Hello Tanzanians!
Kwa vijana mliosoma IT & Computer science mnaweza mkatengeza Mobile Software Application (Mobile App) nzuri ambayo itakayoweza kutoa huduma na wewe mtengenezaji ukawa Controller wa hiyo huduma.
Mfano, ukaamua kutengeneza Mobile App ya huduma ya Car Parking Spaces kwa mkoa wa Dar es Salaam yote. Mtu ambaye aidha ni mwenyeji au mgeni katika jiji hilo ataweza kuweka oda ya parking ya gari au chombo chake cha usafiri ili asikose mahali pakuhifadhi usafiri wake na hii itasaidia kuongeza usalama kuwa mkubwa na kutengeneza ajira za kutosha.
Ushauri wa tozo: Kula 10% ya mteja (customer) na 10% ya mwenye huduma (Space owner) au kinyume chake.
Mifano ya huduma nyingine;
1. Uuzaji wa vyakula vya bei nafuu (migahawa badhifu yenye bei isioumiza).
2. Huduma ya choo na bafu
3. Kumbi za harusi na sherehe
4. Kumbi za starehe na bar
5. Nyumba za kulala wageni classic ila bei isioumiza.
6. Maduka yenye kutoa huduma ya bidhaa mbalimbali masaa 24 siku 7 za wiki (24/7).
7. Vibanda vya huduma ya chipsi safi, kongoro, supu mkia wa mbuzi, makange nk
8. Sehemu zenye watu watoa huduma za ucheshi nk
9. Car wash
10. Vehicles parking
11. Sehemu ya kupumzika yaani open space free charge area nk
12. Utajiongeza na wewe
Haya mawazo hayahitaji mtaji zaidi ya Tsh. 50,000/=. Kijana msomi kazi ni kwako.
Kuhusu soko ni mkoa uliopo na wilaya zake hii inaitwa kutembelea nyota.
Karibu "wauza mawazo ya biashara"
Sent using
Jamii Forums mobile app