Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lakini mzee mwenzangu hujawahi kuniambia nani hasa anaufubaza moyo wako humuš¤£š¤£š¤£au hutaki ijulikane ili uendelee kula mema ya jfšššHapo uhakika Mzee mwenzangu, lazima akunjue roho na mwili ukimimina š¤
Mmmmmmmmmmmmmmh!!Hahaha........mtuombee tu
Ndiyo maana sisi wengine tuliamua kutulia tu na kustaafu hayo mambo š¤
We mdanganye tu, litamkuta jamboš¤£š¤£Hahaha.............ukiendelea kumbembeleza atakubali tu, maana hata yeye alisema anatamani kumpata wa kumtuma glass ya Maji š
Eeeeh ndiwoooo!Maana ya kustaafu ni kupumzika baada ya kufanya kazi kwa miaka yako 60 na kuchoka kimwili na akili. Sitarajii eti mtu anasaafu halafu aendelee na kufuga ua kulima au kufanya biashara. Ukistaafu unatakiwa kupumzika warume! kwa maana hiyo jiwekee sasa vituo vya kukusanya pesa ukishastaafu. Tunataka tumuone mstaafu anaamka asubuhi, anapiga mazoezi yake ya kutembea tartiiiibu, akirudi home anaoga, anapiga breakfast health anapumzika chini ya kamwembe hapo nje na baadae anatoka kwenda kukusanya maokoto mdogo mdogo na kupiga umbea kidogo na majirani.... jioni anaingia kanisani au msikitini anamshukuru Mungu wake anarudi kulalala..... wekend anapanda SGR anaenda kusalimia wajukuu. huku ndio kustaafu
š¤£š¤£š¤£š¤£š¤£Woga wako hauji kuisha, una shida gani mke wanguš š
Thubutuuuu! Nikale makandešāāšššAsipoelewa tumia mbinu ya kumpeleka vacation Milimani kule Upareni, lazima atakubali š
Wazee wa hovyo!Hahaha..................hiyo mbinu lazima ifanye kazi, maana last time alishaanza kuulizia bei ya matairi size 16š
Ila hapo kwenye kumimina yote huwa ni moment nzuri sana Kwa sisi Wazee
Kwa hiyo tunafanyaje my love wangu!!Hebu niwache!!
šššš wewe na nani?Kwa hiyo tunafanyaje my love wangu!!
Na wewe, si hili jambo letu la kutafuta last born wa uzeeni?šššš wewe na nani?
Hebu kale lunch, itakuwa njaa hiyo inakusumbua.Na wewe, si hili jambo letu la kutafuta last born wa uzeeni?
Umenifurahisha! Hivi unadhani kianzio kinatoka wapi? Kustaafu kusikie kwa mwenzako. Kwa upande wetu kustaafu ni kubadili ajira kutoka katika ajira ya serikali kuingia ajira binafsi ambayo ni ngumu ajabu (own account).Salaam,
Kila mtumishi aliyeajiriwa, akumbuke itafikia wakati atalazimika kustaafu kazi. Kustaafu huku inaweza kuwa ni kwa hiari ama kulazimishwa kutokana na Umri (Miaka 60 ama 65 kwa Wakufunzi wa Vyuo Vikuu) ama sababu za Ulemavu ama Maradhi yasiyotibika.
Kwa kujua huku kwamba kuna siku tutalazimika kustaafu na kupisha damu changa kwenye utumishi wetu, ndiyo maana inashauriwa kuanza kujiwekeza tangu tarehe ya kwanza unapokea mshahara wako wa kwanza.
Kama mnavyofahamu, Mtumishi akisha staafu, hunufaika na kulipwa kiasi cha 1/3 ya Mshahara wake aliokuwa anapokea wakati anastaafu. Mathalani ikitokea unastaafu ukiwa unapokea mshahara wa shilingi za Kitanzania 1,500,000 kwa Mwezi (Gross Salary) basi ukisha staafu utaanza kulipwa kiasi cha shilingi 500,000 tu hadi siku unaaga Dunia (Kufariki).
Pamoja na hilo, mtumishi huyu atalipwa kiiunua mgongo chake ambacho kwa kikokotoo kipya atalipwa 33% ya fedha zake za Mkupuo.
Kwa taarifa ambazo sio rasmi, watumishi wengi sasa wanapokea fedha zao za Mkupuo unao-range kati ya shilingi 25,000,000 hadi 200,000,000 kulingana na kiwango chako cha mshahara.
Kwa kutambua hili, napenda kuwasisitiza wastaafu watarajiwa, kuhakikisha mnajenga nyumba zenu za kuishi ukiwa bado upo kazini. Ili utakapolipwa fedha zako za kiinua mgongo, basi uzitumie kwenye shughuli nyingine lakini isiwe kujenga.
Kupitia andiko hili, tunaweza kupeana dondoo za aina ya miradi inayoweza kufanywa na Wastaafu ili kujikidhi na maisha yao ya baada ya kustaafu.
Kumbukeni, Uzee bila hela ni changamoto, utaanza kula kwa shida ya kukosa chakula, kukosa matibabu,kukosa sehemu nzuri ya kulala, kukosa hata fedha ya kwenda mapumziko ya Mwisho wa Mwaka. Anza kuwekeza sasa ili uepuke kutokupokelewa kwa simu zako, ukiwapigia Watoto wako, Ndugu,Jamaa na marafiki, bila kusahau kuepuka kuitwa Mchawi (Hakuna mtu mwenye kipato cha wastani/juu akaitwa Mchawi).
- Uwekezaji kupitia Kilimo Biashara; Ufugaji wa Nyuki,mazao ya chai, matunda, Ufugaji na Kuku wa Kisasa kwaajili ya Mayai na Nyama.
- Uwekezaji kupitia biashara ya Majengo(Real Estates); Biashara ya GuestHouses, Biashara ya kununua na kuuza viwanja, Nyumba za Kupangisha n.k
- Biashara mtandao ya kununua na kuuza iwe ni vifaa vya Umeme ama vya nyumbani
- Biashara kupitia Teknolojia; Kuna baadhi ni wataalamu wa Tehama kama vile Website development, Apps n.k. bila kusahau biashara ya fedha mtandao mfano Mpesa,Airtel Money,CRDB Wakala n.k.
- Unaweza kuwekeza kwenye Utalii, kwa kufungua kampuni ya Utalii (Safari Tours) n.k, hii ni kwa wale wanaofanya kazi sekta ya Utalii ama wengine wowote.
- Uwekezaji kupitia Usafirishaji; Iwe Uber/Bolt ama biashara ya kusafirisha mizigo ama parcels
- Uwekezaji kupitia Vituo vya Elimu, iwe ni daycare centers, Tuitions centers hii ni maalumu kwa Walimu n.k
- Kuwekeza kupitia huduma za afya iwe ni Maabara binafsi, maduka ya madawa, ama utoaji wa huduma tembezi ya kuwafikia wagonjwa majumbani (Mobile Health clinics)
- Uwekezaji kupitia Ujenzi; Unaweza kufanya uwekezaji kwa kujisajiri kama Local Fundi na kisha kuanza kuchukua tenda za Ujenzi wa Miradi ya Serikali ama Binafsi, wakati mwingine unaweza kufanya biashara ya kuuza vifaa vya Ujenzi (Hardwares), kiwanda cha kuzalisha tofali n.k
- Uwekezaji kupitia huduma za Kisheria (Kuanzisha Ofisi za Uwakili) n.k
- Kufungua kampuni za Ulinzi, kwa wale wenzetu walioajiriwa kwenye idara za Ulinzi na Usalama
Kila la Kheri Wazee na Wastaafu wenzangu watarajiwa
Mtumishi una uwezo wa kukopeshwa na Benki Kwa dhamana ya mshaharaUmenifurahisha! Hivi unadhani kianzio kinatoka wapi? Kustaafu kusikie kwa mwenzako. Kwa upande wetu kustaafu ni kubadili ajira kutoka katika ajira ya serikali kuingia ajira binafsi ambayo ni ngumu ajabu (own account).