Baadhi ya miradi ya uwekezaji inayoweza kufanywa na wastaafu

Baadhi ya miradi ya uwekezaji inayoweza kufanywa na wastaafu

Mzee mwenzangu bado ana nguvu za kutafuta wa Uzeeni?

Mimi nina mmoja nilimpata nikiwa na miaka 68, saivi nipo namlipia ada

Ndiyo maana nisingependa Wazee wenzangu kurudia hilo kosa 😜
Hii ndio raha ya kuwa mwanaume mpaka miaka 68 bado unaperfom...!
 
Maana ya kustaafu ni kupumzika baada ya kufanya kazi kwa miaka yako 60 na kuchoka kimwili na akili. Sitarajii eti mtu anasaafu halafu aendelee na kufuga ua kulima au kufanya biashara. Ukistaafu unatakiwa kupumzika warume! kwa maana hiyo jiwekee sasa vituo vya kukusanya pesa ukishastaafu. Tunataka tumuone mstaafu anaamka asubuhi, anapiga mazoezi yake ya kutembea tartiiiibu, akirudi home anaoga, anapiga breakfast health anapumzika chini ya kamwembe hapo nje na baadae anatoka kwenda kukusanya maokoto mdogo mdogo na kupiga umbea kidogo na majirani.... jioni anaingia kanisani au msikitini anamshukuru Mungu wake anarudi kulalala..... wekend anapanda SGR anaenda kusalimia wajukuu. huku ndio kustaafu
Nimeipenda hii hakika😅
 
Salaam,

Kila mtumishi aliyeajiriwa, akumbuke itafikia wakati atalazimika kustaafu kazi. Kustaafu huku inaweza kuwa ni kwa hiari ama kulazimishwa kutokana na Umri (Miaka 60 ama 65 kwa Wakufunzi wa Vyuo Vikuu) ama sababu za Ulemavu ama Maradhi yasiyotibika.

Kwa kujua huku kwamba kuna siku tutalazimika kustaafu na kupisha damu changa kwenye utumishi wetu, ndiyo maana inashauriwa kuanza kujiwekeza tangu tarehe ya kwanza unapokea mshahara wako wa kwanza.

Kama mnavyofahamu, Mtumishi akisha staafu, hunufaika na kulipwa kiasi cha 1/3 ya Mshahara wake aliokuwa anapokea wakati anastaafu. Mathalani ikitokea unastaafu ukiwa unapokea mshahara wa shilingi za Kitanzania 1,500,000 kwa Mwezi (Gross Salary) basi ukisha staafu utaanza kulipwa kiasi cha shilingi 500,000 tu hadi siku unaaga Dunia (Kufariki).

Pamoja na hilo, mtumishi huyu atalipwa kiiunua mgongo chake ambacho kwa kikokotoo kipya atalipwa 33% ya fedha zake za Mkupuo.

Kwa taarifa ambazo sio rasmi, watumishi wengi sasa wanapokea fedha zao za Mkupuo unao-range kati ya shilingi 25,000,000 hadi 200,000,000 kulingana na kiwango chako cha mshahara.

Kwa kutambua hili, napenda kuwasisitiza wastaafu watarajiwa, kuhakikisha mnajenga nyumba zenu za kuishi ukiwa bado upo kazini. Ili utakapolipwa fedha zako za kiinua mgongo, basi uzitumie kwenye shughuli nyingine lakini isiwe kujenga.

Kupitia andiko hili, tunaweza kupeana dondoo za aina ya miradi inayoweza kufanywa na Wastaafu ili kujikidhi na maisha yao ya baada ya kustaafu.

  • Uwekezaji kupitia Kilimo Biashara; Ufugaji wa Nyuki,mazao ya chai, matunda, Ufugaji na Kuku wa Kisasa kwaajili ya Mayai na Nyama.
  • Uwekezaji kupitia biashara ya Majengo(Real Estates); Biashara ya GuestHouses, Biashara ya kununua na kuuza viwanja, Nyumba za Kupangisha n.k
  • Biashara mtandao ya kununua na kuuza iwe ni vifaa vya Umeme ama vya nyumbani
  • Biashara kupitia Teknolojia; Kuna baadhi ni wataalamu wa Tehama kama vile Website development, Apps n.k. bila kusahau biashara ya fedha mtandao mfano Mpesa,Airtel Money,CRDB Wakala n.k.
  • Unaweza kuwekeza kwenye Utalii, kwa kufungua kampuni ya Utalii (Safari Tours) n.k, hii ni kwa wale wanaofanya kazi sekta ya Utalii ama wengine wowote.
  • Uwekezaji kupitia Usafirishaji; Iwe Uber/Bolt ama biashara ya kusafirisha mizigo ama parcels
  • Uwekezaji kupitia Vituo vya Elimu, iwe ni daycare centers, Tuitions centers hii ni maalumu kwa Walimu n.k
  • Kuwekeza kupitia huduma za afya iwe ni Maabara binafsi, maduka ya madawa, ama utoaji wa huduma tembezi ya kuwafikia wagonjwa majumbani (Mobile Health clinics)
  • Uwekezaji kupitia Ujenzi; Unaweza kufanya uwekezaji kwa kujisajiri kama Local Fundi na kisha kuanza kuchukua tenda za Ujenzi wa Miradi ya Serikali ama Binafsi, wakati mwingine unaweza kufanya biashara ya kuuza vifaa vya Ujenzi (Hardwares), kiwanda cha kuzalisha tofali n.k
  • Uwekezaji kupitia huduma za Kisheria (Kuanzisha Ofisi za Uwakili) n.k
  • Kufungua kampuni za Ulinzi, kwa wale wenzetu walioajiriwa kwenye idara za Ulinzi na Usalama
Kumbukeni, Uzee bila hela ni changamoto, utaanza kula kwa shida ya kukosa chakula, kukosa matibabu,kukosa sehemu nzuri ya kulala, kukosa hata fedha ya kwenda mapumziko ya Mwisho wa Mwaka. Anza kuwekeza sasa ili uepuke kutokupokelewa kwa simu zako, ukiwapigia Watoto wako, Ndugu,Jamaa na marafiki, bila kusahau kuepuka kuitwa Mchawi (Hakuna mtu mwenye kipato cha wastani/juu akaitwa Mchawi).

Kila la Kheri Wazee na Wastaafu wenzangu watarajiwa
Hakuna haja ya kuanzisha mradi mpya katika umri maana muda sio mrefu utaaga dunia.
 
Hakuna haja ya kuanzisha mradi mpya katika umri maana muda sio mrefu utaaga dunia.
Utaisheje kabla hujafa

Maana Kuna watu wanaishi miaka mingi baada ya kustaafu

Hapo juu nimeeleza nina Mzee wangu amestaafu miaka ya 90 mwanzoni

Hadi sasa yupo hai, vipi angekuwa Hana kipato cha ziada? Maana Mishahara ya miaka ya zamani mingi ilikuwa haizidi elfu30
 
Hahaha.............ukiendelea kumbembeleza atakubali tu, maana hata yeye alisema anatamani kumpata wa kumtuma glass ya Maji 😜
Unajua mzee mwenzangu, hii inahitaji mbinu kidogo, natafuta kamkoko kwa ajili yake...

..nikimwambia kamkoko haka ni kwa ajili yako najua usiku wake napewa na kuambiwa babe miminia yote😀😀😀😀🤣
 
Unajua mzee mwenzangu, hii inahitaji mbinu kidogo, natafuta kamkoko kwa ajili yake...

..nikimwambia kamkoko haka ni kwa ajili yako najua usiku wake napewa na kuambiwa babe miminia yote😀😀😀😀🤣
Hahaha..................hiyo mbinu lazima ifanye kazi, maana last time alishaanza kuulizia bei ya matairi size 16😜

Ila hapo kwenye kumimina yote huwa ni moment nzuri sana Kwa sisi Wazee
 
Back
Top Bottom