Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Linachofugwa na nani?Cha buku kisungura
Linachofugwa na nani?Cha buku kisungura
Vita vya uchumiView attachment 3644574
Sekta ya vinywaji vya kilevi ya Tanzania inakabiliwa na usumbufu katika soko la Rwanda baada ya mamlaka za udhibiti nchini Kigali kusitisha kwa muda uagizaji wa bidhaa na kuagiza kurejeshwa sokoni kwa aina 14 za bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania.
Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda (Rwanda FDA) ilitangaza hatua hiyo tarehe 5 Agosti 2026 kama sehemu ya hatua pana za udhibiti zilizolenga jumla ya aina 52 za vinywaji vya kilevi vinavyotoka Tanzania, Uganda, Kenya, India, Burundi na Poland.
Bidhaa kutoka Tanzania zilizoorodheshwa ni pamoja na Konyagi, Strong Dry Gin, Diamond Rock Gin, Tzee Lemon and Ginger, Kiwingu Spirit, K-Vant, Blackhat, Campfire Gin, Cuca Vodka, Hanson’s Vodka, Relax Vodka, Tzee Portable Spirit na X5 Gin. Diamond Rock Gin imeonekana mara mbili katika kiambatisho cha mamlaka hiyo ikiwa na maelezo yanayotofautiana kidogo kuhusu mtengenezaji.
Bidhaa hizo zinatengenezwa na Tanzania Distilleries Limited, Mati Super Brands Limited, East African Spirits Tanzania, Serengeti Breweries Limited, Kilimanjaro Biochem Limited, Mega Beverages Limited na John Beverages Tanzania Limited.
Konyagi, ambayo ni mojawapo ya chapa zinazotambulika zaidi za pombe kali nchini Tanzania, ni miongoni mwa bidhaa zilizoathiriwa.
Rwanda FDA ilisema uamuzi huo umechukuliwa “kwa maslahi ya afya ya umma,” ingawa taarifa yake haikubainisha sababu maalum za kiusalama, ubora au masuala ya udhibiti yanayohusiana na kila bidhaa. Mamlaka hiyo iliongeza kuwa orodha nyingine ya bidhaa zilizoathiriwa itatolewa kadri utekelezaji wa hatua hizo utakavyoendelea.
Kwa mujibu wa agizo hilo, waagizaji wanapaswa kuanzisha mara moja zoezi kamili la kurejesha bidhaa na kuwaelekeza wasambazaji kuziondoa bidhaa zilizoorodheshwa kutoka kwa wateja wao. Bidhaa zote zilizopo sokoni pamoja na zile zitakazorejeshwa zinapaswa kurudishwa kwa waagizaji.
Waagizaji pia walipewa siku tatu za kazi tangu kutolewa kwa tangazo hilo kuwasilisha ripoti za zoezi la kurejesha bidhaa. Wakati huo huo, wasambazaji na wauzaji wa rejareja wameagizwa kusitisha mara moja uuzaji wa vinywaji vilivyoathiriwa, huku watumiaji wakishauriwa kuacha kuvitumia.
Kuna pombe inatwa smatgin na ingine kisungura sio sungura kufugwaLinachofugwa na nani?
Kagame akiondoka wataendelea na huo ustaarabu?Kagame yuko serious sana na Raia wake wa Rwanda.
Anaanza kuwafunza Ustaarabu ni nini.
Kigali imekua clean city.
Kupanda daladala nchini Rwanda ni kwa Ustaarabu sasa. Hakuna kusukumana kama wabongo wa daladala za mbagala.
Hakuna kupanda boda mshkaki.
Wanyarwanda wana elekea Ustaarabu wa kuwa binadamu timamu wenye akili kama wazungu.
Haswaa.Rwanda ina kila strategies za kulinda raia wao kimipaka na kiafya. Nationalism na uzalendo uko juu sana.
Sio Tz ukisikia “tunalinda raia dhidi ya mambo mabaya “ ujue kuna kikundi cha wanasiasa kinalindwa, mnalindaje Raia wakati kuna bidhaa feki kila kona na nchi yetu? Ujasusi wa kiuchumi upo kwenye dustbin.
Konyagi inagongwa copy sana aiseeKonyagi wameionea....!!!!
Nakubaliana na wewePengine ili taifa liwe na watu wenye akili timam lazima lipitishwe kwenye Vita vikali sana, na sio maigizo ya vita vya Uganda na Idd amin.
Eeeh ndio washushe bei sasa🙏🙏🙏Mopak njoo uone huku konyagi ilichofanyiwa rwanda....
Safi sana RwandaView attachment 3644574
Sekta ya vinywaji vya kilevi ya Tanzania inakabiliwa na usumbufu katika soko la Rwanda baada ya mamlaka za udhibiti nchini Kigali kusitisha kwa muda uagizaji wa bidhaa na kuagiza kurejeshwa sokoni kwa aina 14 za bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania.
Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda (Rwanda FDA) ilitangaza hatua hiyo tarehe 5 Agosti 2026 kama sehemu ya hatua pana za udhibiti zilizolenga jumla ya aina 52 za vinywaji vya kilevi vinavyotoka Tanzania, Uganda, Kenya, India, Burundi na Poland.
Bidhaa kutoka Tanzania zilizoorodheshwa ni pamoja na Konyagi, Strong Dry Gin, Diamond Rock Gin, Tzee Lemon and Ginger, Kiwingu Spirit, K-Vant, Blackhat, Campfire Gin, Cuca Vodka, Hanson’s Vodka, Relax Vodka, Tzee Portable Spirit na X5 Gin. Diamond Rock Gin imeonekana mara mbili katika kiambatisho cha mamlaka hiyo ikiwa na maelezo yanayotofautiana kidogo kuhusu mtengenezaji.
Bidhaa hizo zinatengenezwa na Tanzania Distilleries Limited, Mati Super Brands Limited, East African Spirits Tanzania, Serengeti Breweries Limited, Kilimanjaro Biochem Limited, Mega Beverages Limited na John Beverages Tanzania Limited.
Konyagi, ambayo ni mojawapo ya chapa zinazotambulika zaidi za pombe kali nchini Tanzania, ni miongoni mwa bidhaa zilizoathiriwa.
Rwanda FDA ilisema uamuzi huo umechukuliwa “kwa maslahi ya afya ya umma,” ingawa taarifa yake haikubainisha sababu maalum za kiusalama, ubora au masuala ya udhibiti yanayohusiana na kila bidhaa. Mamlaka hiyo iliongeza kuwa orodha nyingine ya bidhaa zilizoathiriwa itatolewa kadri utekelezaji wa hatua hizo utakavyoendelea.
Kwa mujibu wa agizo hilo, waagizaji wanapaswa kuanzisha mara moja zoezi kamili la kurejesha bidhaa na kuwaelekeza wasambazaji kuziondoa bidhaa zilizoorodheshwa kutoka kwa wateja wao. Bidhaa zote zilizopo sokoni pamoja na zile zitakazorejeshwa zinapaswa kurudishwa kwa waagizaji.
Waagizaji pia walipewa siku tatu za kazi tangu kutolewa kwa tangazo hilo kuwasilisha ripoti za zoezi la kurejesha bidhaa. Wakati huo huo, wasambazaji na wauzaji wa rejareja wameagizwa kusitisha mara moja uuzaji wa vinywaji vilivyoathiriwa, huku watumiaji wakishauriwa kuacha kuvitumia.
Kwenu kuna mamlaka au viraka...Huku kwetu mamlaka hazijaona hilo watu wanazifakamia kwa nguvu zote
Nani achukue hatua..unaongea km umekatwa kichwa? Yupo wa kuchukua hatua nchi hii..muwe mnatakafari mambo kwanza kabla ya kutamka..Hili jambo lisipoingizwa siasa, pombe feki ni nyingi mno hata Tanzania mamlaka zichukue rhatua.
Back to square one.Kagame akiondoka wataendelea na huo ustaarabu?
Je nchi yetu inawathamini raia wake?Safi sana Rwanda
Samia usimuite pimbi. Sema hhoja zakoUyo pimbi tu
Hiyo copy inakuwa ndio kali zaidi ama inakiwa oya oya kwamba mtu anaweza kutumia hata zile bapa kubwa kabisa mbili au tatu?Konyagi inagongwa copy sana aisee