Baadhi ya ndugu wauza nyumba ya familia Kariakoo iliyokuwa na waqfu. Mapanga yatembea nje nje

Ila kama baba yao alishatoa wosia rasmi kwamba wasiuze, basi waendelee tu kugawana kodi ya Jengo sawa kwa sawa hadi pale watakapokubaliana wote pauzwe..
 
Mkinga hajui hilo
Inapaswa afahamu, kama mali inamilikiwa na warithi kwa pamoja ambapo wanachukua tu kodi kwa kugawana, ni lazima kipindi cha kuuza warithi wote wakubali kuuza, haweza akaamua mmoja kuuza kwa niaba ya wenzake bila makubaliano, huo utakuwa mgogoro mzito sana
 
Nipo Kariakoo, anaesimamia hiyo nyumba ni dd yao. Ishu ni kua anawapiga ndugu zake. Mfano frem ni 1,000,000 anawaambia wenzake kodi ni 600,000. Hiyo ndo shida
Kwa hiyo ni sawa ilivyouzwa bila hata yeye kuhusishwa?
We mtu una akili inayofanyakazi kweli?

Dhuluma ya Kodi ndo inampora mtu uhalali wa urithi?
 
Mkinga ameyakanyaga. Kama alienda bila utaratibu wa kisheria ana kesi kadhaa hapo za jinai zikiwemo za, Uvamizi, Kuvunja, Kuiba, Kuharibu mali, Shambulizi la maungoni na kadhalika....

Tatizo la Tannzania ni jeshi la polisi kushirikiana na wahalifu wanaosumbua jamii. Na kibaya zaidi tuna mkuu wa Jeshi la Polisi ambaye hajawahi kuwa na huruma kwa raia zaidi ya kuwalinda viongozi na kutiii amri zao hata kama ni za kindezi ndezi.

Hapo ni halali kabisa Rais kuingilia kati hili suala.
 
WAISIHARAMU SIKU HIZI NDIYO WAMEJIVISHA NGOZI YA UISLAMU
 
Hacha kupotosha watu,Mke na mume wakienda kukopa hela kupitia Nyumba ya Familia lazima wakopeshaji waje kuulizia kama kweli familia imekubaliana na maamuzia ya Mkopoaji,lazima baba na mama wapige picha nje ya Nyumba na kama anawatoto pia watapiga picha kukubaliana na ilo swala tena mbele ya nyumba na sahihi kuwekwa na vidole Gumba juu.
 
Nipo Kariakoo, anaesimamia hiyo nyumba ni dd yao. Ishu ni kua anawapiga ndugu zake. Mfano frem ni 1,000,000 anawaambia wenzake kodi ni 600,000. Hiyo ndo shida

Sasa wao wanashindwa kuwauliza wapangaji wao?! Mbona ni jambo dogo tu?!!
 
Imagine baunsa umekodishwa unalipwa elfu 30 kwa siku. Unaenda kwenye kazi unakutana na mapanga watu wanalinda mali yao.

Baunsa Unapigwa mapanga kwenye mali isiyo kuhusu
Yaani watu wanapiganua mabillion
Wewe unarisk maisha kwa ajili 30k
 
Nyumba ya mirathi ina taratibu zake kuuza.Huwezi kuuza kitu cha watu wengi,kijanja janja.Huyo Sheikh,na huyo mnunuzi wakamatwe,ni wezi hao na ni matapeli,na kama yupo wakili,kahusika na huu utapeli,pia akamatwe.
Nani awakamate,polisi ndiyo hao waliahidi usalama na baadaye kuonekana pamoja Mkinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…