZURI AU UKIMPITISHIA JAMBO LAKE
Sasa na wewe kuandika hujui.
Aliokwambia mtu anatajirika na per diem nan?
Labda useme kukopa benk,sabab slip yako ikiwa vizuri kwa mtumish sasa hiv benk inakupa mpaka mil 220 kwa miez 108.
 
Assume una miaka hamsini ndio umepata uwaziri na ukaanza kuchuma dhambi ya wizi wa Mali ya umma, unadhani itakusaidia Nini wakati huo kisukari, presha na uzee vinakuandama.
Ni observation nzuri.Laiti wangewaza beyond their noses.Na hata kama ungepata huo uwaziri with 40 years,basically una miaka mingine 40 tu ya kuishi kama ukiishi sana,so why don't you start bothering about your eternal life.Unajua mkuu,Shetani tu anawapofusha ili wasiuone ukweli.
 
Imagine MTU ana miaka 60+ hata nguvu za kiume Hana, amekatazwa pombe, nyama na sukari na daktari. Anachukua hongo ya Dola milioni ya Nini?
 
5 na 6 ndio balaa 😰
 
Waliruhusiwa
kula kwa urefu wa kamba zao...sasa hao uliowataja kamba zao ni ndefu sana hivyo wanaweza kula eneo kubwa kuliko wengine!.
 
hapana sikujificha, lakini siku hizi uzushi umezidi sana mpaka unashindwa kujua lipi ni la kweli na lipi ni la propaganda.
Macho yanaona

Masikio yanasikia

Kinachobaki hapo ni wewe kuchambua kwa kutumia ufahamu na akili yako kipi ni propaganda na kipi sio.

By the way, usiopaswa kuwaamini hata wakija kwa sura ya malaika ni CCM yeyote kuanzia Rais Samia Suluhu Hassan hadi mfagizi pale Lumumba!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…