Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Kuna baya gani katika nchi njirani kupiga marufuku uingizaji wa pombe zisizotengenezwa kwa viwango? Serikali ya Kagame iko makini sio sisi hapa Tanzania tunameza tu kila kitu kinachoingizwa nchini kwa sababu kinaletwa na wafanya biashara ambao wana connection ya wanasiasa.Ila kila baya linalohusu Tanzania unasherekea?
Hata kama ni upinzani sio kwa kila kitu jamani heh🙌
Juice za Azam watu walitoa ushahidi jinsi zilivyo na kiwango cha juu cha sumu, hadi kwa nyaraka za Umoja wa Mataifa zikatumika, lakini TBS wakawatetea. Haukufanyika hata uchunguzi wa hizo tuhuma na hadi leo watu wanabugia tu sumu za AZAM katika juice. Kwa sababu AZAM ni ndugu moja na CCM na mtu wa Zanzibar sivyo? Kwa hiyo unataka Kagame awe kiongozi wa aina ya huyu wa kwetu?