Baadhi ya miradi ya uwekezaji inayoweza kufanywa na wastaafu

Baadhi ya miradi ya uwekezaji inayoweza kufanywa na wastaafu

Hapo mmefanya vizuri, maana maisha ya Uzee bila Wajukuu ama watoto wa kuwafanyia fujo kidogo inakuwa Mtihani sana
Mdangane tu ajichanganye🤣
Maana Atoto wakati huo atakuwa anapiga tripu za Mjini Kila mara kwenda kusalimia watoto wenu, wakati huo wewe utakuwa unaambiwa ukae nyumbani kulinda nyumba 😜🙌
Baba ni mlinzi wa familia🤣🤣🤣
 
🤣🤣🤣🤣🤣 ananifundisha tu vitu vya ajabu ajabu.
Babu kiko si nilikulerea ukaikataa!! Pambana na hali yako🤪
Hahaha.............. tafadhali mwambie akufundishe vyote sio Upare wake tu

Maana tuliowahi kuwa-date wapare tunajua tuliyopitia

Mtu unampa hela ya Nyama lakini unapikiwa ugali na vidagaa Mchanga kweli 🙌
 
Bora hata vidagaa mchanga, huku ni mwendo wa makande tu! Hata nuru nimekosa🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Hapo mmefanya vizuri, maana maisha ya Uzee bila Wajukuu ama watoto wa kuwafanyia fujo kidogo inakuwa Mtihani sana

Maana Atoto wakati huo atakuwa anapiga tripu za Mjini Kila mara kwenda kusalimia watoto wenu, wakati huo wewe utakuwa unaambiwa ukae nyumbani kulinda nyumba 😜🙌
Nikiwa na kitinda mimba hata aende kukaa mwaka sina shida...muhimu ni maokoto tu mzee mwenzangu!😆
 
Kama mtu hakufanya biashara kabisa wakati wa ajira basi akistaafu mradi pekee usio na stress kwake ni kulea wajukuu zake tu.

Ila kama alikuwa ana biashara aendelee kujichanganya na biashara yake asifikirie kama kastafu, itamsaidia

Ila bhana usije ukajichanganya kutaka kumshauri Mstaafu, kamwe hamtaelewana hata kama ni mzazi wako wewe muache tu alivyo 😂
Bora umshauri akikataa unamwacha, uzuri wake unaweza kumshauri Kwa maandishi kama hivi

Akienda tofauti una mprintia na kumpeleka docs kama ushahidi

Suala la kujifunza kujiwekeza ni muhimu sana, ndiyo maana baadhi ya Ofisi kwenye vile vikao vya mwisho wa Mwaka, mnapewa hizo risala na Maboss wenu

Wakati mwingine mnaletewa hadi Washauri

Ofisi ambazo watumishi wake hawajishughulishi, zinaongoza Kwa majungu aisee
 
Ndugu usidanganye wastaafu, hakuna biashara anaweza kuifanya kwa ustadi at age 60 - 65.

Wewe umekaa ofisini miaka 40 hujawahi hata kuuza maji ya uhai mtaani kwa jumla leo hii uanze uwekezaji kwenye kilimo ama biashara utakufa siku si zako kwanza kikubwa hata thinking yako na mwili ushaanza kuchoka.

Kitu pekee umaweza kufanya ni kuwekeza kiinua mgongo chako benki ili wakulipe faida ya depost yako...unakula polepole hadi cku ya msiba wako hela iwepo ya jeneza na chakula kwa waombolezaji.

Unaweza pia kuwekeza kwenye soko la hisa kama huo utaalamu unao - yaani ulikuwa kwenye fani ya Biashara na uwekezaji kipindi cha ajira yako.

Ni ushauri tu ili wewe mstaafu usije kulia na ukose wa kukufuta machozi kama wenzako eti kuwekeza kwenye kilimo & ufugaji,
 
Nikiwa na kitinda mimba hata aende kukaa mwaka sina shida...muhimu ni maokoto tu mzee mwenzangu!😆
Hahaha..............na kweli, maana Kwa huo umri hata huwezi kuwa na wivu naye sana ila yeye ndiyo atakuwa nao kwako

Maana asipokaba hadi penati atakuta umevizalisha vitoto vya elfu 2 😜
 
Hahaha..............na kweli, maana Kwa huo umri hata huwezi kuwa na wivu naye sana ila yeye ndiyo atakuwa nao kwako

Maana asipokaba hadi penati atakuta umevizalisha vitoto vya elfu 2 😜
🤣🤣🤣🤣 sasa akivizalisha si ni stress zake mwenyewe!!
 
Salaam,

Kila mtumishi aliyeajiriwa, akumbuke itafikia wakati atalazimika kustaafu kazi. Kustaafu huku inaweza kuwa ni kwa hiari ama kulazimishwa kutokana na Umri (Miaka 60 ama 65 kwa Wakufunzi wa Vyuo Vikuu) ama sababu za Ulemavu ama Maradhi yasiyotibika.

Kwa kujua huku kwamba kuna siku tutalazimika kustaafu na kupisha damu changa kwenye utumishi wetu, ndiyo maana inashauriwa kuanza kujiwekeza tangu tarehe ya kwanza unapokea mshahara wako wa kwanza.

Kama mnavyofahamu, Mtumishi akisha staafu, hunufaika na kulipwa kiasi cha 1/3 ya Mshahara wake aliokuwa anapokea wakati anastaafu. Mathalani ikitokea unastaafu ukiwa unapokea mshahara wa shilingi za Kitanzania 1,500,000 kwa Mwezi (Gross Salary) basi ukisha staafu utaanza kulipwa kiasi cha shilingi 500,000 tu hadi siku unaaga Dunia (Kufariki).

Pamoja na hilo, mtumishi huyu atalipwa kiiunua mgongo chake ambacho kwa kikokotoo kipya atalipwa 33% ya fedha zake za Mkupuo.

Kwa taarifa ambazo sio rasmi, watumishi wengi sasa wanapokea fedha zao za Mkupuo unao-range kati ya shilingi 25,000,000 hadi 200,000,000 kulingana na kiwango chako cha mshahara.

Kwa kutambua hili, napenda kuwasisitiza wastaafu watarajiwa, kuhakikisha mnajenga nyumba zenu za kuishi ukiwa bado upo kazini. Ili utakapolipwa fedha zako za kiinua mgongo, basi uzitumie kwenye shughuli nyingine lakini isiwe kujenga.

Kupitia andiko hili, tunaweza kupeana dondoo za aina ya miradi inayoweza kufanywa na Wastaafu ili kujikidhi na maisha yao ya baada ya kustaafu.

  • Uwekezaji kupitia Kilimo Biashara; Ufugaji wa Nyuki,mazao ya chai, matunda, Ufugaji na Kuku wa Kisasa kwaajili ya Mayai na Nyama.
  • Uwekezaji kupitia biashara ya Majengo(Real Estates); Biashara ya GuestHouses, Biashara ya kununua na kuuza viwanja, Nyumba za Kupangisha n.k
  • Biashara mtandao ya kununua na kuuza iwe ni vifaa vya Umeme ama vya nyumbani
  • Biashara kupitia Teknolojia; Kuna baadhi ni wataalamu wa Tehama kama vile Website development, Apps n.k. bila kusahau biashara ya fedha mtandao mfano Mpesa,Airtel Money,CRDB Wakala n.k.
  • Unaweza kuwekeza kwenye Utalii, kwa kufungua kampuni ya Utalii (Safari Tours) n.k, hii ni kwa wale wanaofanya kazi sekta ya Utalii ama wengine wowote.
  • Uwekezaji kupitia Usafirishaji; Iwe Uber/Bolt ama biashara ya kusafirisha mizigo ama parcels
  • Uwekezaji kupitia Vituo vya Elimu, iwe ni daycare centers, Tuitions centers hii ni maalumu kwa Walimu n.k
  • Kuwekeza kupitia huduma za afya iwe ni Maabara binafsi, maduka ya madawa, ama utoaji wa huduma tembezi ya kuwafikia wagonjwa majumbani (Mobile Health clinics)
  • Uwekezaji kupitia Ujenzi; Unaweza kufanya uwekezaji kwa kujisajiri kama Local Fundi na kisha kuanza kuchukua tenda za Ujenzi wa Miradi ya Serikali ama Binafsi, wakati mwingine unaweza kufanya biashara ya kuuza vifaa vya Ujenzi (Hardwares), kiwanda cha kuzalisha tofali n.k
  • Uwekezaji kupitia huduma za Kisheria (Kuanzisha Ofisi za Uwakili) n.k
  • Kufungua kampuni za Ulinzi, kwa wale wenzetu walioajiriwa kwenye idara za Ulinzi na Usalama
Kumbukeni, Uzee bila hela ni changamoto, utaanza kula kwa shida ya kukosa chakula, kukosa matibabu,kukosa sehemu nzuri ya kulala, kukosa hata fedha ya kwenda mapumziko ya Mwisho wa Mwaka. Anza kuwekeza sasa ili uepuke kutokupokelewa kwa simu zako, ukiwapigia Watoto wako, Ndugu,Jamaa na marafiki, bila kusahau kuepuka kuitwa Mchawi (Hakuna mtu mwenye kipato cha wastani/juu akaitwa Mchawi).

Kila la Kheri Wazee na Wastaafu wenzangu watarajiwa
Iko POA .Lakin sio mpaka tustaafu hata kabla ya kustaafu tunaweza kuchukua baadh na kuwekeza ili kuwa na vyanzo vingi vya kipato Zaidi ya mshahara. Maana Kila aliyeajiriwa nimstaaf mtarajiwa na muda was kujiandaa kustaafu ni kabla ya kustaafu
 
Ndugu usidanganye wastaafu, hakuna biashara anaweza kuifanya kwa ustadi at age 60 - 65.

Wewe umekaa ofisini miaka 40 hujawahi hata kuuza maji ya uhai mtaani kwa jumla leo hii uanze uwekezaji kwenye kilimo ama biashara utakufa siku si zako kwanza kikubwa hata thinking yako na mwili ushaanza kuchoka.

Kitu pekee umaweza kufanya ni kuwekeza kiinua mgongo chako benki ili wakulipe faida ya depost yako...unakula polepole hadi cku ya msiba wako hela iwepo ya jeneza na chakula kwa waombolezaji.

Unaweza pia kuwekeza kwenye soko la hisa kama huo utaalamu unao - yaani ulikuwa kwenye fani ya Biashara na uwekezaji kipindi cha ajira yako.

Ni ushauri tu ili wewe mstaafu usije kulia na ukose wa kukufuta machozi kama wenzako eti kuwekeza kwenye kilimo & ufugaji,
Ni sahihi Mkuu

Ndiyo maana tumeshauri kwamba suala la kuwekeza ni endelevu

Inatupasa wote tuanze kujifunza kuwekeza

Of course ukianza Uwekezaji at 60-65 lazima utapoteza Mtaji wote maana ishu ya usimamizi itakuwa vigumu Kwa umri huo
 
Back
Top Bottom