Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Mkuu naomba ushauri mimi nimeanzisha biashara ya kuuza vifaa vya simu japo vichache kama earphone,headphone,charger ,battery ndogo za simu cover za simu japo ni chache na vingine japo baadhi tu ni hayo sasa leo siku ya 4 lakin sijapata mteja hata mmoja toka nifungue sasa kwa mawazo yangu ya haraka haraka nataka nianze kutembeza mtaani japo nipate chochote je haya mawazo yakoje mkuu ,naomba ushauri wako
 
Tumejawa na wivu na roho mbaya
 
Fanya hivo kiongozi, ingekuwa vzuri na hapo dukan unamuacha mtu.. nahuko mtaani pia unawadirect hapo dukan ili wajue dukan kwako pia
 
Upo sahihi kabisa biashara nzuri ni ile inayotokana na hobbie yako na kile unachokipenda kwa 100% hapo utaifanya kwa moyo na upendo na itadumu na itasonga mbele halikadhalika itakuletea mafanikio hata ikiwa kwa kuchelewa kidogo
 
Sahihi mkuu , ila namba 5 unataka kusemaje hapo😄😄
 
Umesomeka mkuu, Mawazo ya biashara yapo mengi kama ulivyojaribu kuonesha, shida yetu kuu ni mitaji ya uhakika.

Historia haiishiwi wino.
Mtaji siyo jambo la msingi, wazo la biashara ndiyo msingi. 1. Taarifa za kina kuhusu hiyo biashara kama ni bidhaa uwe na taarifa za kutosha kuhusu bidhaa pia kama ni huduma unatakiwa uwe na ufahamu wa kutosha kuhusu hiyo huduma utakayo uza, 2. Angalia rasilimali zinazo kuzunguka ama ulizo nazo zinaweza kutumika kama mtaji, (jamaa, ndugu, marafiki), 3. Andiko la biashara, hutokana na utafiti wa kina kuhusu wazo lako la biadhara kumbe ukiwa na andiko zuri la biashara linaweza kuziba pengo la kutokuwa na mtaji ama uzoefu wa hiyo biashara, andiko ama mchanganuo wa mradi inasadia kufanya makosa kwenye makaratasi badala ya kuyafanya kwenye biashara
 
Mimi nawaza kufanya biashara ya mahitaji ya nyumbani nikiwa na mtaji wa 1.5m, location mjini. Je,Niko sahihi? Naomba ushauri wenu jamani
 
Mimi nawaza kufanya biashara ya mahitaji ya nyumbani nikiwa na mtaji wa 1.5m, location mjini. Je,Niko sahihi? Naomba ushauri wenu jamani
Kwa uelewea wangu inawezekana na ni mtaji mzuri sana. Ila kabla ya kuanza kaangalie kwanza eneo unalotaka kufanyia kazi mahitaji, na wauzaji wengine wanafanyaje ili usijekuharikiwa mbeleni
 
kwer kaka mitaji itukute tumesha anza safari
 
 
Watambue mafundi Ndiyo wanaweza kununua vipuli, (spare), jitambulishe kwao, hata hivyo kabla ya kuanza hiyo biashara ilitakiwa uwatambue kwanza wateja wako ni wakina nani
 
Watambue mafundi Ndiyo wanaweza kununua vipuli, (spare), jitambulishe kwao, hata hivyo kabla ya kuanza hiyo biashara ilitakiwa uwatambue kwanza wateja wako ni wakina nani
Nampa pole yake binafsi Kuna sehem nilikuwa nafanya biashara kama hiyo shida ilikuwa mtaji

Naenda sehemu kufanya kazi za vibalua ili nipate mtaji lengo nikienda kariakoo nichukue mzigo wa kutosha

Nilifunga biashara miezi 3 nitafuta mtaji nikapata mtaji wa kutosha

Nilifungua na bidhaa ya kutosha nikawa siuzi hamnaa

Shida Sasa ikaja kwa wanunuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…