Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Nampa pole yake binafsi Kuna sehem nilikuwa nafanya biashara kama hiyo shida ilikuwa mtaji

Naenda sehemu kufanya kazi za vibalua ili nipate mtaji lengo nikienda kariakoo nichukue mzigo wa kutosha

Nilifunga biashara miezi 3 nitafuta mtaji nikapata mtaji wa kutosha

Nilifungua na bidhaa ya kutosha nikawa siuzi hamnaa

Shida Sasa ikaja kwa wanunuzi
Je Kuna wengine wanafany biashara kama hiyo? Pia hapo unafunzo wewe ulifunga biashara kwa muda wa miezi 3, swali je wateja wakusubiri wewe upate mtaji Tena umewatoroka jibu hapo ni wasingelikusubiri walipata chimbo jingine Tena labda kwa bei nafuu zaidi kufunga biashara ni njia moja wapo ya kuwa mbali na wateja
 
IDEA ya Biashara ni moja ya mambo yanayo waumiza watu wengi sana, Na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kuja na wazo lenye tija kwako na kwa jamii nzima.

HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA

1. TUMIA UJUZI ULIO NAO

Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, why usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari why usianzishe gereji yako?

Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza nay a kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya na kwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe

2. BADILISHA HOBBY YAKO KUWA PESA
Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, kama wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga mbwa?

Kama Hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usinzishe mabwawa ya kuogelea na wengine wakawa wankuja huko kuogelea?

Kam unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya landscape gardening.

3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYARI IPO
Ukishindwa kabisa kupa wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua nu kuendelea nayo

4. KUNUNUA FRANCHISE
Hii ni moja ya njiza zinazo tumika kwa sasa na sehemu nyingi sana, Unaweza nunua Popular Brand na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna mashariti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brandi yenyewe, nah ii ni popular sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA MENGINE.

Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa Taarifa make inaweza kula kwako na ukajikuta unafilisiwa.

Na ilisha wahi kutokea kwa Kampuni ya Mabasi ya SABENA baada ya kutimia jina la Shirika la Ndege la Ubeligiji, Ila sijui walimalizana vipi, make jamaa bado wanalitumia

5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu unakuta either ni Mrembo sana, Handsome na kazalika, unaweza utumia huo urembo na uhendsaamu kufanya biashara, either za marketing na kadhalika.

6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenum au maeneo unayo enda kustarehe.

-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
- Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?

7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.

8. TUMIA TEKNOLOJIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara.

9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI NYINGINE WANAHITAJI NINI?
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kadhalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi.

10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza

11. ANGALIA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna chaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, hata TBC huwa ina makala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango w akutosha kwa wewe kupata wazo la biashara

12. COPY BUSINESS IDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copy idea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika

13. TUMIA NJIA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA BIASHARA
  • Maonyesho ya biashara
  • Magazeti,
  • Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
  • Kwa marafiki.

14. UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikio kwako

SO HIZO NI MOJA YA NJIA ZA KUTUMIA, INGAWA BADO KUNA NJIA NYINGI TU ZA KUFANYA ILI KUPATA WAZO LA BIASHARA LILILO BORA

********

Influenza SAID:
Kuchagua wazo la biashara ni hatua ngumu na muhimu sana. Watu wengi hawafanikiwi kwenye biashara zao kwa kuwa wanakosea katika hatua hii. Uchaguzi sahihi wa wazo la biashara ni msingi muhimu katika kufikia malengo ya biashara yako.

Ikiwa unataka kuanza biashara, basi karibu nikushirikishe mambo 5 ambayo unapaswa kuyazingatia kabla ya kuchagua wazo la biashara.

Chagua wazo unalolipenda
“Fanya kile unachopenda na pesa zitakufuata.” Kanuni mojawapo ya kufanikiwa katika kile unachokifanya ni kwa kupenda kile unachokifanya. Unapochagua wazo unalolipenda ni wazi kuwa utalifanya kwa moyo na kwa ufanisi mkubwa hata kama utakutana na changamoto.

Hivyo, usichague wazo kwa sababu fulani amelichagua au linampa faida kubwa mtu mwingine; kwako linaweza kuwa gumu na lenye hasara kubwa.

Chagua wazo unalolifahamu na kulimudu
Watu wengi hufanya kosa la kuchagua wazo la biashara ambalo hawalifahamu vyema au kulimudu. Hii ni kutokana na kuiga, kukosa ubunifu au hata tamaa ya pesa.

Kumbuka ili wazo lifanikiwe ni lazima litekelezwe na mtu anayelifahamu vyema na kulimudu. Kwa mfano unaanzisha biashara ya hoteli huku ukiwa huna maarifa wa ujuzi wowote kuhusu uendeshaji wa hoteli; ni wazi kuwa hutoweza kufanikiwa.

Zingatia swala la fedha
Kila biashara inahitaji fedha ili kujiendesha. Hivyo hakikisha wazo la biashara unalolichagua utaweza kupata fedha za kutosha ili kulitekeleza.

Lifahamu wazo vyema kabla ya kuamua kulifanyia kazi, fahamu gharama zote zinazohitajika katika kulitekeleza pamoja na faida itakayopatikana. Kwa njia hii utaweza kufanya maamuzi bora zaidi kama wazo linafaa au la.

Angalia uhitaji wa soko
Watu wengi hawafahamu umuhimu wa kuangalia uhitaji wa soko kabla ya kuchagua wazo la biashara. Unapoangalia uhitaji wa soko ni wazi kuwa utachagua wazo la biashara ambalo litauzika.

Usichague tu wazo kwa sababu ni wazo au wengine wanalifanya, bali hakikisha wazo lako linahitajika sokoni katika wakati husika.

Ushindani
Ushindani ni jambo muhimu ambalo kila mtu anayechagua wazo la biashara anatakiwa kulizingatia, kwani kufanikiwa kwenye biashara kunategemea kiwango cha ushindani na jinsi utakavyokabiliana nacho.

Hakikisha unafahamu vyema ushindani kwenye wazo husika na unaweza kuumudu vyema. Hakuna haja ya kuchagua wazo ambalo unashindana na makampuni yaliyoenea ulimwenguni kote wakati wewe ni mjasiriamali unayeanza..

Kama nilivyoeleza hapo awali, uchaguzi wa wazo la biashara unahitaji utulivu na umakini mkubwa. Ni muhimu ukahakikisha kuwa wazo unalolichagua unalimudu vyema na linaweza kukupa faida ya uhakika katika eneo unalolilenga.

Usichague wazo kwa kuwa wengine wamelichagua au wengine linawapa faida; bali chagua lile linalokufaa wewe na mazingira yako.
Asante sana Mkuu
 
Mkuu ni kweli kabisa kwamba Mitaji ni Tatizo, Ila si kwa kiwango tunacho taka kuaminishwa, wewe kama Entrepreners ni lazima pamoja na mambo mengine uwe na Mbinu za kupata mitaji, na tatizo lina kuwa mitaji kwa sababu tuna penda kufanya biashara kubwa sana kitu ambacho ni ndoto, mtu anataka aingie kwenye biashara na amfikie Mengi au jamaa wa Azam, sio rahisi,

Nchi kama Kenya wapo watu wanoenda hata Kupiga Debe ilimuradi wapate mitaji, wapo wanao enda kufanya vibarua vya kufyeka ilimuradi wapate mitaji, Je ulisha wahi jaribu hivyo na kukosa mtaji? AU unataka mtaji wa Milioni 100?

Tatizo tunataka kuanzia juu wakati wenzetu wote waliaznia chini na kufika hapo walipo sasa ingawa iliwachuku miaka mingi,

so ni vizuri kuanza na ulicho nacho, na kusonga mbele kwa sababu maswala ya mitaji yatakukuta mbele ya safari na si kusibiri mtaji ndo safari ianze, kwa sababu hata kama kuna sehemu Mikopo au mitaji inatolwe wanao pewa kipaumbele wa kwanza ni ambao tiyali walisha anza na si ambao wana mawazo
Safi sana💯 hii imepiga kwenye mshono wa kuelewa tumeelewa
 
Mimi nawaza kufanya biashara ya mahitaji ya nyumbani nikiwa na mtaji wa 1.5m, location mjini. Je,Niko sahihi? Naomba ushauri wenu jamani
Kitu cha kwanza bi lazima uijue hiyo biashara pili uwezo wako wa kupata taarifa na kuzichakata kwa mtizamo chanya tuanzia hapo karibu kwa maswali
 
Naomba nitofautiane kidogo na wewe Mkuu. Kwa mtazamo wangu sio LAZIMA uijue hiyo biashara bali usahihi ni kwamba ni advantage kwako ikiwa utakuwa unaijua biashara unayotaka kuifanya.
Kimsingi na kwa kutumia kauli ambayo sio ya kukatisha tamaa wajasiriamali wapya ni kuwa, unaweza ukaingia ktk biashara hata kama hauijui ila ukawa na unajifunza ukiwa tayari ndani yake. Huko ndiko kunaitwa kuVenture.
 
If you do not know where you are going any road or path will take you there

Usipo jua uendako je nikweli utapotea? Jibu ni ndiyo, kwasababu hiyo ni lazima uijue hiyo biashara unayotaka kuifanya kwa kupata taarifa sahihi

Njia sahihi ya kupata taarifa sahihi ni kufanya utafiti wa soko na mpango wako wa biashara ili uweze kufanya biashara shindani bila kufanya utafiti huwezi kuandika mpango mzuri wa biashara

Nasisitiza kitaalamu ili ufanye biashara shindani ni lazima uwe na andiko la mpango wa biashara nafahamu kwamba biashara nyingi zinafanyika bila kuwa na mpango wa biashara na si kweli kwamba hao wanao anzisha biashara hizo bila mpango wa biashara hukosa akili za kuchunguza soko na ushindani ulivyo kabla ya kuanzisha hiyo biashara

Baadhi ya faida za mpango wa biashara:

1. Kufanya makosa kwenye makaratasi

2. Kabla ya kufungua mlango wa biashara yako utakuwa unalijua soko lako pamoja na washindani wako hata wateja

3. Mpango mzuri wa biashara unaweza kukuongoza nini kifanyike kuhusu upungufu wa mtaji na kukosa uzoefu

4. Ni rahisi kujirekebisha na kusahihisha mapungufu katikati biashara, (you can make adjustments)
 
🧺 Je, biashara ya kufua nguo (laundry) ni rahisi kuanzisha kwa mtu mwenye mtaji mdogo?

Jibu ni ndiyo kwa mtazamo wa Bizmtaa, na si rahisi tu inaweza kuwa fursa kubwa ya mapato ikiwa itapangwa vizuri. Watu wote wanahitaji nguo safi, lakini si kila mtu ana muda au vifaa vya kufua, kukausha, na kupiga pasi. Miji na vitongoji vyenye shughuli nyingi vina idadi kubwa ya wateja wanaotafuta huduma hizi kila siku.

Kwa nini inaweza kuanzishwa na mtaji mdogo?
✅ Vifaa vya kuanzia vinaweza kuwa vya bei nafuu – Unaweza kuanza na mashine moja au mbili za kufulia za kiwango cha nyumbani, pasi ya umeme, na vifaa vya kusafisha.
✅ Huduma ya "pick-up & delivery" hupunguza gharama ya eneo – Badala ya kupangisha duka ghali, unaweza kuendesha huduma ya kuchukua na kupeleka nguo nyumbani kwa wateja.
✅ Soko la ndani ni tayari – Wanafunzi, wafanyakazi wa ofisi, familia kubwa, na wageni wa muda wote ni wateja wakuu.
✅ Uwezo wa kuongeza hatua kwa hatua – Unaweza kuanza kwa kiwango cha chini na kupanua taratibu kadri faida inavyoongezeka.

Changamoto na suluhisho
✅ Changamoto kuu ni ushindani na ubora wa huduma. Suluhisho ni kutoa huduma bora, kuwasiliana vizuri na wateja, na kutumia mbinu za kuvutia kama punguzo kwa wateja wa mara ya kwanza au kifurushi cha wateja wa kudumu.
✅ Kutumia mitandao ya kijamii na mawasiliano ya moja kwa moja (WhatsApp groups) kunaweza kukuletea wateja bila gharama kubwa za matangazo.

Hapa ndipo eBook yangu inakusaidia ya laundry service. Nimeandaa mwongozo wa vitendo utakaoonyesha:
✅ Hatua kwa hatua jinsi ya kuanza huduma ya laundry ukiwa na mtaji mdogo.
✅ Namna ya kupata wateja wa mara ya kwanza na kuwageuza kuwa wateja wa kudumu.
✅ Mikakati ya kupunguza gharama na kuongeza faida.
✅ Ubunifu wa huduma—kama "express service", punguzo kwa wanafunzi, au vifurushi vya familia.

💡 Fikiria hivi:
Kila mfuko wa nguo chafu una thamani ya pesa kwa mtu mwenye mpango sahihi. Ukiwa na maarifa yaliyopangwa vizuri kutoka kwenye eBook yangu, unaweza kuanza huduma yako ya laundry kesho, hata kama una mtaji mdogo, na ukaipanua hatua kwa hatua hadi ikawa biashara kubwa. nimekuekea muongozo wa kupata ebook hii kwenye link hii EBOOK:Huduma ya Kufua Nguo (Laundry Service) from Bizmtaa on WhatsApp.
 
IDEA ya Biashara ni moja ya mambo yanayo waumiza watu wengi sana, Na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kuja na wazo lenye tija kwako na kwa jamii nzima.

HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA

1. TUMIA UJUZI ULIO NAO

Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, why usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari why usianzishe gereji yako?

Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza nay a kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya na kwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe

2. BADILISHA HOBBY YAKO KUWA PESA
Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, kama wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga mbwa?

Kama Hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usinzishe mabwawa ya kuogelea na wengine wakawa wankuja huko kuogelea?

Kam unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya landscape gardening.

3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYARI IPO
Ukishindwa kabisa kupa wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua nu kuendelea nayo

4. KUNUNUA FRANCHISE
Hii ni moja ya njiza zinazo tumika kwa sasa na sehemu nyingi sana, Unaweza nunua Popular Brand na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna mashariti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brandi yenyewe, nah ii ni popular sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA MENGINE.

Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa Taarifa make inaweza kula kwako na ukajikuta unafilisiwa.

Na ilisha wahi kutokea kwa Kampuni ya Mabasi ya SABENA baada ya kutimia jina la Shirika la Ndege la Ubeligiji, Ila sijui walimalizana vipi, make jamaa bado wanalitumia

5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu unakuta either ni Mrembo sana, Handsome na kazalika, unaweza utumia huo urembo na uhendsaamu kufanya biashara, either za marketing na kadhalika.

6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenum au maeneo unayo enda kustarehe.

-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
- Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?

7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.

8. TUMIA TEKNOLOJIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara.

9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI NYINGINE WANAHITAJI NINI?
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kadhalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi.

10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza

11. ANGALIA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna chaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, hata TBC huwa ina makala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango w akutosha kwa wewe kupata wazo la biashara

12. COPY BUSINESS IDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copy idea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika

13. TUMIA NJIA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA BIASHARA
  • Maonyesho ya biashara
  • Magazeti,
  • Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
  • Kwa marafiki.

14. UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikio kwako

SO HIZO NI MOJA YA NJIA ZA KUTUMIA, INGAWA BADO KUNA NJIA NYINGI TU ZA KUFANYA ILI KUPATA WAZO LA BIASHARA LILILO BORA

********

Influenza SAID:
Kuchagua wazo la biashara ni hatua ngumu na muhimu sana. Watu wengi hawafanikiwi kwenye biashara zao kwa kuwa wanakosea katika hatua hii. Uchaguzi sahihi wa wazo la biashara ni msingi muhimu katika kufikia malengo ya biashara yako.

Ikiwa unataka kuanza biashara, basi karibu nikushirikishe mambo 5 ambayo unapaswa kuyazingatia kabla ya kuchagua wazo la biashara.

Chagua wazo unalolipenda
“Fanya kile unachopenda na pesa zitakufuata.” Kanuni mojawapo ya kufanikiwa katika kile unachokifanya ni kwa kupenda kile unachokifanya. Unapochagua wazo unalolipenda ni wazi kuwa utalifanya kwa moyo na kwa ufanisi mkubwa hata kama utakutana na changamoto.

Hivyo, usichague wazo kwa sababu fulani amelichagua au linampa faida kubwa mtu mwingine; kwako linaweza kuwa gumu na lenye hasara kubwa.

Chagua wazo unalolifahamu na kulimudu
Watu wengi hufanya kosa la kuchagua wazo la biashara ambalo hawalifahamu vyema au kulimudu. Hii ni kutokana na kuiga, kukosa ubunifu au hata tamaa ya pesa.

Kumbuka ili wazo lifanikiwe ni lazima litekelezwe na mtu anayelifahamu vyema na kulimudu. Kwa mfano unaanzisha biashara ya hoteli huku ukiwa huna maarifa wa ujuzi wowote kuhusu uendeshaji wa hoteli; ni wazi kuwa hutoweza kufanikiwa.

Zingatia swala la fedha
Kila biashara inahitaji fedha ili kujiendesha. Hivyo hakikisha wazo la biashara unalolichagua utaweza kupata fedha za kutosha ili kulitekeleza.

Lifahamu wazo vyema kabla ya kuamua kulifanyia kazi, fahamu gharama zote zinazohitajika katika kulitekeleza pamoja na faida itakayopatikana. Kwa njia hii utaweza kufanya maamuzi bora zaidi kama wazo linafaa au la.

Angalia uhitaji wa soko
Watu wengi hawafahamu umuhimu wa kuangalia uhitaji wa soko kabla ya kuchagua wazo la biashara. Unapoangalia uhitaji wa soko ni wazi kuwa utachagua wazo la biashara ambalo litauzika.

Usichague tu wazo kwa sababu ni wazo au wengine wanalifanya, bali hakikisha wazo lako linahitajika sokoni katika wakati husika.

Ushindani
Ushindani ni jambo muhimu ambalo kila mtu anayechagua wazo la biashara anatakiwa kulizingatia, kwani kufanikiwa kwenye biashara kunategemea kiwango cha ushindani na jinsi utakavyokabiliana nacho.

Hakikisha unafahamu vyema ushindani kwenye wazo husika na unaweza kuumudu vyema. Hakuna haja ya kuchagua wazo ambalo unashindana na makampuni yaliyoenea ulimwenguni kote wakati wewe ni mjasiriamali unayeanza..

Kama nilivyoeleza hapo awali, uchaguzi wa wazo la biashara unahitaji utulivu na umakini mkubwa. Ni muhimu ukahakikisha kuwa wazo unalolichagua unalimudu vyema na linaweza kukupa faida ya uhakika katika eneo unalolilenga.

Usichague wazo kwa kuwa wengine wamelichagua au wengine linawapa faida; bali chagua lile linalokufaa wewe na mazingira yako.
 
Mimi naujuzi wa kuondoa neno au kuweka neno kwenye documents au kuweka saini ya mtu kwenye documents hata kama hayupo ilimladi tu unioneshe hiyo niiweke kwenye documents. Mfano labda unataka saini kwenye documents fulani ya baba au mama au yeyote yule lakini hayupo naweza kukuwekea aini yake.je ujuzi huu naweza kuutumia wapi?
 
Mkuu unatafuta jinai. Na kwa jinsi hawa jamaa walivyo na hasira kipindi hiki...
 
Back
Top Bottom