Chasha, nataka kujifanya Musa, niwatoe wanaisrael kutoka misri hadi nchi ya ahadi... kuna vikundi kijijini kwangu, ni masikini sana na hawana elimu yoyote. maisha yao ni shida sana. nataka kuwa-support waweze kuwa na miradi yao ya uzalishaji (IGA). nimepitia literature nyingi za entrepreneurship, nimejenga imani kuwa katika makundi ufanisi utakuwa mdogo kuliko nikiwa-support mojammoja (...may be am wrong).
Challenge niliyoiona ni kwamba mawazo wanayotoa wao (yaani types of IGA they propose) naona kama hazitaleta faida/tija yoyote na pengine nitapoteza bure msaada wangu wasibadilike chochote katika maisha yao. Naomba unishauri, naweza kuwabunia biashara ya kufanya ambayo haipo akilini mwao? ni jinsi gani naweza kuwashauri wazo langu likawanufaisha?
Nitashukuru pia kama utanipanua mawazo zaidi