Baadhi ya viongozi hawana sifa za kuongoza

Baadhi ya viongozi hawana sifa za kuongoza

Makumu wa raisi akihutubia kongamano la vijana hapo jana amesema kwamba tatizo kubwa kwenye nchi hii ni kuwa na wimbi kubwa la vijana wenye tamaa ya kupata utajiri wa haraka.
Amewataka vijana kuwa wazalendo na wawajibikaji Kwan hatma ya taifa hili IPO mkononi mwao .
Samaki huonza kuanzia kichwani au masikioni
 
Magu ndio mtu pekee ambae angeweza kuleta maendeleo ya kweli kwenye nchi hii.

Huo ndio ukweli.

African tuna safari ndefu sana.
 
Amewataka vijana kuwa wazalendo
Uzalendo kwa nchi za Africa ni dhana ngumu sana. Mtu akiangalia connections zote wanapewa watoto wa vigogo/wakubwa mpaka scholarships alafu leo umuimbishe wimbo wa uzalendo ili aje kudhalilika uzeeni??
 
Achana na huko juu, Yani Huku CHINI serikali za mitaa kwa MAANA ya watendaji wa kata na Miata ndo Kuna kilio, pameozaa Hawa hawaujui dhamana zao na WANAIKOSANISHA SERIKALI na WANANCHI wao... Sijui kwanini mabadiliko hayafanyiki. Kama hakutakuwa na mkeka mpya Huku chini (serikali za mitaa) ambalo ndio Kila siku wanakutana na wananchi sijui itakuwaje 24/25
Sisi tunaokutana nao hawa WEOs na VEOs tunajua taabu tunazopata.
Yaani mara nyingi inabidi tugeuke kuwa waalimu kuwafundish vile wanapaswa kutenda majukumu yao.

Ni hawana kitu wanajua kabisa kwa wengi wao kwa kweli.
Kama Wilaya ya Mkuranga nimekutana na issue ya hovyo sana.
Nina shida na WEO wa Kata fulani,nafika ofisini kwake saa 3 mpaka saa 6 mtu hajafika.

Kumpigia simu,anasema kwa nini sikumjulisha mapema kuwa leo nitakuwa nina shida naye! Nikamuuliza ile ofisi maana yake nini,anasema yeye anafanya kazi kiteknolojia (kwa simu).
Fikiria mimi ni muwekezaji ndio nafanyiwa hivyo kama nataka hisani vile.
Yeye anaishi km 30 toka ofisi yake ilipo,yaani anaishi nnje ya Kata yake umbali wa km 30.
Haendi ofisini mpaka apigiwe simu.

Kwa kweli huu mnyororo wa viongozi wabovu ni kuanzia chini mpaka juu, na nimeushuhudia mwenyewe huku Mkuranga,Kibiti,Rufiji na Kilwa.
 
Serikali yetu inapitia Changamoto pia ya Kuwa na Viongozi ambao hawajui dhamana yao, kazi zao, wajibu wao, lengo la kuwa eneo hilo.

Hawajui namna ya kuishi na Raia ambao 2025 utarudi tena kwao kuomba kura🤔🤔🤔

Nape Nnauye ndio namba moja wao kati ya viongozi wajinga.
Ni nchi gani inaongozwa na akina saa100 africa na imefanikiwa?

Isije ikawa tunajaribu kitu tusichokijua!!
 
Back
Top Bottom