Baadhi ya miradi ya uwekezaji inayoweza kufanywa na wastaafu

Hahaha............kule ungefundishwa Kilimo cha Miti, wakati Upareni umefundishwa biashara na Ubahili

Hapo ushindwe wewe tu, kuninunulia ile Kiko niipendayo 🤗
Nimefundishwa ubahili na kula makande😭😭😭
 
Sitakiiiiiii😭😭😭
Bila Ubahili Mjukuu huwezi kutunza hela ya kununua tofali za nyumba ya ndoto yenu 🤗

Kwahiyo nampongeza Mzee mwenzangu 😜
 
Salaam,

Kila mtumishi aliyeajiriwa, akumbuke itafikia wakati atalazimika kustaafu kazi. Kustaafu huku inaweza kuwa ni kwa hiari ama kulazimishwa kutokana na Umri (Miaka 60 ama 65 kwa Wakufunzi wa Vyuo Vikuu) ama sababu za Ulemavu ama Maradhi yasiyotibika.

Kwa kujua huku kwamba kuna siku tutalazimika kustaafu na kupisha damu changa kwenye utumishi wetu, ndiyo maana inashauriwa kuanza kujiwekeza tangu tarehe ya kwanza unapokea mshahara wako wa kwanza.

Kama mnavyofahamu, Mtumishi akisha staafu, hunufaika na kulipwa kiasi cha 1/3 ya Mshahara wake aliokuwa anapokea wakati anastaafu. Mathalani ikitokea unastaafu ukiwa unapokea mshahara wa shilingi za Kitanzania 1,500,000 kwa Mwezi (Gross Salary) basi ukisha staafu utaanza kulipwa kiasi cha shilingi 500,000 tu hadi siku unaaga Dunia (Kufariki).

Pamoja na hilo, mtumishi huyu atalipwa kiiunua mgongo chake ambacho kwa kikokotoo kipya atalipwa 33% ya fedha zake za Mkupuo.

Kwa taarifa ambazo sio rasmi, watumishi wengi sasa wanapokea fedha zao za Mkupuo unao-range kati ya shilingi 25,000,000 hadi 200,000,000 kulingana na kiwango chako cha mshahara.

Kwa kutambua hili, napenda kuwasisitiza wastaafu watarajiwa, kuhakikisha mnajenga nyumba zenu za kuishi ukiwa bado upo kazini. Ili utakapolipwa fedha zako za kiinua mgongo, basi uzitumie kwenye shughuli nyingine lakini isiwe kujenga.

Kupitia andiko hili, tunaweza kupeana dondoo za aina ya miradi inayoweza kufanywa na Wastaafu ili kujikidhi na maisha yao ya baada ya kustaafu.

  • Uwekezaji kupitia Kilimo Biashara; Ufugaji wa Nyuki,mazao ya chai, matunda, Ufugaji na Kuku wa Kisasa kwaajili ya Mayai na Nyama.
  • Uwekezaji kupitia biashara ya Majengo(Real Estates); Biashara ya GuestHouses, Biashara ya kununua na kuuza viwanja, Nyumba za Kupangisha n.k
  • Biashara mtandao ya kununua na kuuza iwe ni vifaa vya Umeme ama vya nyumbani
  • Biashara kupitia Teknolojia; Kuna baadhi ni wataalamu wa Tehama kama vile Website development, Apps n.k. bila kusahau biashara ya fedha mtandao mfano Mpesa,Airtel Money,CRDB Wakala n.k.
  • Unaweza kuwekeza kwenye Utalii, kwa kufungua kampuni ya Utalii (Safari Tours) n.k, hii ni kwa wale wanaofanya kazi sekta ya Utalii ama wengine wowote.
  • Uwekezaji kupitia Usafirishaji; Iwe Uber/Bolt ama biashara ya kusafirisha mizigo ama parcels
  • Uwekezaji kupitia Vituo vya Elimu, iwe ni daycare centers, Tuitions centers hii ni maalumu kwa Walimu n.k
  • Kuwekeza kupitia huduma za afya iwe ni Maabara binafsi, maduka ya madawa, ama utoaji wa huduma tembezi ya kuwafikia wagonjwa majumbani (Mobile Health clinics)
  • Uwekezaji kupitia Ujenzi; Unaweza kufanya uwekezaji kwa kujisajiri kama Local Fundi na kisha kuanza kuchukua tenda za Ujenzi wa Miradi ya Serikali ama Binafsi, wakati mwingine unaweza kufanya biashara ya kuuza vifaa vya Ujenzi (Hardwares), kiwanda cha kuzalisha tofali n.k
  • Uwekezaji kupitia huduma za Kisheria (Kuanzisha Ofisi za Uwakili) n.k
  • Kufungua kampuni za Ulinzi, kwa wale wenzetu walioajiriwa kwenye idara za Ulinzi na Usalama
Kumbukeni, Uzee bila hela ni changamoto, utaanza kula kwa shida ya kukosa chakula, kukosa matibabu,kukosa sehemu nzuri ya kulala, kukosa hata fedha ya kwenda mapumziko ya Mwisho wa Mwaka. Anza kuwekeza sasa ili uepuke kutokupokelewa kwa simu zako, ukiwapigia Watoto wako, Ndugu,Jamaa na marafiki, bila kusahau kuepuka kuitwa Mchawi (Hakuna mtu mwenye kipato cha wastani/juu akaitwa Mchawi).

Kila la Kheri Wazee na Wastaafu wenzangu watarajiwa
Kuna mda we mzee ukitulia unashusha vitu

Shida ni ukianza kuwafikiria kina jantacash
 
Uzi mzuri ila mi ningekushauri wazo ulielekeze kwa watu wanaojiandaa kistaafu walau 5 to 10 yrs kabla.. ndo waanzishw hizo biashara wakistaafu ni kuziendeleza tu.. kwangu mimi mtu aliestaafu ndo umwambie aanze harakati za biashara yoyote ambayo itahitaji fedha na uzoefu tayar hiyo project inakuwa "dead on arrival"

Kumbuka unamzungumzia mtu mwenyw age ya 60+ ambaye kama
Ulivyosema amestaafu aidha kwa umri au ugonjwa maana yake yuko limited kwenye kila kitu..

So anatakiwa awe tayar ana biashara inayorun ambayo akistaafu ni kuiendelezea tu sio amestaafu pesa ya mafao ndo afikirie biashara ya kufanya na hiyo hiyo pesa ndio aendeshee maisha yake hapo kapoteza..

Biashara ambayo walau inaweza ikawa na guarantee kwa mstaafu kuanzisha ni ile itakayoendana na ujuzi wake mfano daktari kufungua clinic, mwalimu kufungua shule.. na bado kuna hatari na changamoto nyingi zitakazomlazimisha kutoa huduma
Chini ya viwango maana pesa hiyo
Hiyo atataka kuendeshea maisha so atakuwa very sensitive na uwekezaji

Kama mtu anastaaafu na hana biashara inayorun tayar.. anaweza fanya vitu viwili kuiwekeza hiyo
Pesa akawa anapata gawio la
Mwezi.. au kama ni ya kutosha around 200m nusu awekeze kwenye nyumba za kupangiaha nusu kwenye uwekezaji wa magawio ya kila Mwez au quartely

nje ya hapo biashara yoyote lazima awe ukianzisha lazima uwe na cushion fund ambayo itakubeba kwenyw rain days.. sasa fikiria mtu anaona kabisa hii ndio karata ya mwisho atakuwa anafanya maamuzi kimhemuko sana
 
Shukrani Mkuu Kwa kujazia nyama kwenye huu Uzi.

Ushauri wako nimeupokea, japo lengo langu ilikuwa kushea na Wastaafu watarajiwa.

Nimegundua watumishi wengi, hujisahau kuwekeza wakiwa Kazini.

Wakistaafu, wengi huishia kuishi maisha ya taabu na dhiki

Ndiyo maana niliandika walau kukumbushana

By the way, angalizo lako ni muhimu sana kuzingatia kabla hujafanya uamuzi wa kuwekeza.

Kama ulivyosema, mtu akiwa kwenye umri wake wa 60+ hawi na efficiency kwenye biashara za kukimbizana

Ataweza kumudu hizo biashara za real estate tu na sio nyinginezo
 
Eeh naona mvi mbili Tatu hapa😀
Hongera, njoo tuwekeze kwenye Ufugaji wa Kuku za Mayai na Nyama

Najua hatuwezi kukosa laki 4.5 Kila Mwezi kama faida

Tukiongeza na Posho yetu ya Mwezi hatuwezi kukosa hela ya matibabu tukiugua
 
Yan kama ulikuwa kwenye akiliyang natamni sana huo mradi hebu unipe updates
 
Usijali, nitakupatia Mjukuu

Vyema kujiandaa mapema kabla hujasubiri Ustaafu ndiyo ujiandae

Hamtuonei huruma sisi Wazee wenu tunavyopauka na maisha, maana Pension yenyewe tunayopokea ni kidogo hasa tuliostaafu miaka ya 90 kurudi nyuma
 
Back
Top Bottom