Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Ya mkuu ni wewe tu, Watu engi uoga tulio nao uko ktika sehemu hizi

1. Kuchekwa
2. Kudharauliwa mtaani,
3. Kuhofia kama ukiflisika mpenzi wako unaye mpeda sana atakula kona,
4. Majirani wenzako watakupiku make ushazoea kushindana kimaisha hapo mtaani
5. Kuhofia kupoteza pesa zote
6. Kufofia lawama kutoka kw wazazi make ulishazoea kuwatoa na sasa hutakuwa unawatoa kwa wingi kama zamani,

7. Kuhofia kupoteza washikaji wa mtaa ambao mlikuwa mnabadili viwanja kila siku,

8. Kazini kwangu watanishaangaa sana na kuniona kama nimechanganyikiwa vile,

9. Nilikuwa napiga sana misere na gari la ofisi sasa itanibidi niwe na piga mguu au kupanda Toyo,

UKIYAZINGATIA HAYA HAKIKA, UJASIRIAMALI SI SEHEMU YAKO, NA HUTAWEZA KAMWE
Mkuu naomba ushauri mimi nimeanzisha biashara ya kuuza vifaa vya simu japo vichache kama earphone,headphone,charger ,battery ndogo za simu cover za simu japo ni chache na vingine japo baadhi tu ni hayo sasa leo siku ya 4 lakin sijapata mteja hata mmoja toka nifungue sasa kwa mawazo yangu ya haraka haraka nataka nianze kutembeza mtaani japo nipate chochote je haya mawazo yakoje mkuu ,naomba ushauri wako
 
Ni kweli mitaji ni changamoto kubwa sana kwa tulio wengi,
Lakini hiyo siyo sababu yenye mashiko kwa mtu Anaetaka kuwa mjasiriamali(mfanya biashara)

Shida kubwa tulizo nayo Watanzania wengi ni uvivu wa kutumia hobi zetu, tunachokipenda ni kuangalia Fulani anafanya biashara fulani na inamuingizia kipato basi nae anaenda kufungua biashara ileile tena eneo hiloholo analofanyia alie muona anafanya hiyo biashara

Ni afadhari uige biashara lakini ukafungue eneo lingine,

Jamani tubadilike watoto wa mama SAMIA, tusiige tu biashara bila kuzifanyia uchinguzi,

Ukiona mwenzio anauza Nguo za kike wewe Uza viatu, hapo tutaweza kutokomeza umaskini
Tumejawa na wivu na roho mbaya
 
Mkuu naomba ushauri mimi nimeanzisha biashara ya kuuza vifaa vya simu japo vichache kama earphone,headphone,charger ,battery ndogo za simu cover za simu japo ni chache na vingine japo baadhi tu ni hayo sasa leo siku ya 4 lakin sijapata mteja hata mmoja toka nifungue sasa kwa mawazo yangu ya haraka haraka nataka nianze kutembeza mtaani japo nipate chochote je haya mawazo yakoje mkuu ,naomba ushauri wako
Fanya hivo kiongozi, ingekuwa vzuri na hapo dukan unamuacha mtu.. nahuko mtaani pia unawadirect hapo dukan ili wajue dukan kwako pia
 
Upo sahihi kabisa biashara nzuri ni ile inayotokana na hobbie yako na kile unachokipenda kwa 100% hapo utaifanya kwa moyo na upendo na itadumu na itasonga mbele halikadhalika itakuletea mafanikio hata ikiwa kwa kuchelewa kidogo
 
Sahihi mkuu , ila namba 5 unataka kusemaje hapo😄😄
 
Umesomeka mkuu, Mawazo ya biashara yapo mengi kama ulivyojaribu kuonesha, shida yetu kuu ni mitaji ya uhakika.

Historia haiishiwi wino.
Mtaji siyo jambo la msingi, wazo la biashara ndiyo msingi. 1. Taarifa za kina kuhusu hiyo biashara kama ni bidhaa uwe na taarifa za kutosha kuhusu bidhaa pia kama ni huduma unatakiwa uwe na ufahamu wa kutosha kuhusu hiyo huduma utakayo uza, 2. Angalia rasilimali zinazo kuzunguka ama ulizo nazo zinaweza kutumika kama mtaji, (jamaa, ndugu, marafiki), 3. Andiko la biashara, hutokana na utafiti wa kina kuhusu wazo lako la biadhara kumbe ukiwa na andiko zuri la biashara linaweza kuziba pengo la kutokuwa na mtaji ama uzoefu wa hiyo biashara, andiko ama mchanganuo wa mradi inasadia kufanya makosa kwenye makaratasi badala ya kuyafanya kwenye biashara
 
Mimi nawaza kufanya biashara ya mahitaji ya nyumbani nikiwa na mtaji wa 1.5m, location mjini. Je,Niko sahihi? Naomba ushauri wenu jamani
 
Mimi nawaza kufanya biashara ya mahitaji ya nyumbani nikiwa na mtaji wa 1.5m, location mjini. Je,Niko sahihi? Naomba ushauri wenu jamani
Kwa uelewea wangu inawezekana na ni mtaji mzuri sana. Ila kabla ya kuanza kaangalie kwanza eneo unalotaka kufanyia kazi mahitaji, na wauzaji wengine wanafanyaje ili usijekuharikiwa mbeleni
 
Mkuu ni kweli kabisa kwamba Mitaji ni Tatizo, Ila si kwa kiwango tunacho taka kuaminishwa, wewe kama Entrepreners ni lazima pamoja na mambo mengine uwe na Mbinu za kupata mitaji, na tatizo lina kuwa mitaji kwa sababu tuna penda kufanya biashara kubwa sana kitu ambacho ni ndoto, mtu anataka aingie kwenye biashara na amfikie Mengi au jamaa wa Azam, sio rahisi,

Nchi kama Kenya wapo watu wanoenda hata Kupiga Debe ilimuradi wapate mitaji, wapo wanao enda kufanya vibarua vya kufyeka ilimuradi wapate mitaji, Je ulisha wahi jaribu hivyo na kukosa mtaji? AU unataka mtaji wa Milioni 100?

Tatizo tunataka kuanzia juu wakati wenzetu wote waliaznia chini na kufika hapo walipo sasa ingawa iliwachuku miaka mingi,

so ni vizuri kuanza na ulicho nacho, na kusonga mbele kwa sababu maswala ya mitaji yatakukuta mbele ya safari na si kusibiri mtaji ndo safari ianze, kwa sababu hata kama kuna sehemu Mikopo au mitaji inatolwe wanao pewa kipaumbele wa kwanza ni ambao tiyali walisha anza na si ambao wana mawazo
kwer kaka mitaji itukute tumesha anza safari
 
Kamuzu,

Kwama Peremende si Biashaa? Biashara ni kuuza magari na kazalik? wapo walioanza na mafunfu mawili ya Mchicha na kwa sasa hivi wanaongea story zingine kabisa,

Watu tunakosa focus ndo maana unatuona tunauza sigara au pipi stendi miaka nena rudi, ni kukosa focus na si kingine kile

Wachina tunao walalamikia kwmba wanakuja kufanya biashar za uchuuzi si wajinga kabisa, wana tageti mbali sana sisi tunaakia kulaumu wakati kutembeza bidhaa kwnewe hatutaki,

Juzi nilikuata na jama mmoja huku Arusha ametokeakenya na Graduate, anatembeza madawa fulani ya kienyeji mtaani, kwa kukusanya watu na kunaza kuwaelezea madhara ya sijui Soda, na kazalika na mwisho wa siku anawauzia madawa, jamaa nilijaribu kumtafuta baada ya hp kwa kweli alinielezea lengo lake ndoto zake ni zipi,

Kwa kifupi sisi tutabaki kulaumu serikali mara wachina wanakuja kufanya umachinga mara sijui imepanda ikashuka wakati wenzetu wanacheza na furusa

Ok mkuu wewe tafuta mtaji wa mabilioni ili uanze iasharami
 
Mkuu naomba ushauri mimi nimeanzisha biashara ya kuuza vifaa vya simu japo vichache kama earphone,headphone,charger ,battery ndogo za simu cover za simu japo ni chache na vingine japo baadhi tu ni hayo sasa leo siku ya 4 lakin sijapata mteja hata mmoja toka nifungue sasa kwa mawazo yangu ya haraka haraka nataka nianze kutembeza mtaani japo nipate chochote je haya mawazo yakoje mkuu ,naomba ushauri wako
Watambue mafundi Ndiyo wanaweza kununua vipuli, (spare), jitambulishe kwao, hata hivyo kabla ya kuanza hiyo biashara ilitakiwa uwatambue kwanza wateja wako ni wakina nani
 
Watambue mafundi Ndiyo wanaweza kununua vipuli, (spare), jitambulishe kwao, hata hivyo kabla ya kuanza hiyo biashara ilitakiwa uwatambue kwanza wateja wako ni wakina nani
Nampa pole yake binafsi Kuna sehem nilikuwa nafanya biashara kama hiyo shida ilikuwa mtaji

Naenda sehemu kufanya kazi za vibalua ili nipate mtaji lengo nikienda kariakoo nichukue mzigo wa kutosha

Nilifunga biashara miezi 3 nitafuta mtaji nikapata mtaji wa kutosha

Nilifungua na bidhaa ya kutosha nikawa siuzi hamnaa

Shida Sasa ikaja kwa wanunuzi
 
Back
Top Bottom