Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sababu zilizotolewa na watetezi wanasema eti sisi Wazee wa Kiume tulikuwa tunaibiwa hela zote za Pension na wachuchu bila kuzifikisha nyumbani.Ila yule baba!! Acha alale tu🙌🙌
Kwa hicho kipato cha almost 1M Kwa Mwezi kinamtosha kabisa MstaafuMstafu yoyote asipofanya chochote kwa hela zake,atazila mpaka kufa.Mfano Mama yangu alikuwa Mwalimu mafao yake alipata 92.5M na fedha ya kila mwezi anapata 500K.
Alisitafu na 55,ukiweka makadirio kuwa ataishi 25 yrs to come maana yake ataishi mpaka 80 yrs.Akisema atumie 92.5 kwa miaka hiyo 25 kila mwaka atatumia 3.7M wastani wa 308,000 kwa mwezi,fedha hii ukijumuisha na 500K anayopata kila mwezi maana yake kila mwezi atakuwa na kipato cha 800K.
Kwa mstafu anayeishi wilayani 800,000 ni hela nyingi sana,ukitegemea hana mtoto hata moja anamtegemea.
Ni lazima kuwa strategic mzee, yaani ukishafika 45yrs habari ya kuzaa achana nayo kabisa, labda kwa mtu mwenye changamoto za uzazi, ila umri huo ukijumlisha 20 manake ukiwa na 65 bado unasumbuka na kusomesha....Kwa hicho kipato cha almost 1M Kwa Mwezi kinamtosha kabisa Mstaafu
Muhimu asiwe na stress za kusomesha wakati huo
Ndiyo maana katika vitu sipendi ni kuendelea kuzalisha watoto hata baada ya miaka 45
Ukifanya hilo kosa, ni lazima utakuwa unatumia kipato chako cha Pension kulipia ada watoto wako maana wakati huo watakuwa Sekondari🙌
Wapuuzi kweli!Sababu zilizotolewa na watetezi wanasema eti sisi Wazee wa Kiume tulikuwa tunaibiwa hela zote za Pension na wachuchu bila kuzifikisha nyumbani.
Nikasema hivi hawa jamaa, wanafikiri Mzee wa Kipare ERoni anaweza kweli kuibiwa na Mwanamke hata elfu 10 yake ya Pension?
All in all sababu zao, hazikuwa na mashiko, maana kama ni watumishi wote wa Umma mbona Wabunge wanapewa zote Kila baada ya miaka 5
Cc ERoniKwa hicho kipato cha almost 1M Kwa Mwezi kinamtosha kabisa Mstaafu
Muhimu asiwe na stress za kusomesha wakati huo
Ndiyo maana katika vitu sipendi ni kuendelea kuzalisha watoto hata baada ya miaka 45
Ukifanya hilo kosa, ni lazima utakuwa unatumia kipato chako cha Pension kulipia ada watoto wako maana wakati huo watakuwa Sekondari🙌
Tutafute wa nwisho wa uzeeni babe!!
Uzi mzuri...Salaam,
Kila mtumishi aliyeajiriwa, akumbuke itafikia wakati atalazimika kustaafu kazi. Kustaafu huku inaweza kuwa ni kwa hiari ama kulazimishwa kutokana na Umri (Miaka 60 ama 65 kwa Wakufunzi wa Vyuo Vikuu) ama sababu za Ulemavu ama Maradhi yasiyotibika.
Kwa kujua huku kwamba kuna siku tutalazimika kustaafu na kupisha damu changa kwenye utumishi wetu, ndiyo maana inashauriwa kuanza kujiwekeza tangu tarehe ya kwanza unapokea mshahara wako wa kwanza.
Kama mnavyofahamu, Mtumishi akisha staafu, hunufaika na kulipwa kiasi cha 1/3 ya Mshahara wake aliokuwa anapokea wakati anastaafu. Mathalani ikitokea unastaafu ukiwa unapokea mshahara wa shilingi za Kitanzania 1,500,000 kwa Mwezi (Gross Salary) basi ukisha staafu utaanza kulipwa kiasi cha shilingi 500,000 tu hadi siku unaaga Dunia (Kufariki).
Pamoja na hilo, mtumishi huyu atalipwa kiiunua mgongo chake ambacho kwa kikokotoo kipya atalipwa 33% ya fedha zake za Mkupuo.
Kwa taarifa ambazo sio rasmi, watumishi wengi sasa wanapokea fedha zao za Mkupuo unao-range kati ya shilingi 25,000,000 hadi 200,000,000 kulingana na kiwango chako cha mshahara.
Kwa kutambua hili, napenda kuwasisitiza wastaafu watarajiwa, kuhakikisha mnajenga nyumba zenu za kuishi ukiwa bado upo kazini. Ili utakapolipwa fedha zako za kiinua mgongo, basi uzitumie kwenye shughuli nyingine lakini isiwe kujenga.
Kupitia andiko hili, tunaweza kupeana dondoo za aina ya miradi inayoweza kufanywa na Wastaafu ili kujikidhi na maisha yao ya baada ya kustaafu.
Kumbukeni, Uzee bila hela ni changamoto, utaanza kula kwa shida ya kukosa chakula, kukosa matibabu,kukosa sehemu nzuri ya kulala, kukosa hata fedha ya kwenda mapumziko ya Mwisho wa Mwaka. Anza kuwekeza sasa ili uepuke kutokupokelewa kwa simu zako, ukiwapigia Watoto wako, Ndugu,Jamaa na marafiki, bila kusahau kuepuka kuitwa Mchawi (Hakuna mtu mwenye kipato cha wastani/juu akaitwa Mchawi).
- Uwekezaji kupitia Kilimo Biashara; Ufugaji wa Nyuki,mazao ya chai, matunda, Ufugaji na Kuku wa Kisasa kwaajili ya Mayai na Nyama.
- Uwekezaji kupitia biashara ya Majengo(Real Estates); Biashara ya GuestHouses, Biashara ya kununua na kuuza viwanja, Nyumba za Kupangisha n.k
- Biashara mtandao ya kununua na kuuza iwe ni vifaa vya Umeme ama vya nyumbani
- Biashara kupitia Teknolojia; Kuna baadhi ni wataalamu wa Tehama kama vile Website development, Apps n.k. bila kusahau biashara ya fedha mtandao mfano Mpesa,Airtel Money,CRDB Wakala n.k.
- Unaweza kuwekeza kwenye Utalii, kwa kufungua kampuni ya Utalii (Safari Tours) n.k, hii ni kwa wale wanaofanya kazi sekta ya Utalii ama wengine wowote.
- Uwekezaji kupitia Usafirishaji; Iwe Uber/Bolt ama biashara ya kusafirisha mizigo ama parcels
- Uwekezaji kupitia Vituo vya Elimu, iwe ni daycare centers, Tuitions centers hii ni maalumu kwa Walimu n.k
- Kuwekeza kupitia huduma za afya iwe ni Maabara binafsi, maduka ya madawa, ama utoaji wa huduma tembezi ya kuwafikia wagonjwa majumbani (Mobile Health clinics)
- Uwekezaji kupitia Ujenzi; Unaweza kufanya uwekezaji kwa kujisajiri kama Local Fundi na kisha kuanza kuchukua tenda za Ujenzi wa Miradi ya Serikali ama Binafsi, wakati mwingine unaweza kufanya biashara ya kuuza vifaa vya Ujenzi (Hardwares), kiwanda cha kuzalisha tofali n.k
- Uwekezaji kupitia huduma za Kisheria (Kuanzisha Ofisi za Uwakili) n.k
- Kufungua kampuni za Ulinzi, kwa wale wenzetu walioajiriwa kwenye idara za Ulinzi na Usalama
Kila la Kheri Wazee na Wastaafu wenzangu watarajiwa
Huyu atasaidia kutuondolea upweke mzee mwenzangu😆😆😆 tutazeeka nako...Mzee mwenzangu bado unataka kuendelea kusomesha watoto Kwa hela ya Pension
Tena watoto wenyewe hawa, Shule wanazo soma Kila Mwaka wanaenda Vacation South Africa🙌
Hapo mmefanya vizuri, maana maisha ya Uzee bila Wajukuu ama watoto wa kuwafanyia fujo kidogo inakuwa Mtihani sanaHuyu atasaidia kutuondolea upweke mzee mwenzangu😆😆😆 tutazeeka nako...
Azitoe wapi!!! Anajitutumua tu🙆♂️Mzee mwenzangu bado ana nguvu za kutafuta wa Uzeeni?
Aaah wewe tena!!Mimi nina mmoja nilimpata nikiwa na miaka 68, saivi nipo namlipia ada
Ndiyo maana nisingependa Wazee wenzangu kurudia hilo kosa 😜
Ushindwe na ulegee🤣Tutafute wa nwisho wa uzeeni babe!!
Shule za kata zipo🤣🤣Mzee mwenzangu bado unataka kuendelea kusomesha watoto Kwa hela ya Pension
Tena watoto wenyewe hawa, Shule wanazo soma Kila Mwaka wanaenda Vacation South Africa🙌
🤣🤣🤣🤣🤣 ananifundisha tu vitu vya ajabu ajabu.Angalia Mpare asikufundishe Upare wake hadi Kwa Mimi Babu yako
Maana tangu nimeomba uninunulie Kiko imepita miezi 8 sasa na Kiko haiji 😜
🤣🤣🤣🤣Kama mtu hakufanya biashara kabisa wakati wa ajira basi akistaafu mradi pekee usio na stress kwake ni kulea wajukuu zake tu.