Baadhi ya wadada huwa mnawapoteza watu wa kuwasaidia sababu ya njaa zenu

Baadhi ya wadada huwa mnawapoteza watu wa kuwasaidia sababu ya njaa zenu

Wakuu people's
Yale majizi 👉 kidumu

Aisee nilikwenda duka moja kupata huduma nikamkuta mdada mmoja tukazungumza hapa na pale nikaomba namba basi tukaanza mawasiliano na nikamuweka wazi kwamba nimempenda na akanielewa.

Akaanza kunishirikisha mambo yake kwamba alikuwa na mume wametengana sababu mumewe hamataki tena na ameoa mke mwingine na alimtesa sana.

Hapo dukani kaajiliwa tu na anaishi kwa bosi wake nikaamuliza wanakulipa shs ngapi akasema elfu 40 nikamwambia si mbaya sn sababu anaishi kwa bosi wake.

Nikamshauri kama kweli anania ya kusonga mbele basi anatakiwa apange room yake mi tamsaidia kodi ya miezi mitatu na baadhi ya vitu kama godoro akasema sawa ngoja ajipange.

Nikapata wazo nyumbani kwangu kuna vitu kibao vya kufanyia biashara kama ya chips au mama ntilie nk nikawaza atakapokuwa tayari kupanga room nimfungulie biashara mojawapo ili aachane na hiyo kazi ya kulipwa elfu 40 kwa mwezi hili skumgusia ili nilimwambia kama anaweza kufanya biashara akasema anaweza kabisa.

Sasa kilichonileta hapa ni kwamba siku moja usiku tukiwa tuna-chat akasema ooh hana amani nikamuuliza kwanini akajibu ooh mama yake amekabwa na watu wasiojulikana na wamenyang'anya kila kitu pamoja na pesa ya kikundi na anatakiwa alipe pesa za watu 😀 na yeye ndo wa kumsaidia kuilipa mi nikawapa pole kisha nikamwambia utawezaje kulipa hiyo hela kwa mshahara huo sasa akasema hata hajui afanyaje mi nikamwambia bnafsi siwezi kumsaidia hilo ukizngatia ndo kwanza tumeanza mahusiano kisha nikalipotezea hilo.

Zikapita kama siku 2 tukawa tunawasiliana vzuri tu sasa juzi namsalimia ananambia ooh leo hata sijui takula nn nikamuuliza kwann akajibu ooh hela ya mboga ameisahau nyumbani na hapo hana hela ya mboga 😀 mkumbuke alinambia anaishi kwa bosi wake. Mi nikamuliza ww ulisema unaishi kwa bosi wako sa mambo ya mboga na wewe wapi na wapi wakati wewe mambo hayo hayakuhusu unaishi kwenye mji wa watu.

Akasema kwani kakosea kuniambia nikamjibu hapana ila mi ninashangaa unaishi kwa bosi halafu wewe ndo unatakiwa utoe hela ya mboga 🤣. Hilo nikalipotezea akili ikakaa sawa kwamba huyu mdada hamna kitu anataka kunivuna tu hakuna jipya hapo nikamblock na nikaachana naye.

Sasa enyi wadada wakati mwingine mpunguze njaa na vibomu visivyo na kichwa wala miguu aisee mnapoteza watu wa muhimu sana kwenu wa kuwatoa hatua 1 kwenda nyingine ila njaa zenu zinawaponza sana. Huyu nilikuwa na nia ya kumsaidia kabisa ila kwa upuuzi huo wa kujaribu kunipiga vibomu nani anaweza wanaweza mambwiga tu.

NB: wale wanaoona eti namind vihela vidogo kama hivyo ni wao na akili zao tu mimi hata shs 50 ina thamani kubwa maana kwenye bil 1 ukitoapo shs 50 tayari siyo bil 1 tena.

Je, wakuu maamuzi yangu ni sahihi au si sahihi.🤔
Subiri vibamia na washamba wa mapenzi waje kukushambulia sasa
 
Sasa nimejitoa akili kwanini?
Hilo ni swali niliuliza kama unaamini analipwa 40k wewe unaleta mambo ya kushukuru nina pa kuamkia.
Mtu anakudanganya mambo ya kitoto sana ndo maana ninakuuliza umeamini analipwa 40k kwa mwezi?
Kwanini asiamini kwani unamjua uyo dada? Unajuaje kama kamdanganya? Sio kila kazi watu wanafata mshahara kuna kazi zingine hakuna cha maana wanacholipwa lakini wanaishi kwa kutegemea viujanja janja fulani tu hapo hapo kazini mfano mabaamedi.
 
😂😂😂 ndio, sasa ww huoni hapo km kuna tatizo? Huyo anajimwambafai anataka kumpa maisha binti, binti naye kaanza kuleta changamoto zake. Lkn matokeo yake jamaa kala kona. Halafu amtoe mwenzie kwenye duka akamfungulie banda la chipsi kweli?? Hapo ni yeye alitaka apate kupiga free P huku anajichukulia posho za kwenye chipsi. Huyo binti alikuwa anaenda kupoteza.
Wewe unauzaje P?
 
Kwanini asiamini kwani unamjua uyo dada? Unajuaje kama kamdanganya? Sio kila kazi watu wanafata mshahara kuna kazi zingine hakuna cha maana wanacholipwa lakini wanaishi kwa kutegemea viujanja janja fulani tu hapo hapo kazini mfano mabaamedi.
namfahamu mtoa mada na jambo analoliongelea
 
Kwanini uwe na mawazo ya kumsaidia mwanamke?. Wanawake washaweka wazi kwa maneno na vitendo ya kwamba kwao mapenzi ni fursa ya kifedha, sasa kwanini wanaume bado hamtaki kuelewa na kujitoa mkifikiri mnapendwa?. Tafuta mwanamke ambae tayari ana vigezo unavyovitaka kama unataka mke msomi tafuta ambae tayari kashasomeshwa na wazazi wake, kama unataka mke mwenye biashara tafuta ambae tayari ana biashara yake achaneni na huu ujinga wa kusomesha au kufungulia biashara wanawake. You have to know the hypergamous nature of women, their love is opportunistic. Women don't love men they love value. Understand the game.
 
Kwa hiyo unatafuta pesa ili uwape hata watu wajinga na wapuuzi km huyo msichana au unatafuta pesa kwa ajili ya maendeleo
Msemo wa "tafuta hela" mara zote unatumika kuhamasisha utafutaji wa hela ili ufanye mambo ya kipuuzi especially starehe au ngono, ndio maana wanaoendekeza huo msemo nawaonaga ni watu fulani wajinga jinga
 
Uhalisia ni kuwa hukua muhimu kwake, pesa yako ndo ilikuwa muhimu na pesa anaipata kupitia uongo uongo. Tangu day 1 alikutazama kama fursa ya kujipatia chochote kisha upite zako.

Labda useme wanawake wadangaji waboreshe janja janja zao ili usiwashtukie mapema wavune zaidi.
 
Kati ya watu nisiowapenda ni wale mnawakuta wenzenu wapo kwenye ajira za watu mnaanza kuwarubuni,mwisho wa siku mnawaharibia sana mabosi wenye biashara na nyumba binafai kutafuta mabinti wengine.

Mtu unafahamu ndoa ilishamshinda nawe bichwa gumu unajipeleka hapo kisha unakuja kujaza lawama mtandaoni aiseee
 
Sisi wanaume tuko hivi mwanamke tunampima kulingana na matendo yake kwenye mahusiano either ni wakupita au kujenga nae maisha jamaa kampenda huyo manzi in really baada ya matendo ya huyo dada ndio imemfanya achange gia angani
Nakujibu kesho leo nimechoka
 
Unavosema kuwa "namtumia mwanamke" unamaanisha nini? Mimi Ku-sex na mwanamke inamaanisha namtumia?

Kwani kwenye sex huyo mwanamke hapati raha? Au huyo mwanamke hanitumii kupata raha? Kama Mimi ninavomtumia kupata raha? Lamomy
Wanapenda sana kujifanya victim. Sex ni mutually pleasure wala hawatufanyii favour yoyote kiasi cha kutaka tuwalipe
 
Unavosema kuwa "namtumia mwanamke" unamaanisha nini? Mimi Ku-sex na mwanamke inamaanisha namtumia?

Kwani kwenye sex huyo mwanamke hapati raha? Au huyo mwanamke hanitumii kupata raha? Kama Mimi ninavomtumia kupata raha? Lamomy
Na wewe ntakujibu kesho, huu muda naingia kwenye maombi.
 
Mwamba ulitaka umpe vifaa vya chips au mama ntilie na mzigo awe anakupa unajipigia akashtuka,
 
Jambo la msingi kuliko lote, kwa muda wako woteeee mpaka mnachat usiku wa manane. Ulifanikiwa kambani ? Au ulikuwa unasubiria kodi ya miezi mitatu ijae ukaloekee utakapolipa kodi ww
 
Sina pesa ya kumpa bali ninayo ya kumfanya apate pesa yake mwnyw za kupewa kwangu hazipo mfundishe mtu kuvua samaki na uumpe namna ya kuvua akavue mwnyw kuliko ww ukavue na kumpa siku ukiwa haupo itakuwaje.
sahihi broo maana leo utampa kesho anarudi tena
 
Ulikutana na kausha damu pro, huyo ni aina ya wanawake ambao wanaamini kupewa/kupokea/kutatuliwa matatizo yao(yakiwemo ya kipuuzi) ni jukumu la lazima la wewe mwanaume as long as umeonesha nia ya kuwa nae kwenye mahusiano. Halafu mbaya zaidi hata shukrani hawanaga, siku ukiacha tu kutimiza hayo utakutana na maneno ya shombo.... na wakati wewe unafanya hayo yote unakuta kuna kijana wa ovyo hapo mtaani kwao anambinua anavyotaka bila kumsaidia chochote.
Point
 
Back
Top Bottom