... sekta ya kilimo inahitaji mkakati wa kipekee kweli kweli. Ni aibu taifa leo linaagiza ngano, sukari, na mafuta ya kula. Serikali iwekeze kwenye mashamba makubwa yaliyotelekezwa miaka na miaka; vifaa vya kisasa vipelekwe huko; wataalamu waajiriwe huko plan iwe miaka mitano ijayo marufuku kuagiza ngano; miaka 8 marufuku kuagiza mafuta ya kula; miaka 10 marufuku kuagiza sukari badala yake tuwe tuna export.
Tutakuwa tumeokoa mabilioni ya dola yanayotumika kuagiza vyakula hivyo; tutakuwa tumetengeneza ajira kwa watu wetu; tutakuwa tunapata fedha za kigeni kwa kuuza nje. Uwezo wa rocket science hatuna basi hata kujitosheleza kwa ngano? Aibu!