Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

mkuu umetisha sana!
how 2 get capital ndo tatizo
Juma WALEO capital si tatizo, kinacho tusumbua ni udhubutu, hapo ndo kuna taabu mkuu, Capital kubwa kuliko zote ni Sprit uliyo nayo, Unaweza fika mbali sana endapo utakuwa kweli na dhamira ya kufanya hivyo, Watu wengi walianza bila mitaji na sasa wako mbali sana, Mtaji mkubwa ni afya yako, ni akili uliyo pewa na mwenyezi mungu na kazalika
 
Last edited by a moderator:
JamiiForums ni Chuo kikuuu! nilishapata shahada ya II[Uzamili] JF...kwa kusoma Minakasha iliyonitanua Akili, kiujasiriamali, biashara, kisiasa, kiuhusiano, Mapenzi, kiteknolojia, kiafya, Dini, kijamii, Katiba na Elimu.

Naendelea kutanua Akili ili nipate shahada III[Uzamivu]
Iwa mwema
Wakatabahu
Adharusi
 
Kazini kwetu kuna mdada na mpongeza sana. Kagundua kua, migahawa ya kazini hapa inatengeneza chakula cha aina moja tu na ambacho baadhi ya watumiaji hawakipendi. Basi kila siku asubuhi anaingia katika gari la wafanyakazi na aina tofauti ya vitafunywa, basi anazichanga kuliko watu wengi wanavyo dhania. Asante mkuu kwa kutufumbua macho
 
Shida siyo mtaji ni ujuzi na mawazo,kuna biashara ambazo unapoanza unaanza na mtaji wa nguvu yako kwanza.na hata hivyo zipo biashara ambazo mitaji yake ni midogo sana ambapo itakuwezesha kusave na kugain mitaji mikubwa baadae.kwa ushauri wa aina gani ya biashara wasiliana na mimi.
 
Nawaza sana nifanye biashara gani, kwani mshahara wangu nilianza kujengea nyumba ambayo itatumia zaid ya mil20. Nataka nistopishe ujenzi nianze biashara. Take home ni around tsh laki nne. Nipeni wazo wakuu.
 
Hii mada imekuja wakati husika maana ni mwezi wa kwanza nimeacha kazi na kuamua kutumia ujuzi nilionao kua mjasiriamali. Sitarajii kuajiriwa tena nimeamua kupambana mpaka kieleweke. Uoga wako ndo umasikini wako.
 
Back
Top Bottom