Ya mkuu ni wewe tu, Watu engi uoga tulio nao uko ktika sehemu hizi
1. Kuchekwa
2. Kudharauliwa mtaani,
3. Kuhofia kama ukiflisika mpenzi wako unaye mpeda sana atakula kona,
4. Majirani wenzako watakupiku make ushazoea kushindana kimaisha hapo mtaani
5. Kuhofia kupoteza pesa zote
6. Kufofia lawama kutoka kw wazazi make ulishazoea kuwatoa na sasa hutakuwa unawatoa kwa wingi kama zamani,
7. Kuhofia kupoteza washikaji wa mtaa ambao mlikuwa mnabadili viwanja kila siku,
8. Kazini kwangu watanishaangaa sana na kuniona kama nimechanganyikiwa vile,
9. Nilikuwa napiga sana misere na gari la ofisi sasa itanibidi niwe na piga mguu au kupanda Toyo,
UKIYAZINGATIA HAYA HAKIKA, UJASIRIAMALI SI SEHEMU YAKO, NA HUTAWEZA KAMWE
Mkuu Chasha maneno yako yameshanikamata, ninapita kwenye kipindi cha mpito, nimeshakiona kisiwa na meli nimeshaipaki tayari! Nachoma moto meli mieeeeee !!!:
1. Kuchekwa: kwa akili yangu nikipiga mahesabu nimejiridhisha hii kitu nikiifanya vizuri natapiga hela kubwa kama ikitokea nikapiga mweleka atakaecheka na acheke salama, maana hata hivyo nitakuwa nimeshajifunza kitu ambacho anaenicheka hajui, na nikijinyanyua na kusimama tena baada ya mieleka kadhaa iko siku nitasimama imara na hapo wanichekao ndiyo watatafuta njia ya kupita kwa aibu na wivu! Na hili ndilo linalonitia nguvu zaidi badala ya kunitia hofu ya kuchekwa! Kama ni kuchekwa kwa ajili ya biashara ya mkaa afadhari nipate pesa kuliko kuendekeza ubishoo huku pesa ya kujirusha sina.
2. Kudharauliwa mtaani: acha wanidharau najua kudharauliwa ni jambo la muda mfupi tu, mimi natazama miaka mingi mbeleni, najua hii ni safari na ninaijua mimi mwenyewe, wao hawaijui, shida ninazopata mimi wao hawazijui na haziwahusu, nafuu yao ya maisha mimi hainihusu, siku nikifika safari yangu wao wale wale wataanza kusema tulipiga nae soga mtaani kwetu siku hizi anaringa!
3. Kuhofia kama ukiflisika mpenzi wako unaye mpeda sana atakula kona: Ndiyo ninalijua hilo kwamba mpenzi wangu kinachotuunganisha nae hivi sasa ni pesa tu, ni kweli kwamba nikifilisika atanikimbia, so sasa nachukua maamuzi magumu ya kuchoma meli moto! Maana nimeshaona kwa hali ya maisha inavyobadilika kama nisipichangamka leo kwa hali jinsi inavyokwenda huko mbeleni ni wazi atanikimbia tu, kama noma na iwe noma, nachoma meli sasa kama ni wa kunikimbia na anikimbie hivi sasa!
4. Majirani wenzako watakupiku make ushazoea kushindana kimaisha hapo mtaani: ni kweli tumekuwa na ka ushindani wa kuangusha vipati vya komonio na ubatizo wa watoto wetu, mavazi krisimasi na iddi na kukaangiza samaki SATO, ila sasa naamua kubadilika, maana kama nisipobadilika kila kitu kitaendelea hivi hivi maisha yangu yote, kama nataka kutajirika yapasa kubadilika ili nipate matokeo tofauti! Ushindani huo ninataka niuache na wao acha wajisikie washindi ingawa mambo yangu yakienda kulingana na vision yangu najua watakuja kunikubali tu na ingawa najua nitapitia mieleka kadhaa kabla sijasimama ila najua hii ni njia ambayo wengi waliofanikiwa walipitia!
5. Kuhofia kupoteza pesa zote: nitatumia akili na maarifa pia maana pamoja na kuwa ninakwenda kuwa mjasilia mali haimaanishi niingie kichwa kichwa tu. Ila hata kama nitapoteza pesa zote lakini nitakuwa nimebadilika ki-fikra na utajiri siyo kupata pesa tu bali kuwa na mwenendo unaovuta pesa (attracting wealth) kuwa na nidhamu ya pesa na kubadilika tabia kabisa niweze kuongea, kufikiri, na kutenda kama wanavyofanya matajiri! Nimeona matajiri wengi biashara zao zinaungua moto na kuteketea kabisa lakini punde wanasimama tena na kuja juu, ni kwa sababu utajiri wao umejichimbia ndani ya vichwa vyao, wao wanawaza tofauti, mipangilio ya mambo yao ni tofauti na sisi wapokea mishahara, yaani matajiri wanafanya mambo yao tofauti na kinyume ya kila jambo vile tunafanya sisi.
6. Kuhofia lawama kutoka kwa wazazi make ulishazoea kuwatoa na sasa hutakuwa unawatoa kwa wingi kama zamani: hawa wazazi wangu ndiyo kichocheo cha mimi kutafuta zaidi ili nisiwatoe kwa kuwapeleka out Coco beach pekee sasa nataka niwapeleke hadi Hawaii, kama niliweza huko nyuma ninajiamini nitaweza kwenda hatua kubwa zaidi! Itabidi wanivumilie tu.
7. Kuhofia kupoteza washikaji wa mtaa ambao mlikuwa mnabadili viwanja kila siku: ni kweli nimekuwa na washikaji ila hivi sasa nataka kubadili maisha yangu, washikaji kama ilivyo kwa mke wangu watakaonikimbia tutakutana mbele, nachoma meli!!
8. Kazini kwangu watanishaangaa sana na kuniona kama nimechanganyikiwa vile: kwa kweli nakubali kila mtu kazini hatanielewa, kila mtu atacheka kwa vile mshahara wangu kwa sasa umeshakuwa mkubwa sana, nimechoka kupimiwa pesa kwenye kijiko, nimeshapiga mahesabu pesa ninayolipwa kwa sasa ni kidogo sana ukilinganisha na ninachokiona mbele ya safari! Ninajiamini ninaweza kusimama na ninajua nitapata kipato kikubwa sana kuliko hiki cha sasa!! Ninakwenda kufanya jambo ambalo ndiyo fani yangu na nitahama na wateja na utaalamu na uzoefu niuhamishie kwenye ishu zangu. Kwa vile wao hawaelewi ninachokiona acha waendelee kunishangaa na kunicheka!! Ninajiamini kuwa mimi sifikiri kama wao ninachokiona mimi wao hawakioni!! Inawezekana wameridhika na wanachokipata acha wacheke tu.
9. Nilikuwa napiga sana misere na gari la ofisi sasa itanibidi niwe na piga mguu au kupanda Toyo: Yees ni kweli gari la ofisi lilinipa tafu na umaarufu sana. Ila gari la ofisi kwa sasa linanikera sana, nimeona wakubwa wangu wa kazi wanastaafu hawana gari shauri ya kubweteka na vya kazini. Gari la ofisi linaniletea kelele sana na majungu mengi! Siwezi kujivunia gari la ofisi, likionekana bar napigwa majungu, nikibebea majani ya ng'ombe inakuwa kesi, nisipompa mtu lift inakuwa masimango, gari la ofisi si la kujivunia!! Sasa hilo gari ndiyo imekuwa Fimbo ya kunitishia, oh tumekupa gari tunataka uchape kazi ukiwa mzembe tutampa mwingine, ooh toka tukupe gari siku hizi hutulii, ohh tumekupa nyumba ukizembea tutakunyang'anya looooh!!! Changu ni changu nitanunua tu, nachoma moto meli mie.......